SITETEI KWA SABABU NI MWANAUME...
natetea kwa sababu sugu kapeleka hoja mahakamani na kaitetea na kashinda...na ndio maana kila siku kwenye masuala ya kisheria mtuhumiwa huambiwa akae kimya maana anachoongea kinaweza kutumika dhidi yake mahakamani.
NITUMIE FURSA HII kuwashauri "wanawake wengi na wanaume wachache" wanaoendeshwa na emotions badala ya kufuata uhalisia wa mambo na hasa kisheria. muambieni huyo faiza akate rufaa kupinga hukumu ya yeye kunyimwa haki ya kulea mwanae. pia aandae utetezi na ushahidi utakao tumika kuonyesha kuwa yeye ni bora na anafaa zaidi ya mh. sugu kulea huyo mtoto.
kwa mfano....aeleze vyanzo vyake vya mapato ili mahakama imuamini na kumuona anao uwezo wa kumlea mtoto asilale au kufa kwa njaa.
aeleze mahakama kuwa alivyovaa pampas alikuwa anaigiza muvi ambayo bado haijatoka na apeleke mahakamani script za hiyo muvi zikionyesha kuwa actress atavaa pampas na kushoot scene ya birthday.
pia apeleke ushahidi mahakamani kuwa hizo post anazopost kwenye mitandao ya kijamii ni strategy ya marketing na kupata public attention as wamepanga kurelease double dvd siku zijazo...asisahau ushahidi wa hayo waliyoyapanga kupeleka mahakamani kama utetezi.
kuhusu yeye kuja na tuhuma kuwa sugu ni mlevi, mvuta bange mara alimtia mimba sita ya saba ndio hiyo kazaa navyo avipeleke mahakamani na ushahidi pia....kama anazo picha za sugu anapuliza mibhange mpaka nyumba inatoka moshi kama inaungua itamsaidia kushinda kesi.
pia mumshauri akae kimya kwa miezi kama sita aende mahakamani kuomba arejeshewe mtoto sasa amekuwa na kubadilika kitabia...akae kimya kweli na hasa kwenye mitandao na mtaani wawepo mashuhuda kuwa keshabadilika...atarudishiwa mtoto wake.
asanteni kwa kunisikiza nataraji mutamfikishia ujumbe huu "TEAM FAIZA MAJANGA"