Sugu awachana Clouds,Jay Dee na aina ya T.I.D,Barnaba

Bei Mbaya

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
2,262
Reaction score
847
7.2 Harakati za kudai haki za wasanii.
Mheshimiwa Spika,
sanaa imeendelea kufanywa mtaji wa biashara na watu wachache ambao wanatumia nguvu waliyo nayo katika jamii na uwezo wao wa kifedha katika kukandamiza maslahi ya wasanii hapa nchini. Katika harakati za kutafuta haki za wasanii hapa nchini, mimi binafsi pamoja na wasanii wengine wachache, tulianzisha harakati za kudai haki kwa kupitia programu maarufu iliyojulikana kama 'Anti Virus' chini ya 'Vinega' ikiwa na lengo na juhudi za kudai haki za wasanii dhidi ya ukandamizaji unaofanywa na wajanja wachache kwenye muziki, ambao wametumia nafasi kama njia ya kutumia mitaji yao ya fedha kuwaendesha wasanii jinsi wanavyotaka wao.

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyo kawaida, wasanii wengi walidharau jitihada zetu na kutotuunga mkono. Leo hii katika tasnia ya muziki, kuna mgogoro mkubwa uliofuka moto kati ya msanii maarufu Lady Jaydee dhidi ya wamiliki wa radio ya Clouds FM hatua iliyosababisha nyimbo za wanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama 'Bongo Flavour' kutopigwa kwa siku moja katika kituo hicho. Sasa, ukiangalia kilio cha Lady Jaydee ni kilio kilekile kilichopelekea VINEGA kuingia vitani.

Mheshimiwa Spika, kama msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, na mwenye dhamana na uchungu na tasnia ya sanaa nchini, niweke wazi kwa umma wa watanzania kuwa, tumefikia hapa tulipo si kwa kuwa na sheria kandamizi tu bali pia kwa kukosekana kwa umoja wa wasanii nchini. Wakati tukiwa na juhudi za kutetea maslahi ya watanzania kupitia Anti Virus, ni wasanii wachache ambao walituunga mkono na wengi wao wakibeza jitihada zetu, wakiwemo hawa ambao leo wanalalamika kuwa wananyonywa haki zao. Wengine walifikia hatua ya kusema kuwa tumepewa fedha ili kuzima harakati tulizozianzisha.

Mheshimiwa Spika,
Umoja wa wasanii hasa wa muziki wa kizazi kipya nchini, unasimamiwa na chombo halali kinachojulikana TUMA-‘Tanzania Urban Music Association', lakini kutokana na ujanja wa watu wachache, waliudhoofisha umoja huu kwa kuanzisha kampuni iliyosajiliwa kama TFU- ‘Tanzania Flavour Unit' iliyowalaghai wasanii kuwa ni muungano wa wanamuziki wa Bongo Fleva na kuhodhi majukumu ya TUMA ambacho ni chama halali cha kusimamia wanamuziki wa Bongo Fleva. Mpaka tunapoongea leo hii, hata Studio iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi, bado ipo katika mikono ya TFU pamoja na Serikali kuamuru irudishwe katika mikono ya Serikali ili ikabidhiwe kwa wasanii wote chini ya chama halali cha TUMA. Sasa tunataka wasanii wote nchini waache uoga na unafiki na wajiunge na vyama vyao halali ili viwatete haki zao.

Mheshimiwa Spika,Kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa utetezi wa haki za wasanii kwa kuwa wanaotuhumiwa kunyonya haki za wasanii wameweza kutajirika na kuneemeka kwa kupitia jasho na mgongo wa wasanii. Hawa hawa wanaotuhumiwa kuhujumu wasanii ndio wanatumia nafasi yao kuupotosha ukweli wa tuhuma dhidi yao. Wanatumia fedha na rasilimali walizo nazo katika kunyanyasa wasanii, kuwakandamiza, kuwapokonya haki zao na kuwadhalilisha kuwa bila wao, wasanii wasingekua kitu.

