Mkuu watu wananua magari bila kujua matumizi yake.
Nimetumia Subaru matoleo mawili sasa, ya '98 na ya 2002.
Hizi gari hazikukopeshi, ni brilliant perfomers. Engine zake ni sports, hazikutengenezwa kubania mafuta bali ku-out perform.
Nilijaribu hilo katika mbuga za Makambako-Iringa.
Cruiser moja ilinipita kwa fujo, nami nikaamua kukanyaga mafuta.
Spidi zikifika zaidi ya 140km/hr. valves zinazibuka na kamnyama haka ka Subaru kana paa kirahisi sana hadi 180km/hr na mashine wala haipandishi temperature wakati wa high revs.
Kwa kifupi ile Cruiser nami tukawa ngoma droo hadi Iringa, na dereva mwenzangu wa Cruiser ilibidi akubali.
Hala hala lakini, kamchezo hako ni kwa wazoefu tu na pochi ikiruhusu.