ngafu.fijo
JF-Expert Member
- Oct 3, 2015
- 1,237
- 1,099
Aiseee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lawama nyingine za kijuha hizi. Ningeuelewa huu uzi kama ungeletwa na marehemu mwenyewe kulalamika ni vipi sugu kawatelekeza hao wasanii na pindi wanampa kampani alikuwa akiwapa ujira bei gani na huo udereva walielewana sh ngapi kwa trip/mwezi maana yawezekana kabisa pengine John Walker(RIP) mwenyewe hakuipenda hiyo kazi au mkataba haukuruhusu kumfanya aendelee na hiyo kazi.Kesho tunaaga muhimbili kesho kutwa tunasafirisha kijijini kwao. Roho ya marehemu itamlilia Sugu mpaka mbele ya haki kwa kumtumia kisha kumtelekeza akistuggle sana.
Umeona eee.............mi kimya sana mkuu.Mmh, jamaa kaumia jana na tangu hyo jana yupo mahututi unaambiwa sugu kamtelekeza "tangu" aanze kuuumwa hadi anakata roho hajamtumia 'salam' za pole. Mbongo mtu hatari sana aisee.
ivi marehemu aliugua kwa muda mrefu eeehee????Kwanza kabisa natoa pole kwa wafiwa wote kwa msiba wa msanii John Walker.
Pili nasikitika kusema nasikitishwa sana na ambavyo mbunge wa Mbeya mjini Mr Sugu alivyomtelekeza John Walker kiasi aliishi maisha magumu sana mpaka kifo chake.
Mnatakiwa kufahamu John Walker, Mapacha, Mkoloni na G Solo ndio wasanii waliopigana bega kwa bega kuakikisha Sugu anaingia bungeni hiyo ni mwaka 2010. Walijitoa kwa hali na mali kuakikisha Sugu anapata ubunge. Walichangisha michango, walisimama kwenye kampeni bila malipo ili kamanda aingie mjengoni.
Baada ya kuukwaa ubunge John Walker akawa ndio dereva wake wa kwanza wa mbunge Sugu. Walishiriki nae kwenye movement nyingine ya Anti virus ambayo Sugu aliwaaminisha wenzake wanapigania maslahi ya muziki wa bongofleva. Mwisho wa siku Sugu alipppata pesa yake aliyodhulumiwa na Ruge akaenda kimya kimya kupatana na Ruge kisha mzozo ukaanzia hapo. Akawapiga chini rafiki zake wote waliojiita vinega akiwemo dereva wake John Walker akamwondoa kwenye kazi ya udereva na Walker akarudi mtaani kubangaiza kwa kazi ya ufundi wa magari na kuchomelea vyuma.
Tangia anaumwa mpaka anakata roho marehemu akuwai kupata msaada wowote wala salamu ya pole toka kwa rafiki yake kipenzi wa zamani Sugu.
Ama kweli maskini akipata...........
fanya kazi kwa bidii na ukumbuke kujiwekea akiba itakusaidia baadae,tatizo lenu vijana mnapenda starehe na mnasahau kusave salio.mkipatwa na majanga mnaanza lawama za kutelekezwa achana na tabia za utegemezi mtoto wa kiume.au na wewe ni ommy dimpoz?Sugu ana posho na mshahara zaidi ya million 10 per month kutumia mshikaji wako awe attended earlier ilikuwa ni jambo la kiutu na kiungwana ata kama alimtupa angemkumbuka japo for once.
Mkuu kweli unaamini Sugu alikuwa anawajibika kwa afya ya rafiki yake wa zamani? Umekutana na watu wangapi katika maisha yako? Unategemea ukipata shida wote waje kukusaidia? Tuache hizi tabia za utegemezi.Sugu ana posho na mshahara zaidi ya million 10 per month kutumia mshikaji wako awe attended earlier ilikuwa ni jambo la kiutu na kiungwana ata kama alimtupa angemkumbuka japo for once.
Kwa hiyo ilitakiwa awe anawalipa kila mwez aw?Issue ya kumtelekeza haioanishwi na kifo!
Hebu soma maandiko kwa makini!
Timing tu ya huyu mleta mada ndio tata, lkn context yake iko clear kabisa kuwa Sugu aliwatosa jamaa aliofight nao ili apate ubunge na miongoni mwao ni marehemu John Walker!
Mkuu unapofanya kheir kwa mtu usitegemee malipo hasa hapa duniani,kama amewasahau mwenyezi mungu anajua ukweliIssue ya kumtelekeza haioanishwi na kifo!
Hebu soma maandiko kwa makini!
Timing tu ya huyu mleta mada ndio tata, lkn context yake iko clear kabisa kuwa Sugu aliwatosa jamaa aliofight nao ili apate ubunge na miongoni mwao ni marehemu John Walker!