Mheshimiwa Spika, Leo hii wasanii wanaishi kwenye hali ngumu, umasikini mkubwa lakini bado wanatolewa maneno ya kashfa na dharau na Serikali imeendelea kukaa kimya. Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kuacha siasa kwenye kutatua migogoro ya taifa hili. Siasa zimetumika sana katika kuzima jitihada za wanyonge kwenye taifa hili, leo hii wananchi hawana imani na Serikali kwa kuwa imeonesha wazi imeshindwa! Kushindwa kwa Serikali katika kutatua migogoro ya wasanii kwa kutotekeleza makubaliano mbalimbali yanayoafikiwa kati yake na wasanii, yameshusha hadhi yake kwa wasanii. Swali kubwa kwa Serikali sikivu ya CCM, Je mnasubiri migogoro mingapi ili mjue kuwa wasanii hawatendewi haki?
Je mnasubiri vikao vingapi vya upatanishi na usuluhihishi ili mjue kuna tatizo?
Ama mnataka wasanii wagombane, wapigane, wauane ili mjue kuwa kuna tatizo?

Mheshimiwa Spika,
Leo hii, Serikali bila ya kukaa na wadau wa muziki wa dansi, taarabu, bongo fleva, hip hop, mnanda na mahadhi mengine na kuwasikiliza kwa makini wamejikuta wanajihusisha na mambo ambayo hawajui. Watendaji wa Serikali wameendelea kuwaingiza mkenge viongozi wa Serikali katika masuala ya sanaa nchini. Hivi karibuni,hapa Dodoma, bila ya kuwa na taarifa muhimu juu ya unyonyaji wa haki za wasanii, waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, alishiriki katika tamasha la kudai haki za wasanii ambalo liliandaliwa na baadhi ya watu ambao kwa muda mrefu wamekua wakituhumiwa kuwa ni wanyonyaji wa kazi za wasanii. Kiongozi mkuu wa Serikali, unashiriki katika kupiga mihuri na kuhalalisha mikakati ya kimafia ya kuua umoja wa wasanii bila ya kuwa na taarifa sahihi. Je, waziri mkuu ana taarifa kuwa walioandaa tamasha la kudai haki za wasanii ndio walalamikiwa namba moja nchini dhidi ya haki za wasanii hasa wa muziki? Tuinataka Serikali na wanasiasa wote kuacha kutumia wasanii kwa faida zao binafsi bali wasaidie kutatua matatizo halisi ya wasanii ili waondokane na umasikini.

Source:Hotuba ya Kambi ya Upinzani iliyowasilishwa kabla ya kuondolewa Bungeni
 
Uwiiiiiii........kuna dokta wa macho humu......? Nakuja na A B C zangu........
 
7.1 Kulinda kazi za wasanii Mheshimiwa Spika, TBC leo inapiga na kucheza nyimbo za wasanii bila kuwalipa, huku wizara inayotakiwa kusimamia vyombo hivi inashuhudia sheria zilizopitishwa na bunge hili zinavunjwa. Mbaya zaidi TBC inauza CD na kanda za nyimbo zilizoko katika maktaba yake bila kutoa hata senti kwa wanamuziki waliorekodi nyimbo hizo, iko wapi tofauti yao na maharamia wengine? Leo hii wizara inawezaje kusema kuwa wao ni wasafi? Ni aibu kwa wizara, ni aibu kwa watendaji wake, ni aibu kwa serikali , sikivu, ya CCM! Mwaka 2003 zilipitishwa kanuni zilizoagiza wenye vyombo vya utangazaji nchini ziwalipe wanamuziki kutokana na matumizi ya nyimbo zao mbalimbali ambazo wanazitumia kwenye vipindi mbalimbali.

Ni jambo la kushangaza kuona kuwa Serikali ya CCM inayojitapa kuwa na utawala wa sheria inashindwa kudhibiti vyombo vya habari na utangazaji ambavyo vimeendelea kutumia kila aina ya ubabe na njia za kiunyonyaji ili visilipe fedha hizi kwa wasanii.
Leo hii wasanii wanalazimishwa kuandika barua kuwa wametoa nyimbo zao kwa vyombo hivyo zipigwe bila kulipia na kutokana na mazingira yaliyotengenezwa, wanamuziki wanajikuta ni lazima wahonge! ili nyimbo zao zipigwe ili waweze kupata soko la kazi zao.

