Sugu na Jide ni wasanii wasioguswa, ukiwagusa umepotea kimoja, pitia hapa ushuhudie

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
1. Lady Jaydee

Uyu dada ndio msanii mwenye washabiki kuliko wasanii wote Bongo, ni mwanamuziki anayeheshimika na wasanii wenzake karibu wote na wadau mbalimbali wa muziki na sekta zingine.

Aliyejaribu kumgusa Msanii yoyote anayejaribu kumgusa uyu dada unapotea yeye, wasanii waliioonja joto ya Jide ni awa wafuatao na wakapotea

Chidi benzi;
uyu baada ya kuvuma sana akawa anamchokoza uyu dada kwa kufanya mambo ya kumkosea heshima Komando leo amebakia hadithi, ameishia kuwa mteja.

Mwana FA;
uyu alikuwa rafiki mkubwa wa Jide na alimshirikisha Jide kwenye album zake zote, ata maisha ya kawaida walikuwa wakishirikiana kwenye vingi.
Mwishoni alikuja kumsaliti Jide kwa kutumika na Joseph Kusaga na Clouds kujaribu kudhoofisha mahudhrio ya show ya Jide ya kutimiza miaka 10, hii ilizua ugomvi mkubwa kati yao na baada ya hapo FA akapoteza mashabiki wake wengi sana waliomchukulia kama msanii mwenye upeo mkubwa.
Ana wimbo mpya mkali sana ‘mfalme' ila umepotea kwa kuwa FA ameshatoka mioyoni mwa watu.

Mrisho Mpoto

Msanii uyu wa ushahiri alijiharibia baada ya kumtaka Jide amkabidhi kijiti Lina au Recho wakati wake umepita, na aliyazungumza haya kwenye jukwaa la fursa.
Baada ya hapo waliomchukulia kama mwanaharakati ambao ndio walikuwa washabiki wake wakubwa wakambeza na kumpotezea moja kwa moja.
Mpoto amebaki kupata matangazo ya serikali ila muziki umeisha na ataki kukabidhi kijiti kwa Mpoki wanaefanya style moja kama alivyomtaka Anaconda.

Ben Pol
Uyu alimwita Jide mgonjwa wa akili kupitia social networks, baada ya Jide kumtuhumu kuvunja mkataba wa kutumbuiza show yake ya kutimiza miaka 10. Kwa sasa Ben ni hadithi iliyopita.

Wapo wengi wengine ni ishu za chini ya kapeti

MR II Sugu aka Nyerere wa Rap

Uyu ndio baba wa Bongofleva na hiphop kwa ujumla. Ni msanii anayeheshimika kwa misimamo yake ‘tata' na uwezo wa kupambania mambo mbalimbali. Historia na mchango wake kwenye muziki wa Tanzania hakuna anayeweza kumnyang'anya japo kuna waliojaribu ila wakashindwa.
Kwa sasa ameeegemea zaidi kwenye siasa, akiwa kama mwakilishi wa watu wa Mbeya mjini.

Waliomgusa

Mwana FA

Uyu FA alikuwa rafiki mkubwa wa Sugu, aligeuka adui baada ya FA kujigeuza ngao kwenye ugomvi wa Sugu na Clouds media akisimama kati kumzuia Sugu asifikishe makombora yake kwa upande wa pili (refer AntiVirus Saga). Tangia hapo FA alijipoteza ushawishi na zaidi baada ya kuharibu na kwa Jide, akajibrand upya kama kibaraka.

Roma Mkatoriki

Uyu alimdiss Sugu kwenye wimbo wake wa KKK na ukawa ndio mwisho wa Roma. Kwa sasa anatoa ngoma zinabaki kuwa habari tu kuwa Roma ametoa mpya ila zinabuma.

Bwana Misosi

Alimdiss Sugu kwenye kwenye ‘nitoke vipi' na akafanikiwa kuvuma kwa muda . Ingawa alikuja kusahihishakauli lakini alipotea yeye akamwacha Sugu aliyemkashifu .

Joh Makini

Kwenye wimbo wake ' manuva' alimdiss Sugu akisema anafanya harakati magirini. Kwa sasa Joh anasafiria nyota ya weusi maana nyimbo anazotoa baada ya hapo zinabuma.

Kuna wengine wengi tu kina Afande sele, Mox, Jafarai na wengineo wote waliomjaribu Sugu wamepotea.

Kifupi hakuna aliyewahi kuwagusa awa manguli akabaki salama.

Swali ni je, Kwa nini imekuwa hivi?
 
Kumdis Sugu ni kujitafutia laana ya bure, Sugu ni mtu mwenye misimamo ambaye aliweza kusimama mwenyewe kama soul artist kitu ambacho ilikuwa haiwezekani.

Kwenye Mabonanza ya Kim & boys alikuwa anafanya show bila kulipwa hata shilling, nakumbuka kwenye mashindano ya Taifa ya Rap yalifanyika Avalon mwaka 93 lakini yeye hakushiriki kwa sababu hakuna vigezo yalitakiwa makundi ila walimpa nafasi ya kutoa show na single yake ya siku yangu.

