Sudan yakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula au hata kuwa mgogoro wa chakula mwaka 2022

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Wataalamu nchini Sudan wameonya kuwa mwaka huu nchi hiyo inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula au hata kuwa mgogoro wa chakula, na idadi ya watu wanaoathiriwa na njaa inaweza kuongezeka na kufikia milioni 18 ambayo ni asilimia 45 ya jumla ya watu wa nchi hiyo.

Mchumi wa Sudan Bw. Abdul-Khaliq Mahjoub amesema, vyanzo vikuu vitatu vinavyosababisha ukosefu wa chakula nchini Sudan ni pamoja na mgogoro kati ya Russia na Ukraine, sera za uchumi wa ndani na uzalishaji duni wa kilimo.

Amesema, inafahamika kuwa asilimia 90 ya ngano ya Sudan inatoka Russia na Ukraine, na sasa ni vigumu kupata chanzo mbadala. Nchi hiyo inakabiliwa na hatari inayoonekana kwamba haina uwezo wa kununua ngano kwa gharama kubwa.

Hivi sasa bei ya tani moja ya ngano nchini Sudan imezidi dola mia 6 za kimarekani, ambayo imekuwa asilimia 180 juu zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.
 
Hivi wanaryhusiwa kutumia majibya mto Nile
 
Kilo nzimà ya ngano iko chini ya buku jelo bado wanalia. Kumbe bei ilikuwa nzuri sana. Inamaana walikuwa wananunua ngano chini ya buku kwa kilo
 
Sisi tulishajifunza kuzoea shida toka baada ya vita na Uganda mwaka 1979 na tumekuwa na wakati mgumu kipindi chote hicho hadi leo.
Hakuna mtu anayezoea shida ila mazingira ndio yanayomfanya aishi kwenye shida
 
Back
Top Bottom