Sudan: Watu wameanza kula majani ya pori au chakula cha mifugo ili kuendelea kuishi

Sudan: Watu wameanza kula majani ya pori au chakula cha mifugo ili kuendelea kuishi

Hata nashindwa kuelewa kama wangekaa chini pamoja na kuwa na umoja kuendeleza taifa wangepungukiwa nini!?
Kuna habari nilitizama raia wanasema RSF wanatumia mercenaries wengine wanaonekana kutoka West Africa hawana huruma wao wakikuta hata mtoto wanapiga panga.
Afrika tuna matatizo sana aisee.
Shida kubwa ya sisi ngozi nyeusi ni ubinafsi...
 
Shida kubwa ya sisi ngozi nyeusi ni ubinafsi...
Ndio maana hata UN imewapuuza imeona wacha wauane tu akili ikiwakaa sawa wataacha upuuzi wao.
Hata Afrika huoni organization yeyote ikishughulika nao.
Wana ugomvi usio na kichwa wala miguu.
 
Habari: El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini nchini Sudan, umekuwa chini ya mzingiro wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) kwa zaidi ya miezi 14, hali iliyosababisha janga kubwa la kibinadamu kwa wakazi takriban 900,000.

Athari kwa Binadamu
Masoko yamekauka, bidhaa za msingi kama sukari, unga na mafuta hazipatikani au ni ghali mno. Mfano, gunia la sukari linauzwa kwa zaidi ya pauni bilioni 2 za Sudan.
Watu wameanza kula majani ya pori au chakula cha mifugo ili kuendelea kuishi.

Kutokana na ukosefu wa dawa na maji safi, milipuko ya magonjwa kama kipindupindu imeongezeka. Vifo vya kipindupindu vimeripotiwa kuwa zaidi ya 191.
Takriban asilimia 40 ya watoto walio chini ya miaka mitano wanaugua utapiamlo mkali.

Zaidi ya watu 400,000 wamekimbia makazi yao.
Misafara ya misaada ya kibinadamu hushambuliwa na wanamgambo, hali inayozuia misaada kuwafikia walioko ndani ya mji.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa RSF kusitisha mzingiro na kulinda raia, lakini hali bado haijabadilika.
RSF inaendelea kuzuia upatikanaji wa chakula, mafuta, na dawa, na hivyo kuongeza mateso kwa wakazi.




www.aljazeera.com/news/2024/6/13/un-security-council-demands-end-to-siege-of-el-fasher-in-sudans-darfur?



Shida wanazozipata ndugu zetu walioko Sudan ni kama zimesahaulika kwetu sisi na zinazungumzwa kwa uchache. Allah Awanusuru ndugu zetu hawa kutokana na mabalaa yanayowakuta na awape ushindi dhidi ya makhawaarij wa RSF.

Dah wanateseka sana ndugu zetu hawa.
 
Habari: El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini nchini Sudan, umekuwa chini ya mzingiro wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) kwa zaidi ya miezi 14, hali iliyosababisha janga kubwa la kibinadamu kwa wakazi takriban 900,000.

Athari kwa Binadamu
Masoko yamekauka, bidhaa za msingi kama sukari, unga na mafuta hazipatikani au ni ghali mno. Mfano, gunia la sukari linauzwa kwa zaidi ya pauni bilioni 2 za Sudan.
Watu wameanza kula majani ya pori au chakula cha mifugo ili kuendelea kuishi.

Kutokana na ukosefu wa dawa na maji safi, milipuko ya magonjwa kama kipindupindu imeongezeka. Vifo vya kipindupindu vimeripotiwa kuwa zaidi ya 191.
Takriban asilimia 40 ya watoto walio chini ya miaka mitano wanaugua utapiamlo mkali.

Zaidi ya watu 400,000 wamekimbia makazi yao.
Misafara ya misaada ya kibinadamu hushambuliwa na wanamgambo, hali inayozuia misaada kuwafikia walioko ndani ya mji.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa RSF kusitisha mzingiro na kulinda raia, lakini hali bado haijabadilika.
RSF inaendelea kuzuia upatikanaji wa chakula, mafuta, na dawa, na hivyo kuongeza mateso kwa wakazi.




www.aljazeera.com/news/2024/6/13/un-security-council-demands-end-to-siege-of-el-fasher-in-sudans-darfur?

Halafu utasikia mjinga mkubwa mmoja yeye ni Israel na Palestine kutwa kucha.
 
Kuna mijitu humu huwa hizi habari za migogoro ya ndani ya Afica hujidai haiwahusu ila sasa ile ya ughaibuni inawasikitisha na kuwakasirisha sana,shwaini zao na utumwa wao.
Wapo wengi watumwa wa Palestina na Israel wakati waafrika wenzao wanachinjana hapo Sudan na Congo. Ngozi nyeusi ina machungu na raia wa Gaza au Israel kuliko Sudan na Congo. Watu weusi wako hatua za kua Binadamu kamili
 
Huu upuuzi sihusikii bara la amerika ya kusini sihusikii bara la asia sihusikii bara la ulaya ni huku tu ambapo bado tumegoma kubadilika kimaisha bado tupo zama ya ujima
Wewe unadhani wafuasi wa CHADEMA wasingekuwa wastaarabu nini kingekuwa kinaendelea leo hapa Tanzania kama siyo vita...watu wanatembea kwenda mahakamani ila polisi wanawapiga na kuwateka; viongozi wao wanawekwa ndani bila sababu kila kukicha.
Wangekuwa na magruneti kwenye mabagi yao na kuanza kuwarushia mapolisi wasiyofuata utaratibu wa ukamataji.
Japo viongozi wetu hawaoni dalili, japo natambua kuwa itakuwa hivyo huko mbeleni.
Haiti ilikuwa nchi nzuri na iliyoitawala Dominica Republic....ila sasa Haiti inaomba misaada Dominica Republic kwasababu ya ujinga wa Mapolisi ba viongozi wapenda rushwa.
 
Back
Top Bottom