Washindi wa kwanza walichukuwa Hard blasters wa pili wakawa Gangstes with Matatizo GWM na watatu wakawa Live with purpose LWP.
 
Jide binafsi namkubali sana
Sababu anajua anachokifanya
 
Kwa hiyo jide ndio alosababisha chidi benzi kuwa teja????

Mrisho mpoto nae ni msanii au mganga njaa tu????

Kwa lugha nyungine FA ni kambi ya clouds..... hivyo kwa namna moja au nyingine amejikuta kubeba chuki za clouds toka kwa wananchi???

Kwwli bongo kuna wasanii wengi...roma ben pol loh...

Nitamalizia kuisoma baadae... nitarudi
 
Sugu ana CV kubwa sana.
 
Jide ni next level ki ukweli, wala sio kwamba tunampa sifa za kijinga, yule bibi ni shidaa, kashindikana afrika mashariki nzima, hyo benpol nae anatafuta kick jide atamuwezea wapi kapuku wa buguruni

Teh teh nani tena uyo kapuku wa buguruni? Jide ni mkubwa sana...Angalia wanawake alioanza nao na waliomkuta wako wapi.
 
Kwa hiyo jide ndio alosababisha chidi benzi kuwa teja????

Mrisho mpoto nae ni msanii au mganga njaa tu????

Kwa lugha nyungine FA ni kambi ya clouds..... hivyo kwa namna moja au nyingine amejikuta kubeba chuki za clouds toka kwa wananchi???

Kwwli bongo kuna wasanii wengi...roma ben pol loh...

Nitamalizia kuisoma baadae... nitarudi

Haina aja ata ya kumalizia maana ata hapo ulipoishia kusoma panatosha...Au unaonaje?
 
Kwa wanaofatilia music hawa wat walifaham walichifany na pia wanastahil pongez,ila FA n moja kat ya wana music wazr kw level za kina jide ila kua vibarak kimemwalibia hasa kw ss mashabk..all n all anaepigwa vita ya fitna hulindwa na umati
 
Ila Jide ana miaka mingapi maana kuna siku nikicheki diary yake...uso umekomaa sana yani pamoja na ma make up lakini wapi..
Sema wanaficha umri wao ila sura zinawaumbua sana.
Emenem kazaliwa 1972 ila nahisi Jide ni mkubwa kushinda Eminem
 
Kweli kabisa kugusa hawa raia ni sawa na kudeki bahari. Kuna watu wanamponda sugu kuhusu kusaliti vinega lakini kiukweli ile ishu haikuwa usaliti bali ilikua msukumo wa viongozi wa cdm kumwomba sugu akae meza ya maridhiano na clouds. Coz ruge aliwafata kina mbowe akawaomba wambembeleze sugu, ila sugu alikataa ila badae ilibidi akubali kwa kubembelezwa sana na makamanda. Na ndo maana katika friday night Live ya EATV sugu alimdisi sana ROMA kwa kusema jamaa alikua anatafuta vina tu ktk wimbo
 
Hebu twambie Chid alimfanya nini Jide? Mbona Mwana FA yupo na anapendwa na show anapiga kila Leo?
Huyo Sugu kampoteza nani? Mbona walio kwaruzana nao bado wapo na wanafanya biashara zina kwenda vyema tuu?

Hivi Jide ndio sababu ya Chid kula madawa?
Sijaona Ushahidi wowote usio tia shaka kubeba habari yako!
Ni nani aliyewagusa akapotea? Kuguswa maana yake nini?

Hii habari yako haina ukweli wowote Jide na Sugu ni wapenda ugomvi na mifarakano na hawakuwai kumpoteza yeyote zaidi ya kupata umaarufu kupitia mafarakano!
 
Kama jide kuwa na uso ulokomaa ni shida .....ina maana wewe hautokua???
Some people bhana, growing old is mandatory hata wewe muda ukifika shavu litakushuka tu na sura itakakamaa kwa sana.
Ila Jide ana miaka mingapi maana kuna siku nikicheki diary yake...uso umekomaa sana yani pamoja na ma make up lakini wapi..
Sema wanaficha umri wao ila sura zinawaumbua sana.
Emenem kazaliwa 1972 ila nahisi Jide ni mkubwa kushinda Eminem
 
1.Lady Jaydee

Uyu dada ndio msanii mwenye washabiki kuliko wasanii wote Bongo, ni mwanamuziki anayeheshimika na wasanii wenzake karibu wote na wadau mbalimbali wa muziki na sekta zingine.

Aliyejaribu kumgusa Msanii yoyote anayejaribu kumgusa uyu dada unapotea yeye, wasanii waliioonja joto ya Jide ni awa wafuatao na wakapotea

Chidi benzi;
uyu baada ya kuvuma sana akawa anamchokoza uyu dada kwa kufanya mambo ya kumkosea heshima Komando leo amebakia hadithi, ameishia kuwa mteja.