Baada ya jitihada za hapa na pale, Serikali kwa kupitia TRA wameleta stika mpya, ambazo Tatizo moja tu hapa ni kuwa TRA kazi yao ni kukusanya kodi tu na sio kulinda hakimiliki, hivyo stika ya TRA ni stika ya kukusanya kodi na italeta mkanganyiko katika utekelezaji wa taratibu za hakimiliki.
Je, wizara imepanga mikakati gani kuhakikisha kuwa kazi za sanaa hazidurufiwi, kuuzwa na kusambazwa bila ya ridhaa za wasanii nchini? Kambi rasmi ya upinzani bungeni inarudia kuitaka Serikali kuifumua COSOTA na kuunda chombo kipya kitachokuwa na uwezo wa kusimamia kazi za sanaa.
Mwaka 2001, ilitengenezwa kamati iliyoitwa National Anti Piracy Committee ikiongozwa na Mwenyekiti John Kitime, iliyokuwa chini ya COSOTA, kazi yake kubwa ni kuwezesha kutengeneza sheria na kanuni za kuwezesha kazi za audio na video kuwa na stika za mapato. Kazi hii ilifanyika na kukamilika na kanuni hizo zilipita kwa usimamizi wa Waziri Mh. Juma Ngasongwa kabla tu ya uchaguzi wa mwaka 2005, lengo likiwa ni kupata sapoti ya wasanii.

Mheshimiwa Spika,
7.2 Nyimbo za wasanii na Mapato kwao.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Spika,
Wizara hii ambayo inasimamia TBC, televisheni na redio ya Taifa, imeshindwa kuvichukulia hatua za kisheria vyombo vyake ambavyo vimekua moja wapo ya wakiukaji wa sheria hii. Ni kejeli kwa taifa, ni kejeli kwa wasanii wanaopata shida kujikwamua kimaisha.
 
7.2 Harakati za kudai haki za wasanii.
Mheshimiwa Spika,
sanaa imeendelea kufanywa mtaji wa biashara na watu wachache ambao wanatumia nguvu waliyo nayo katika jamii na uwezo wao wa kifedha katika kukandamiza maslahi ya wasanii hapa nchini. Katika harakati za kutafuta haki za wasanii hapa nchini, mimi binafsi pamoja na wasanii wengine wachache, tulianzisha harakati za kudai haki kwa kupitia programu maarufu iliyojulikana kama 'Anti Virus' chini ya 'Vinega' ikiwa na lengo na juhudi za kudai haki za wasanii dhidi ya ukandamizaji unaofanywa na wajanja wachache kwenye muziki, ambao wametumia nafasi kama njia ya kutumia mitaji yao ya fedha kuwaendesha wasanii jinsi wanavyotaka wao.

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyo kawaida, wasanii wengi walidharau jitihada zetu na kutotuunga mkono. Leo hii katika tasnia ya muziki, kuna mgogoro mkubwa uliofuka moto kati ya msanii maarufu Lady Jaydee dhidi ya wamiliki wa radio ya Clouds FM hatua iliyosababisha nyimbo za wanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama 'Bongo Flavour' kutopigwa kwa siku moja katika kituo hicho. Sasa, ukiangalia kilio cha Lady Jaydee ni kilio kilekile kilichopelekea VINEGA kuingia vitani.

Mheshimiwa Spika, kama msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, na mwenye dhamana na uchungu na tasnia ya sanaa nchini, niweke wazi kwa umma wa watanzania kuwa, tumefikia hapa tulipo si kwa kuwa na sheria kandamizi tu bali pia kwa kukosekana kwa umoja wa wasanii nchini. Wakati tukiwa na juhudi za kutetea maslahi ya watanzania kupitia Anti Virus, ni wasanii wachache ambao walituunga mkono na wengi wao wakibeza jitihada zetu, wakiwemo hawa ambao leo wanalalamika kuwa wananyonywa haki zao. Wengine walifikia hatua ya kusema kuwa tumepewa fedha ili kuzima harakati tulizozianzisha.

