- Source #1
- View Source #1
Wakuuw
Wakuu huko mjini Facebook nimekutana na hii taarifa ya MillardAyo na Wasafi kuwa Sugu ametangaza rasmi kugombea ubunge Mbeya mjini na anaonekana Sugu mwenyewe amepost huko X, Je, ni kweli wakuu?
Wakuu huko mjini Facebook nimekutana na hii taarifa ya MillardAyo na Wasafi kuwa Sugu ametangaza rasmi kugombea ubunge Mbeya mjini na anaonekana Sugu mwenyewe amepost huko X, Je, ni kweli wakuu?
- Tunachokijua
- Joseph Mbilinyi anayejulikana zaidi kwa jina la Sugu ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho. Pia aliwahi kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kwa vipindi viwili, mwaka 2010 hadi mwaka 2020. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulimuondoa Sugu katika nafasi hiyo baada ushindi wa Tulia Akson aliyekuwa akigombea kupitia Chama Tawala CCM.
Madai yaliyoibuka hivi karibuni
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuchapishwa na Millard Ayo pamoja na Wasafi Media zikinukuu kwenye Chapisho lililodaiwa kuchapishwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kupitia mtandao wa X kuwa ametangaza rasmi kugombea ubunge Mbeya Mjini wakati huo akihoji uhalali wa ajenda ya 'No reforms No election'
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key word search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haijachapishwa na Wasafi Media pamoja na Millard Ayo.
Aidha machapisho hayo yamebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayoyatofautisha na taarifa rasmi zinazochapishwa na vyombo hivyo, Muundo wa chapisho la Wasafi sehemu ya nembo (logo) ni tofauti na nembo rasmi ya chombo hicho huku tarehe iliyotumiwa katika chapisho la Millard Ayo haina taarifa hiyo kutoka kwenye ukurasa husika.
Hata hivyo JamiiCheck imebaini kuwa chapisho lililodaiwa kuachapishwa na Sugu kupitia ukurasa wake mtandao wa X si la kweli limetengenezwa na wapotoshaji kwani halikuchapishwa kabisa katika mtandao huo.