Submeter za Kijanja hakuna kushea umeme tena

kaka hapo utachoka mnunuaji anapiga simu. mtu anakuambia atanunua kwa alibaba hapo haangalii gharama za usafirishajoi wake kutoka china. bado hajalipa kodi. kama anaona china ni bei rahisi akanunue tu. kama anaona tunafaidi. watanzania wengi wanapigwa kwa kutaka rahisi. bei kujua athari zake. mnunuaji hawezi kukomenti alichokomenti yule jamaa. nahisi anatumika na mapepo.
 
sasa wewe ndio mtaalamu tunakutegemea utufafanulie ndio imekuwa tumetumwa na mapepo?
Mtu sasa mtu unamwambia bei bidhaa halafu yeye anakuambia china zinauzwa 42000. kamani Asiende kununua huko china..... ? au Aagize kupitia Alibaba. ndio maana nikasema watu wengine wanatumika na mapepo. ila aliyetaka kujua nimemuelekeza... ingekuwa kila mtu anaweza kununua huko china basi Tanzania kusingekuwa na maduka.
 
mkuu, una uhakika na hili ?

maana ndicho anachopigia kelele Pdidy
Hizi meter matumizi yake yapo hivi: utanunua umeme kama kawaida na utauweka kupitia main meter.

Baada ya hapo kwa zile meter za (vending meter) utaingia online uta- login kupitia registration iliyofanywa kwa meter yako, utaenda sehemu ya manunuzi ya umeme hapa utaingiza kiasi cha pesa ulichonunulia umeme ulioungiza kwenye main meter.

Kisha baada ya hapo utaingiza kiasi cha unit ulizopata. Kisha uta-generate kupata token ambazo utatumiwa kwa ajili ya kuziingiza kwenye sub meter yako. Hizi token ni kama code za kuruhusu umeme uingie kwenye sub meter yako.

Hivyo kiasi cha umeme uliouingiza kupitia main meter kitasoma huku. Kikiisha meter yako ita- disconnect. Hivyo uta- recharge Tena baada ya kuwa imesoma 0.00 kama ulivyofanya awali. Nadhani nitakuwa nimeeleweka.
 
Hapo umenyoosha maelezo, ambaye hatakuelewa hapa mwambie alipie kuelekezwa. Haya sasa naomba ndugu mtaalamu utuwekee mawasiliano hapa ili tuweze kujua namna ya kukupata ili tupatiwe huduma.
 
Kwa maisha ya kibongo Tanesco walipaswa kuwa na suluhisho la submitter kitambo sana
Wajinga sana wale jamaa huwa wanatia hasira sana mipango yao. Lile shirika wakinipa mimi ndani ya miaka mitano nitakuwa billionaire mkubwa sana. Na raia hawata lalamika tena.
 
suppose nyumba moja tunaishi A,B na C. Kuna submeter 3. Tulichanga 10.000 baada ya wiki umeisha kwa wote. C asiponunua tukinunua wawili inakuaje? Kwake hautawaka?
Umeme utakata kwenye sub meter ambazo zimeshamaliza units zake tu ila sio ambazo bado zipo. So ukinunuliwa mpya mtaweka tu kule kwenye mita kubwa bila kumgawia huyu C sababu yeye wakwake bado upo.

Kwa kifupi hii inasaida eneo ambalo kuna wasumbufu. Wewe kama unatumia units za shilingi 10,000 kwa mwezi halafu wapangaji wenzako wasiojielewa wanatumia zaidi ya 10,000 wewe katika mchango utanunua umeme wa 10,000 na utatumia mwezi mzima bila bugudha ya kukatika kisa units zimeisha kwenye mita za wenzako sababu zako zinakuwa bado zipo kwenye main switch.
So hizi mita ni kama distribution agents wa umeme na zina control matumizi ya muingiliano ili kila mtu apate haki yake.
 
Sio lazima iwe mwenye nyumba, mnaweza wapangaji ukikubaliana nani awe na jukumu la kusimamia hilo swala.
 
Roho ya kwanini ndicho kichaka cha umasikini wa watanzania wengi.
 
Mmmh, hapo mbona ni kama physics haiapply? Mfano mimi binafsi nikitaka kufungiwa mimi kama mimi, si nitakuwa sawa na mtu anayetumia umeme wao? Kiasi kwamba umeme ukikata kwao na kwangu kwisha habari!?
Haitafaa.
 
Ni nzuri ikiwa kila mpangaji awe na yake kwa sababu mtegemea mita kuu akiwa mtata huwezi kumzuia kutumia unit zako wote mita Δ·uu ndio pilot wenu.Kama hizo submiter zingekuwa zinalupiwa kwenye input terminals ya mita kuu sawa otherwise utata utakuwepo tu labda uandaliwe na mfumo wa kum-isolate asiyechangia umeme.
 
Nyumba ina vyumba 7, mita ya Tanesko ipo 1, kwenye matumizi ya umeme 1>> Taa ya barazani. 2>> Taa ya uwani 3>> Taa ya uchochoroni 4>> Taa ya msalani.

Swali: Naweza kufunga hicho kifaa chumbani kwangu, nikanunua Luku na kuweka kwenye mita ya Tanesko, kisha nikafanya utaratibu wa kuzihamisha tokeni kwenda kwenye kifaa nilichofunga chumbani kwangu na umeme ukawa kwangu pekee bila Taa za Barazani, Uwani, Uchochoroni na Msalani kuwaka??
 
Security bulbs, taa za chooni zitakuwa na sub meter yake pia? Au yule aliyeconnected na hizo taa atafidiwa vipi? Maendeleo yana chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…