Subaru forester, naipenda sana, nipeni moyo niinunue tafadhali.

inategemea wewe kawaida unaitafsiri vipi. mimi gari ya kawaida ni kama toyota spacio/raum/rav4 na jamii hio linapokuja suala la gari kama Subaru/Mitsubishi Evo siiweki kwenye magari ya kawaida.

Evo hii ndio inapiga chafya!!!?????
 
Comment za watu zinatuvuta sana kununua subaru forester
 
Evo hii ndio inapiga chafya!!!?????

hahahahaha ile chafya hata IMPREZZA inapiga,sauti ile inatoka kwenye BOV-BLOW OFF VALVE....nimeiba maelezo yaliyonyooka kutoka wikipedia kidogo hapo chini

A blowoff valve (BOV), bypass valve or dump valve is a pressure release system present in most turbocharged engines. Its purpose is to prevent compressor surge, and reduce wear on the turbocharger and engine. Blowoff valves relieve the damaging effects of compressor "surge loading" by allowing the compressed air to vent to the atmosphere, making a distinct hissing sound, or recirculate into the intake upstream of the compressor inlet.
 
Ndugu subaru forester sikushauri maana nimeitumia sana..spare zake ni ghali sana na upatikanaji ni shida pia..niligongwa na toyo taa ya mbele niliitafuta arusha sijapata saba general stores hata dar nliagiza sijapata mpaka nikaipata nairobi tena used kwa milioni 1 na laki 6...sikushauri ununue forester ndugu
 
inategemea wewe kawaida unaitafsiri vipi. mimi gari ya kawaida ni kama toyota spacio/raum/rav4 na jamii hio linapokuja suala la gari kama Subaru/Mitsubishi Evo siiweki kwenye magari ya kawaida.

huyu anataka forester, hii gari ya kawaida sana huwezi kuiweka kundi la evo, viwango vya evo ni wrx ambayo bei yake haiwezi.
 

hahaaa, ilikuwa mwaka gani hiyo? kweli watu mnaumizwa, wajanja kama wewe mkuu?!!! spare zipo kibao dar sku hizi, ukiona wanakuzingua unaagiza.

hii hapa laki350 mpaka mlangoni kwako
View attachment 149955
 

Kaka nimekuelewa sana...inaelekea ww mdau sana wa rally cars
 
uko sahihi, lakini ndiyo ilikuwa yangu ya kwanza, tena pickup.

umetoka mbali,salute gari yangu ya kwanza ni 1995 peugeot 405sri....nilikuwa nakimbia na hii gari mpaka sasa hivi nikikaa najiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini???lakini nagundua ni ujana tu na irresponsibility.
 
umetoka mbali,salute gari yangu ya kwanza ni 1995 peugeot 405sri....nilikuwa nakimbia na hii gari mpaka sasa hivi nikikaa najiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini???lakini nagundua ni ujana tu na irresponsibility.

lol, ukosahihi mkuu, kuna umri wa mchezo!
 
ndio subaru impreza na mitsubishi evo huwa zinapiga chafya ukibadili gear.....ni blow off valve inatoa compressed air nje ya turbo unit.....inafanya kama malori ya zamani yale mafiat

Shukrani mkuu!
 
Ukisha nunua usubiri wajukuu waje waione hutouza kamwe ni ndowa ya kikristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…