View attachment 2992573
Kwa msioelewa ufanyaji kazi wa hizi submeter haya hapa maelezo mafupi.
Muhimu:
ili kuondoa changamoto za ziada ni lazima watumiaji wote wa eneo husika wafungiwe mita, sio afunge mmoja mwingine aache.
Kutoka kwenye mchoro
A- ni mita ya tanesco
B, C, na D ni submeter za kutenganisha watumiaji.
unaponunua umeme labda unit 10, ukaweka kwenye mita B (ambayo ni submeter), unit zako zitaingia kwenye mita kuu ya tanesco ambayo ni A, lakini kumbukumbu za kuingizwa unit 10 zitabaki kwenye mita B, mita C na D hazitakua na taarifa yoyote kuhusu zile unit 10 za mita B,
kwa hivyo sasa hizo submeter zote zinapowekewa umeme zitatunza kumbukumbu ya idadi ya unit zilizoingia, ila unit zote zitajikusanya kwenye mita kuu ya tanesco.
kutoka pichani submeter zimewekewa unit zifuatazo B=10, C=50, D=100
kwa idadi ya hizo unit mita kuu ya tanesco itakua na jumla ya units 160.
inapokuja kwenye kuhesabu nani katumia unit ngapi, hapa zile kumbukumbu zilizohifadhiwa na submeter husika ndipo zinapoanza kufanya kazi.
mfano mita B aliweka unit 10 tu, ila kwenye mita kuu ya tanesco kuna jumla ya unit 160, hii mita B ina uwezo kutumia unit 10 tu na si zaidi ya hapo, kwasababu ndio kumbukumbu ya units zilizoingizwa zinasomeka hivyo, kama units 10 zikiisha submeter B itakosa umeme mpaka aongeze.