Sugu awatukana waandaaji wa fiesta kwenye facebook


Kapata faida gani kwa kumwaga matusi facebook? Imewauia hao wezi? Je hao walengwa hata wameona ujumbe? Tuache unafiki kwa kutetea alichofanya hakumsaidii bali kunambomoa. Kulikua hakuna haja ya matusi unaweza tumia maneno ya ukali bila kutukana. SIjui ni nini haswa mnacho tetea hapa???
 
kinachonikera ni kuwa hao waseng,e anaowasema sugu,hawalipi kodi kwa matamasha wanayofanya.
 
kinachonikera ni kuwa hao waseng,e anaowasema sugu,hawalipi kodi kwa matamasha wanayofanya.
Una uhakika gani hawalipi kidi? Mpaka waje kukutangazia kuwa wamelipa kodi kiasi flani? TRA siyo wazembe kama unavyofikiri
 
Awali nilishasema kuwa chadema ni chama cha wahuni, na mods wakafuta bandiko langu... Sasa angalieni mhuni mbunge huyo!
Wahuni wa namna hii ndiyo tunaowataka nchi hii! siyo uhuni wa ngono kama wa ........... Utamalizia mwenyewe ukipenda.
 
CHADEMA is led by a mobster Mboye, no wonder the surbodinates copy their prexy's ways. Mboye has yet to enoxerate himself from allegations that he is an infamous marijuana smoker. Imagine in the future having these type of hooligans acting as our ministers, this should never happen during my life time. I am not stupified when I see these 'leaders' coax desperate youths into deluging streets, doing vandalism under the umbrella of peaceful demonstrations.
 
Lugha aliyotumia imefikisha ujumbe uliotakiwa ndiyo maana wewe uko hapa unatoa mapovu vinginevo ungekuwa na time zako.
Nimekwambia waambie clouds next time wawe wastaarabu sio wasanii wote wajinga wasijione wao miungu watu wa kutumia sauti za watu hovyo.
 
Kweli mkude gangwe! Tuache unafiki, kila forums huwa na lugha zake, tujikite kwenye contextual meaning na siyo neno moja moja, mna distruct meaning, na kutupoteza malengo! Kama swala ni matusi mbona huwa yanatamkwa na mengine kuandikwa kwenye vyombo vya habari tunayasikia!
 
If Chadema is led by mobsters CCM is led by monsters
 
I know Sugu Means Well, I know Sugu in the Streets and in Rap Themes That's kinda Language they Use..., LAKINI inabidi atumie Busara because some comments zinaweza zikawa-alienate baadhi ya watu kama watu wazima na watu wanaoangalia hizi issue kama uhuni; and as a Politician he needs all the votes he can get...

Kwahiyo Mheshimiwa Sugu, Mr II, AKA Joseph Mbilinyi, Kumbuka this is a WAR and NOT A BATTLE, lazima utumie strategies za long term, kushindwa Battle sio kushindwa Vita, tumia Busara, na kufanya mashambulizi yatakayoweza kumuua adui na sio kumjerui na kumwacha ili aje akumalize.
 
Sijapata kuona wabunge wahuni kama Sugu na Lema! hata kama upatani na mtu uwezi kuandika matusi hivyo kama vile mvuta bangi, Sugu angekuwa sio mbunge wala hakuna angaelalamika, mbunge kutoa matusi ni ujinga wa hali ya juu
Wewe kwa kuwa hayakuhusu ndo maana unaona ujinga. Kumbuka ni mara ngapi huwa unatukana unapo udhiwa?Si umeona baada ya kutukana kila mtu amelichukulia swala hili kwa uzito; angeandika lugha ya bungeni nani angechukulia serious?Sugu alitaka kufikisha ujumbe kwa jamii na kweli mmesikia na huu ndo mwanzo wa mapambano yake na hao aliowatukana.
 
well jino kwa jino, wala chadema haihusiki hapo. hapo ni sugu kama msanii ndio maana na wewe umesema sugu na sio joseph mbilinyi
 
Nilisema taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari ilikuwa na makosa ya kiuandishi kwa mtu mwenye wadhifa wa mbunge, lakini hii status yake kwenye facebook imetia fora.

Hapa Sugu kama role model wa vijana anawafunza nini?
 
unataka kujua umuhimu wa lugha aliyotumia??..amefanikiwa kupata attention kubwa ya watu wa rika mbalimbali ivyo mjadala aliouanzisha ambao ndio shabaha yake kubwa utakuwa na wigo mpana zaid na utachukua watu wengi zaidi kuujadili
 
Mkuu, wewe hayo matusi yanakuhusu? Kwani huyo Sugu kashindwa kufikisha ujumbe wake mpaka afikisha kwa njia ya matusi?
 
unataka kujua umuhimu wa lugha aliyotumia??..amefanikiwa kupata attention kubwa ya watu wa rika mbalimbali ivyo mjadala aliouanzisha ambao ndio shabaha yake kubwa utakuwa na wigo mpana zaid na utachukua watu wengi zaidi kuujadili

Alichofanya ni kutuondoa kwenye hoja yake na sasa tunajadili lugha kama ni sahihi au la.

Mtu asiyeona aibu kutukana namna hii kwenye public ni Tanzania pekee anaitwa kwa cheo cha Mheshimiwa.
 
Hahahah..kama mambo yenyewe ndio haya mmmh! Halafu utakuta mtu anajiita Great Thinker halafu ana Kadi ya chama cha kihuni kama cha huyu mheshimiwa!!!

Though I dont condone foual language,But CHADEMA SIO CHAMA CHA KIHUNI.

Hakuna chama cha kihuni kama CCM.Hivi mkuu unataka maneno ambayo yanasemekana yameandikwa Facebook yawe sababu ya watanzania kuona CHADEMA haifai na badala yake waikumbatie CCM na uhuni wake wa EPA,MEREMETA.RICHMOND,na takataka zote?
 
Nilisema taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari ilikuwa na makosa ya kiuandishi kwa mtu mwenye wadhifa wa mbunge, lakini hii status yake kwenye facebook imetia fora. Hapa Sugu kama role model wa vijana anawafunza nini?
anatufunza kuwa wazi kutoa hisia zetu yani tusiigize maisha tuache unafiki..
 
Mkuu, wewe hayo matusi yanakuhusu? Kwani huyo Sugu kashindwa kufikisha ujumbe wake mpaka afikisha kwa njia ya matusi?
Mara ngapi wewe watu wanakuambia uache kutumia matusi huwa unashindwa kufikisha ujumbe kwa njia nyingine.
 
anatufunza kuwa wazi kutoa hisia zetu yani tusiigize maisha tuache unafiki..


Kwa hiyo ukiwa na hamu ya kumtukana mwalimu shuleni umtukane tu, ukiona system ya baraza la mitihani inakunyanyapaa mwanafunzi, wakati wa kujibu masuala yale jaza matusi au vipi? Si tunaweka hisia wazi ya nini kuficha?
 
Mara ngapi wewe watu wanakuambia uache kutumia matusi huwa unashindwa kufikisha ujumbe kwa njia nyingine.
Mimi ni mtu mzima najiheshimu ata siku moja siwezi kutumia matusi kufikisha ujumbe, lazima mmkubali Sugu kafanya kitu cha kihuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…