Mheshimiwa Spika,
Umoja wa wasanii hasa wa muziki wa kizazi kipya nchini, unasimamiwa na chombo halali kinachojulikana TUMA-‘Tanzania Urban Music Association’, lakini kutokana na ujanja wa watu wachache, waliudhoofisha umoja huu kwa kuanzisha kampuni iliyosajiliwa kama TFU- ‘Tanzania Flavour Unit’ iliyowalaghai wasanii kuwa ni muungano wa wanamuziki wa Bongo Fleva na kuhodhi majukumu ya TUMA ambacho ni chama halali cha kusimamia wanamuziki wa Bongo Fleva. Mpaka tunapoongea leo hii, hata Studio iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi, bado ipo katika mikono ya TFU pamoja na Serikali kuamuru irudishwe katika mikono ya Serikali ili ikabidhiwe kwa wasanii wote chini ya chama halali cha TUMA. Sasa tunataka wasanii wote nchini waache uoga na unafiki na wajiunge na vyama vyao halali ili viwatete haki zao.

Mheshimiwa Spika,Kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa utetezi wa haki za wasanii kwa kuwa wanaotuhumiwa kunyonya haki za wasanii wameweza kutajirika na kuneemeka kwa kupitia jasho na mgongo wa wasanii. Hawa hawa wanaotuhumiwa kuhujumu wasanii ndio wanatumia nafasi yao kuupotosha ukweli wa tuhuma dhidi yao. Wanatumia fedha na rasilimali walizo nazo katika kunyanyasa wasanii, kuwakandamiza, kuwapokonya haki zao na kuwadhalilisha kuwa bila wao, wasanii wasingekua kitu.

Mheshimiwa Spika, Leo hii wasanii wanaishi kwenye hali ngumu, umasikini mkubwa lakini bado wanatolewa maneno ya kashfa na dharau na Serikali imeendelea kukaa kimya. Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kuacha siasa kwenye kutatua migogoro ya taifa hili. Siasa zimetumika sana katika kuzima jitihada za wanyonge kwenye taifa hili, leo hii wananchi hawana imani na Serikali kwa kuwa imeonesha wazi imeshindwa! Kushindwa kwa Serikali katika kutatua migogoro ya wasanii kwa kutotekeleza makubaliano mbalimbali yanayoafikiwa kati yake na wasanii, yameshusha hadhi yake kwa wasanii. Swali kubwa kwa Serikali sikivu ya CCM, Je mnasubiri migogoro mingapi ili mjue kuwa wasanii hawatendewi haki?
Je mnasubiri vikao vingapi vya upatanishi na usuluhihishi ili mjue kuna tatizo?
Ama mnataka wasanii wagombane, wapigane, wauane ili mjue kuwa kuna tatizo?

Mheshimiwa Spika,
Leo hii, Serikali bila ya kukaa na wadau wa muziki wa dansi, taarabu, bongo fleva, hip hop, mnanda na mahadhi mengine na kuwasikiliza kwa makini wamejikuta wanajihusisha na mambo ambayo hawajui. Watendaji wa Serikali wameendelea kuwaingiza mkenge viongozi wa Serikali katika masuala ya sanaa nchini. Hivi karibuni,hapa Dodoma, bila ya kuwa na taarifa muhimu juu ya unyonyaji wa haki za wasanii, waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, alishiriki katika tamasha la kudai haki za wasanii ambalo liliandaliwa na baadhi ya watu ambao kwa muda mrefu wamekua wakituhumiwa kuwa ni wanyonyaji wa kazi za wasanii. Kiongozi mkuu wa Serikali, unashiriki katika kupiga mihuri na kuhalalisha mikakati ya kimafia ya kuua umoja wa wasanii bila ya kuwa na taarifa sahihi. Je, waziri mkuu ana taarifa kuwa walioandaa tamasha la kudai haki za wasanii ndio walalamikiwa namba moja nchini dhidi ya haki za wasanii hasa wa muziki? Tuinataka Serikali na wanasiasa wote kuacha kutumia wasanii kwa faida zao binafsi bali wasaidie kutatua matatizo halisi ya wasanii ili waondokane na umasikini.

