Subaru Forester Vs Mazda CX5

Subaru Forester Vs Mazda CX5

Hakika Tutafute Hela Kaka [emoji119][emoji119][emoji119]
Nje iyo design wao wanaiita Kodo design or Soul of Motion. Ilianza kwenye izo CX5 sahivi imesambaa kwenye lineup nzima ya Mazda.

Ndani wamechukua interior ya Mazda 6 (Atenza) za kuanzia 2016 aisee. Unyama sana .

View attachment 2938472

Mkuu, hii ni CX5 aisee. Sasa kuna vyuma vinaitwa CX50, CX9 na CX90.

Aisee tutafute hela sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio habari ya mjini Kwa wale wapenda magari mazuri

Hizi ni gari shindani kwa sababu zote zipo kundi moja la COMPACT SUV.

Zinafanana sifa katika utendaji kama vile:

1. Ukubwa wa umbo
2. Nafasi kubwa ndani
3. Ground clearance nzuri
4. Nguvu ya kutosha kustahimili
changamoto za barabara
ngumu

Baadhi ya Tofauti ambazo zinaweza kukusaidia kuchagua kati ya SUBARU FORESTER na MAZDA CX5 ni kama vile:
1. Muonekano, macho
yanatofautiana kila mtu ana
Upendeleo binafsi kati ya
Muonekano wa FORESTER na
MAZDA CX5

2. Matumizi ya mafuta, MAZDA
CX5 nyingi ni Diesel na
zinakwenda mpaka 18KM/L
wakati FORESTER ni Petrol na
zinakwenda 14KM/L. Kuhusu
utofauti wa injini ya Petrol na
Diesel unaweza kurejea somo
hilo lipo humu

3. Upatikanaji wa vifaa na
mafundi, Japo gari zote hazipo
kwa wingi sana, lakini subaru
ipo kwa wingi na hata vifaa ni
vingi na mafundi wapo wengi
pia kulinganisha na MAZDA
CX5

4. MAZDA CX5 zilizo nyingi ni
Non-Turbo lakini zinakuwa na
nguvu kubwa kuliko
FORESTER NON-TURBO (XS)
FORESTER XT inazalisha
nguvu kubwa zaidi kuliko
MAZDA NON-TURBO. Lakini
MAZDA CX5 TURBO inazalisha
nguvu kubwa kuizidi kidogo
FORESTER TURBO (XT)

5. Bajeti, MAZDA CX5 bajeti yake
ni kuanzia TSH 27M mpaka
TSH 30M wakati FORESTER
NEW MODEL zinaanzia TSH
25M mpaka TSH 28M lakini
pia FORESTER OLD MODEL
bajeti ni chini zaidi.

Bila shaka maelezo haya yanajitosheleza kukuwezesha kufanya Uchaguzi sahihi.
[emoji6][emoji1666][emoji1666]
View attachment 2789002View attachment 2789003
Subaru ni 4x4 kawaida
Mazda ni FWD kawaida na 4WD kama uliorder. Si lazima ukaipata ya 4WD kwa second hand
 
Nina fundi wangu mmoja ninamkubali ila anasema engine za Mazda zina changamoto sana, toka zimeanza kuingia kwa wingi hizi Mazda anasema zimeletwa kwake zaidi ya nane kwa matatizo engine tena zote namba E'! Ni kweli au hao watumiaji hawana uelewa nazo.?
Watanzania sijui wapoje aisee. Yaani eneo la kuharibu magari wapo vizuri balaa.
 
Nje iyo design wao wanaiita Kodo design or Soul of Motion. Ilianza kwenye izo CX5 sahivi imesambaa kwenye lineup nzima ya Mazda.

Ndani wamechukua interior ya Mazda 6 (Atenza) za kuanzia 2016 aisee. Unyama sana .

View attachment 2938472

Mkuu, hii ni CX5 aisee. Sasa kuna vyuma vinaitwa CX50, CX9 na CX90.

Aisee tutafute hela sana.
Sijui nimekuaje siku hizi,gari zenye gear lever hata iwe Kali vipi Sina mzuka nazo,Basi tu ni maisha.Natamani wangeweka Kama za Jaguar XF,kitu unazungusha tu P,R,N,D kama redio vile.
 
Au za RR na Disco. Hahahaa unaweza mpa mtu lift akajua cha kuongezea sauti. Mtajikuta mpo mtaroni.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we gear unaweka kama unawasha AC. Hajawahi panda gari na wale mademu wajuaji ambao akiingia kwenye gari anaanza kujiweka huru utadhani gari la baba ake.

Mara kaanza kubonyeza redio, mara aanze kuadjust AC, mara arekebishe siti yake mara aweke miguu kwenye dashboard, mara afungue draw anatafuta chaji. Sasa wa hivi ukimuingiza hizi gari za umeme ambazo gear knob ni kama switch ya AC, na Handbrake wameitengeneza kama button ya power window anaweza kukutia majanga ya mamilioni.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
𝙽𝚒𝚒𝚙𝚊𝚝𝚎 𝙵𝚘𝚛𝚎𝚜𝚝𝚎𝚛 𝚢𝚊 2016-2018 𝚝𝚞𝚛𝚋𝚘 𝚞𝚗𝚒𝚊𝚖𝚋𝚒𝚒 𝚔𝚒𝚝𝚞
 
Being ndio tatizo, hizi za 2017 zina bei iubwa kidogo. Sa chini ya hapo zina matatizo ya DPFkama zilivyo gari nyingi za Diesel za miaka ya karibuni, hasa kwa mazingira yetu ya bongo ambako diesel ni low quality, inaccurate shida nyingine ya ndogo ndogo ila ukizitibu gari inadumu. Inataka service kwa wakati na kutumia oil sahihi
Diesel za bongo low quality?
Duuh haya bhn…
 
Acha uongo 15 - 18 km per liter?

No research no right to speak..
Wenzako huwa wanabisha alafu wanaokupa na data ili kudhihirisha ukweli
Screenshot_20240704-124038.png
 
Acha uongo 15 - 18 km per liter?

No research no right to speak..
Ungesema ukweli ni upi kwa kutumia hizo data. Alichokisema huyo hajakosea kutokana na official data. Ila tu haya magari yakishakuwa yametumika huwa ni ngumu kupata hizo namba. Uzima wa gari, quality ya oil, mafuta, na mazingira huathiri hizo namba. Lakini kwa ujumla bado hii gari ikiwa nzima inakula mafuta vizuri sana ukilinganisha na gari nyingine tulizozoea bongo kama rav 4, vanguard, etc
 
Mwezi ujao nataka nihame kwenye Carina Ti na mimi niwe mtu mwenye gari kweli .

Subaru legacy 2015 na subaru forester 2013 hipi itakua nzuri zaidi bei zina tofautiana kwa 3 million
 
Back
Top Bottom