Subaru mnatufilisi, Gari zinakunywa mafuta kama zinameza!

Subaru gari ya vijana wa kiumeni itaendeshwa na wanaume tu.
 
Nadhani ulitaka kusema reliability na sio liability.
 
Mmmm Mmmmh brother unatudanganya sana ukisema Subaru inakula mafuta sasa subaru forester inatumia hadi 11km/l highway unataka itumieje? pia head gasket failure sio kama unavyoongelea ww watu wanamiliki hizo gari miaka na miaka bila shida ...unasifia mfano BMW wakati zinajulikana kwa engine problems na leakege..miliki kwanza Subaru ndio ucoment kuliko kusoma customers reviews mitandaoni na kuja ku paste hapa
 
Kuendesha Subaru tu siyo kipimo tosha cha kuielewa;Labda uniambie you are a good engineer in this perspective na mwenye ku fanya research za kutosha,just even try kuuliza car from Japan engineers au best car inspection companies wakwambie common issues za Subaru alafu uje na technical data of why am wrong.Infact hapa hatubishani Ila tunaelimishana with fact!
 
Hii ya Subaru kua na head gasket issues naiunga mkono hoja,ni kweli.
 
Nimeona Kampuni ya Nissan Japan wana advertise this car in Nigeria,I think it's so poweful based na wanavyoielezea

2018 Nissan GT-R Engine Specs
This turbocharged 3.8L V6 is capable of outputting a jaw-dropping 565 horsepowerand 467 lb-ft of torque. This engine gives you all the power you could possibly need, in a condensed and ideally sized package, making the 2018 Nissan GT-R lightweight and ready for the track.
 

Attachments

  • 35805baf2fb99cd57e5cc35eb512bd6d.jpg
    40.8 KB · Views: 24
Duuu!! Hii gari ni balaa turbocharger 3.8l si mchezo Mkuu alafu V6.
Bei yake itakuwa IPO juu Sana hata horsepower yake ni kubwa kwelikweli
 
Mkuu nafikiri unaongea tu.
Nimemiliki Subaru aina mbili tofauti SF5 na SG5 Forester.
Matatizo ya Subaru ni mafundi haba wa gari hizi na vipuri ghali sana.

Lakini hizi gari ni za high performance.

Ukisema cylinder head gasket failures huo ni uongo wa kushindwa kuimiliki gari.
Subaru ambayo ninayo sasa ni registration ya B series lakini ni game any time.

Tatizo mliozoea kutozipa service, magari haya yatawafia bure!

Nikuhadithie basi, nilisafiri miaka zaidi ya mitano iliyopita Mbeya.
Kuna VX LC100 ikanipita kwa fujo.

Nami nikalianzisha ligi, hii gari ni wazimu kwa acceleration na baada ya kufukuzana karibia kilometa 100 Ifunda~Makambako VX akakubali yaishe.

Subaru, a leader in its class.
 
Still sijaona point ya msingi uliyo argue kwenye problems identified!Upande wa mbio na nguvu unaouongelea inategemea unaifananisha Subaru na gari gani,Otherwise utabakia na sauti za Subaru yako na wenzako hutowaona!Kwenye mbio suby ni leader wa makelele tu barabaran na kwa wajapani wenzie
 
Tafuta hata ka Volkswagen GTi na Subaru uje utupe experience yako mkuu
 
Mbona hujaongelea suala muhimu lililokuibua, service ya gari husika.
Kubali tu kama una hela ndogo hilo halikufai.
 
Mbona hujaongelea suala muhimu lililokuibua, service ya gari husika.
Kubali tu kama una hela ndogo hilo halikufai.
Brother! Intelligent guys siku zote hupenda kujifunza na siyo kujiringia alichonacho even if it's pointless "knowledge is power always",Subaru corporation wenyewe wana admit hiyo problem ndiyo maana waka redisn cylinder heads na camshaft kwenye model za Subaru kuanzia 2000's and still they do undergo major changes kuondoa leakages,failure rate ya head gasket ya subaru before 2000's was very high ukilinganisha na sasa lakini still problem haijaisha;and the great source ya head gasket challenges ni boxer engine-powerful engine yenyewe ambayo huwa ina create alot of temp. inside blocks ambazo the way cylinder zilivyokuwa designed horizontal opposed zinakuwa prone na coolant system.
 
Subaru zenye turbo late ya gasket failure ni ndogo,non turbo zilikuwa na tatizo,ila fix ni gharama ya kawaida tu,unajua boxer engine zina gerate heat mno,ni gari nzuri kwa price yake,engine strong mno,ni ngumu sana kufa engine hizi gari,ila ulaji wa mafuta sio mzuri,anayekuambia anapata 11kml muhoji VIZURI, petrol ya tanzania ni low quality, wakati subaru zinataka premium fuel, kwahiyo hatupati performance na great mileage, ulaji kwa mjini dar es salaam ni 5kml to 7kml,mimi huwa napata 6.5kml kwa huu mji,haipishani sana na rav4,hawa wanaotoa mileage nzuri ya mafuta nadhani wanakosea kupima,au wako too light footed
 
Subaru ni tofauti sana na gari nyingi sababu huweza kuendesheka mazingira mengi zaidi
 
Mkuu nafikiri unaongea tu.
Nimemiliki Subaru aina mbili tofauti SF5 na SG5 Forester.
Matatizo ya Subaru ni mafundi haba wa gari hizi na vipuri ghali sana.

Lakini hizi gari ni za high performance...
Kukimbizana kiasi kikubwa inategemea na ujasiri wa dereva.

Mwezi uliopita nasafiri kwenda Arusha, kuna jamaa alikuwa anaendesha Nadia, na yeye ana kaza kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…