Source:Hotuba ya Kambi ya Upinzani iliyowasilishwa kabla ya kuondolewa Bungeni

Uwiiiiiii........kuna dokta wa macho humu......? Nakuja na A B C zangu........
Haya dear nimekuletea miwani.
 
Sugu huwa simwelewi bungeni anawakilisha jimbo lake au anawakilisha bongo fleva.
 
Wewe Kilaza sikiliza, hivi unajuwa Sugu ni waziri kivuri wa Wizara gani?

Unataka aongelee barabara kwenye mambo ya sanaa na utamaduni? hivi kwa nini watu wengine hamjaelimika pamoja na kupata fursa ya kutumia mitandao?
 
Sugu huwa simwelewi bungeni anawakilisha jimbo lake au anawakilisha bongo fleva.

labda nikuukize ni bajeti gani inayojadiliwa,
au ulitaka atamuke barabara wakati haihusiani na kunachojadiliwa.!
 
Unajiita babu kijana?? Halafu huna akili za ujana wala busara za ubabu senz sana
 
Huyu mbunge wa mbeya jaman hamna kitu kichwani kweli nimeamini kama usipoenda shule na ukawa unatumia majani utakuuwa na matatizo kidogo sasa katika kuwakilisha maoni ya kambi ya upinzani leo lengo lilikuwa si kushauri bali kutafuta sifa.
Anaongelea vinega jamani hao vinega hata leo mseme show bure watu hawataingia hawana mvuto
Huyo jaydee na prof jay ndio wameloweka jay dee akumbuke dhambi aliyoifanya 2002 ndio inamtafuna mpaka sasa nyimbo zenyewe sasa kama kelele za kundi la nyuki wakiwa wanapita
 
duuuh,sasa hapa sijajua nani amesoma na nani hajasoma,anayejiona amesoma haeleweki,arguements haziendani na kichwa cha thread,sasa hapa sijui nani anatafuta sifa.Ushauri wangu ningeomba urudie ukasome tena ile hotuba hasa hicho kipengele halagu urudi tena.
 
mtoa mada inaonekana unatumiwa na maharamia wa sanaa nchini kwanza ulichoandika hakina kichwa wala miguu ulichoshika kwene hotuba ya sugu ni vinega tu basi kasome tena hotuba yake vizuri naamini utamwelewa
 
duuuh,sasa hapa sijajua
nani amesoma na nani hajasoma,anayejiona amesoma haeleweki,arguements
haziendani na kichwa cha thread,sasa hapa sijui nani anatafuta
sifa.Ushauri wangu ningeomba urudie ukasome tena ile hotuba hasa hicho
kipengele halagu urudi tena.

mkuu,upeo wake ndo umeishia hapo halafu anajiona kuwa yeye ndo amesoma,hajui kuwa hata wasiosoma wakati mwingine wana hoja,hasemi kama tuhuma za sugu zina mantiki au la,yeye anamuona kama mvuta bangi tu
 
Huyu mbunge wa mbeya jaman hamna kitu kichwani kweli nimeamini kama usipoenda shule na ukawa unatumia majani utakuuwa na matatizo kidogo sasa katika kuwakilisha maoni ya kambi ya upinzani leo lengo lilikuwa si kushauri bali kutafuta sifa.
Anaongelea vinega jamani hao vinega hata leo mseme show bure watu hawataingia hawana mvuto
Huyo jaydee na prof jay ndio wameloweka jay dee akumbuke dhambi aliyoifanya 2002 ndio inamtafuna mpaka sasa nyimbo zenyewe sasa kama kelele za kundi la nyuki wakiwa wanapita

mmmh wewe uwezidi ukilaza
 
Kwa ulicho andika hapa hata Lusinde amekuzidi.
 
Back
Top Bottom