Sugu na Jide ni wasanii wasioguswa, ukiwagusa umepotea kimoja, pitia hapa ushuhudie


Uko vizuri mkuuu
Napenda watu wanaoongea with facts/evidences
 
Sasa baada ya kumtongoza nini kilifata?
Niambie Jide alimfanya nini Chid ambacho tunaweza sema kweli ndiye aliyempoteza Chid!

Yaah walikuwa maarufu kabla lakini tujiulize
Umaarufu wa Jide na Chid umeshamiri kipindi gani na watu wame wafatilia sana kipindi gani?
 
Sugu na Jide ni moto wa kuotea mbali hawawalambi watu miguu,ukileta za kuleta kwakua una karedio kako watu wanakupotezea vilevile,watu walianza kuhit kabla ya FM kipindi hicho David Wakati ni Mkurugenzi wa RTD(rip)! Kina FA,Roma,Benzi wote ni walamba miguu wanataka Show za lakilaki za Fiesta!
 

Kuna track waliimba pamoja kati ya Jide na Chid unaitwa upo Juu,inaonekana baada ya ku-hit huo wimbo chid benz akaanza kuleta mapozi kwenye kushoot video mara ana-demand anunuliwe nguo mara apangiwe hotel mara alipwe kiasi kadhaa yani full complication kina Gadner na jide wakaona isiwe shida wakakata audio yake kwenye ile video wakaweka wacheza show basi video ikaruka hewani baada ya kupotezewa ndio akaanza bla bla nyingii na beef likawa juu.
 
Uko vizuri mkuuu
Napenda watu wanaoongea with facts/evidences

Wakati huo Sugu amepanga chumba mbagala na ni mlinzi wa getini BP ajira ambayo alikuwa akipata kipato kizuri sana kutokana na mishemishe za wese,

Kabla ya kupata lidandasi aligunduwa hawezi kufika popote bila kujichanganya na watoto wa kishuwa upanga ndio akajichanganya Don Bosco na kupiga story na kwanza Unity na baadaye Sugu alijumuishwa kwenye kundi la Diplomatz na king Saigon na Balozi lakini yeye akiendelea na Solo project zake kabla xa kwenda kupiga box UK.

Na hapo ndipo ilipotokea hujuma kabla Clouds fm haijaanzishwa na Radio one walikifuta rasmi kipindi cha Rap cha kila ijumaa ambacho kilikuwa chini ya Mike Mhagama hii ilikuwa ni kabla ya mwaka 95 na ndio 2 proud katika mistari aliwachana redio one kwamba yeye alianza kurap kabla ya Fm na watu walimfahamu.

Jide nilianza kumsikia yeye na Ray C wakiwa watangazaji wa clouds na baadaye wakatoa single zao, hakuna mwanabongo fleva nchi wa kumfananisha na Sugu, huyu ni Die harder.

Kama unafuatilia Bongo hiphop kuna vichwa vya ukweli lakini vimeshindwa kukomaa na wamenyoosha mikono juu lakini ni Sugu peke yake aliweza kukomaa.

Angalia hard blasters, Kwanza Unity, LWP, Wateule, Source B, Unique Sisters, Skwiza na dada yake huu ni mfano wa vipaji vilivyopotezwa na mfumo wa muziki wa Bongo.
 
Ila Jide ana miaka mingapi maana kuna siku nikicheki diary yake...uso umekomaa sana yani pamoja na ma make up lakini wapi..
Sema wanaficha umri wao ila sura zinawaumbua sana.
Emenem kazaliwa 1972 ila nahisi Jide ni mkubwa kushinda Eminem

Kwani nani kakwambia msanii hatakiwi kuwa mtu mzima? Unaonekana wee ni mtoto! Kuwa kwanza akili yako ijuwe mambo.
 
Jide ni next level ki ukweli, wala sio kwamba tunampa sifa za kijinga, yule bibi ni shidaa, kashindikana afrika mashariki nzima, hyo benpol nae anatafuta kick jide atamuwezea wapi kapuku wa buguruni

Upo sawa,Jide anamafanikio makubwa.
 
Mleta mada huna hoja wala fact zaidi ya kujifariji ma wasanii wako kuwa ni untouchable

Ungekuwa waZi tu kwamba kwakuwa walithubutu kupinga unyonyaji wa clouds Fm ndio maana unawaona mashujaa ningekuelewa
 

Aisee ayo maswali yako kama tupo mahakamani sasa... Hapa nafikiri wameongrlea. ishu za kijamii zaidi sio kisheria mpaka mtu alete ushahidi..

Maana Jide ni maarufu nadhani tangia Chidi yupo primary school sasa ayo ya baada ya kutongoza ikawaje mie nitakuwa nasema uhongo ila walishafanya wimbo pamoja unaitwa Mpo juu na video Chidi hakuwekwa.

Ni kama watu wa siasa wanavyosema ukitaka kupiga siasa zako bila kuharibu basi usimdiss Nyerere na kweli tunaona watu waliomgusa Nyerere walishindwa siasa. Sasa aya ni mambo ya. kijamii zaidi ayaitaji facts kama we unavyotaka. Na nadhani ndio wanachosema washikaji hapa.
 
Hebu jaribu maandishi haya basi utupunguzie maumivu ya ndimi! maharufu=maarufu
ata=hata,uyo=huyo ,alafu =halafu.
 
Yaah umaarufu wao umechagizwa zaidi na mafarakano.....hili haliitaji ushahidi!

Hili si kweli hata kidogo unless wewe umemjuwa Sugu wakati anaimba mambo ya feza na Jide, lakini kipindi anatembea na Cd yake mkononi yenye beat na anaomba kupewa nafasi ya kuperfom bila hata kupewa mia hukumjuwa.

Na kama ulikuwa hujui maisha ya mshkaji amesurubika mno na watu wa aina yake Mungu huwafuta machozi na kwa nini alifanikiwa kutoa albam alikuwa anatumia pesa anayopata kazini kwake BP kulipia studio Don bosco akipeleka master kwa wadosi anaambulia laki mbili tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…