SI KWELI Sugu awaomba CHADEMA kuiunga mkono CHAUMMA kutafuta kura za urais

SI KWELI Sugu awaomba CHADEMA kuiunga mkono CHAUMMA kutafuta kura za urais

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu

Ni kweli Sugu amesema CHADEMA iwaunge mkono CHAUMMA kutafuta kura za urais au ni uzushi? mwenye ukweli wa wa hizi taarifa naomba msaada.
Sugu screenshot Sept 20.jpg
Sugu Nipashe Sept 20,.jpg
Sugu mwanahalisi Sept 20.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Ipo taarifa inayodai kuwa Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu) kupitia ukurasa wake wa X amechapisha ujuumbe wa kuwataka Wanachadema kuwaunga mkono chama cha ukombozi wa umma (CHAUMMA) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Ujumbe huo unaeleza pia kuwa yeye Sugu ataanza na kumuunga mkono mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Salum Mwalimu. Ujumbe huo umewekwa kweny grafiki yenye utambulisho wa chombo cha Mwanahalisi na Nipashe Digital.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa tarifa hiyo si ya kweli.

kupitia utafutaji wa maneno muhimu, JamiiCheck imebaini kuwa ujumbe huo haujachapishwa na Sugu kupitia ukurasa wake wa X na hivyo umetengenezwa na kuwekewa utambulisho wa kiongozi huyo.

Hadi wakati ripoti hii inaandikwa Septemba 20, 2025, taarifa ya mwisho kuchapishwa katika ukurasa wa Sugu ilikuwa ni kuelezea masikitiko yake juu ya kifo cha kada mwenzao wa CHADEMA, Frank John Nyalusi.

Aidha grafiki zilizotumika kusambazia taarifa hiyo ni za kughushi na hazijachapishwa na vyanzo hivyo (Mwanahalisi na Nipashe). Licha ya kutochapishwa na vyanzo hivyo lakini pia zina mapungufu kadhaa ikiwemo aina ya mwandiko uliotumika na mpangilio ukilinganisha na grafiki halizi za vyanzo hivyo.
Back
Top Bottom