Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alitemwa mwaka 2020, alikuwa ana shida zake na CCM. Mwaka 2019 Ndugai aliandika barua PAP kusitisha uwakilishi wake, wakamrudisha nyumbani na kumpeleka kamati ya maadili kwa utovu wa nidhamu..Umesahau kwamba Yule Mbunge wa Shinyanga Steven Masele alikua Rais wa Bunge la Africa na alitemwa ubunge Mwaka 2015?
Watu mnasahau mapema sana
Yeah nimekumbuka 2020, Ndugai ni majukumu yake kuandika Barua PAP maana hiko cheo kinakoma pale ukiacha kuwa mbunge Maana utakuwa hubanwi na sheria zozote za Uwajibikaji.Alitemwa mwaka 2020, alikuwa ana shida zake na CCM. Mwaka 2019 Ndugai aliandika barua PAP kusitisha uwakilishi wake, wakamrudisha nyumbani na kumpeleka kamati ya maadili kwa utovu wa nidhamu..
Kwamba mtamsaidia kuiba kura kama mlivyofanya 2020, au?!Jambo la pili spika hawezi kushindwa ubunge hasa spika wa bunge la Tanzania haijawai na haitaruhusiwa kutokea.Sina Mengi ni hayo TU.
Hakuna Spika wa Tanzania anaweza kushindwa ubunge kuanzia CCM ndani mpaka nje kipi ambacho hakieleweki, Biteko atashinda TU ubunge kama atagombea, Tulia atashinda TU kama atagombea, Samia atashinda kama atagombea.Kwamba mtamsaidia kuiba kura kama mlivyofanya 2020, au?!
😀😀😀Kuna tetesi mmoja atagombea popote atakapogombea mwenzake katika hayo majimbo mawili endapo yakigawanywa..
Sio mlungula kweli maana hawaaminiki'The IPU Governing Council elects the IPU President for a term of three years. He or she must be a sitting Member of Parliament throughout the term of the presidency'
Leo Tulia Ackson amechaguliwa kuongoza umoja wa mabunge duniani kwa kipindi cha miaka mitatu. Moja ya sifa ya kuendelea kuwa rais wa umoja huo ni kubaki kuwa mbunge kwa kipindi chote cha muhula wake wa miaka mitatu.
Tanzania inatarajiwa kuingia kwenye uchaguzi mkuu miaka miwili ijayo, Tulia atakuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye muhula wake wa Urais IPU. Ukiachana na uchaguzi wa 2020, Sugu amekuwa na rekodi nzuri ya matokeo Mbeya mjini huku mwaka 2015 akizoa kura nyingi mpaka kuwa mbunge wa kwanza aliyechaguliwa kwa namba kubwa ya kura Tanzania nzima.
Mwaka huu wa 2023 wawili hao wamekuwa wakirushiana vijembe kila mmoja akitamba kumgaraza mwenzake uchaguzi wa 2025 huku Dkt. Tulia akianza na Sugu kujibu mapigo.
Uchaguzi wa ubunge jimbo la Mbeya Mjini umetiwa ndimu na chumvi! Tusubiri 2025..
Pia, soma=> Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303
CCM wataongeza nguvu kutetea kiti cha ubunge Mbeya mjini, rekodi huko nyuma zinaonesha CCM huwa wanashinda sehemu ambazo hamna mtu alitarajia watashinda..Kuwa rais IPU, haikufanyi uwe na tiketi ya uhakika ya kubaki bungeni kwa kura za wananchi, matakwa ya IPU Sio matakwa ya watu wa Mbeya. Watu wa Mbeya wanataka kiongozi atakaye timiza haja za Wana Mbeya, na sio habari za IPU. IPU haitatui shida za wanambeya.
Kwa pesa zipi za kugharamia??Jimbo linagawanywa Mkuu. Tulia anapewa la kwake na Sugu naye anapewa la kwake. Hivi ndivyo tunavyoishi Watanzania na mihimili yetu.
Ova
Siyo alikuwa anamkimbia sugu?Tulia ni chaguo sahihi la wana Mbeya na alipopendekeza Jimbo la Mbeya ligawanywe alilenga kumsaidia Sugu.
UmenenaMkuu, tuacheni kujidanganya. CCM bila vyombo vya ulinzi na usalama kwwnye box la kura hawatoki, na wao wanajua kabisa hili.
Mbeya Tulia hatoboi bila polisi na NEC.
Wewe wasemaSugu hawezi kushinda Mbeya atakama Dr. Tulia asingekuwa Rais wa IPU