Mwana FA;
uyu alikuwa rafiki mkubwa wa Jide na alimshirikisha Jide kwenye album zake zote, ata maisha ya kawaida walikuwa wakishirikiana kwenye vingi.
Mwishoni alikuja kumsaliti Jide kwa kutumika na Joseph Kusaga na Clouds kujaribu kudhoofisha mahudhrio ya show ya Jide ya kutimiza miaka 10, hii ilizua ugomvi mkubwa kati yao na baada ya hapo FA akapoteza mashabiki wake wengi sana waliomchukulia kama msanii mwenye upeo mkubwa.
Ana wimbo mpya mkali sana ‘mfalme’ ila umepotea kwa kuwa FA ameshatoka mioyoni mwa watu.

Mrisho Mpoto

Msanii uyu wa ushahiri alijiharibia baada ya kumtaka Jide amkabidhi kijiti Lina au Recho wakati wake umepita, na aliyazungumza haya kwenye jukwaa la fursa.
Baada ya hapo waliomchukulia kama mwanaharakati ambao ndio walikuwa washabiki wake wakubwa wakambeza na kumpotezea moja kwa moja.
Mpoto amebaki kupata matangazo ya serikali ila muziki umeisha na ataki kukabidhi kijiti kwa Mpoki wanaefanya style moja kama alivyomtaka Anaconda.

Ben Pol
Uyu alimwita Jide mgonjwa wa akili kupitia social networks, baada ya Jide kumtuhumu kuvunja mkataba wa kutumbuiza show yake ya kutimiza miaka 10. Kwa sasa Ben ni hadithi iliyopita.

Wapo wengi wengine ni ishu za chini ya kapeti…………………………

MR II Sugu aka Nyerere wa Rap

Uyu ndio baba wa Bongofleva na hiphop kwa ujumla. Ni msanii anayeheshimika kwa misimamo yake ‘tata’ na uwezo wa kupambania mambo mbalimbali. Historia na mchango wake kwenye muziki wa Tanzania hakuna anayeweza kumnyang’anya japo kuna waliojaribu ila wakashindwa.
Kwa sasa ameeegemea zaidi kwenye siasa, akiwa kama mwakilishi wa watu wa Mbeya mjini.

Waliomgusa

Mwana FA

Uyu FA alikuwa rafiki mkubwa wa Sugu, aligeuka adui baada ya FA kujigeuza ngao kwenye ugomvi wa Sugu na Clouds media akisimama kati kumzuia Sugu asifikishe makombora yake kwa upande wa pili (refer AntiVirus Saga). Tangia hapo FA alijipoteza ushawishi na zaidi baada ya kuharibu na kwa Jide, akajibrand upya kama kibaraka.

Roma Mkatoriki

Uyu alimdiss Sugu kwenye wimbo wake wa KKK na ukawa ndio mwisho wa Roma. Kwa sasa anatoa ngoma zinabaki kuwa habari tu kuwa Roma ametoa mpya ila zinabuma.

Bwana Misosi

Alimdiss Sugu kwenye kwenye ‘nitoke vipi’ na akafanikiwa kuvuma kwa muda . Ingawa alikuja kusahihishakauli lakini alipotea yeye akamwacha Sugu aliyemkashifu .

Joh Makini

Kwenye wimbo wake ‘ manuva’ alimdiss Sugu akisema anafanya harakati magirini. Kwa sasa Joh anasafiria nyota ya weusi maana nyimbo anazotoa baada ya hapo zinabuma.

Kuna wengine wengi tu kina Afande sele, Mox, Jafarai na wengineo wote waliomjaribu Sugu wamepotea.

Kifupi hakuna aliyewahi kuwagusa awa maNguli akabaki salama.....Swali ni je, Kwa nini imekuwa hivi?

...uyu = huyu. ( hata hivyo uzi mzuri)
 
Hebu twambie Chid alimfanya nini Jide? Mbona Mwana FA yupo na anapendwa na show anapiga kila Leo?
Huyo Sugu kampoteza nani? Mbona walio kwaruzana nao bado wapo na wanafanya biashara zina kwenda vyema tuu?

Hivi Jide ndio sababu ya Chid kula madawa?
Sijaona Ushahidi wowote usio tia shaka kubeba habari yako!
Ni nani aliyewagusa akapotea? Kuguswa maana yake nini?

Hii habari yako haina ukweli wowote Jide na Sugu ni wapenda ugomvi na mifarakano na hawakuwai kumpoteza yeyote zaidi ya kupata umaarufu kupitia mafarakano!

Hapana, Jide na Sugu walikuwa maharufu kabla ya ugomvi wowote tena miaka mingi iliyopita. So unaposema ugomvi ndio unawapa umaharufu hauwatendei haki ata kama hauwapendi.

Uyo Chidi nilisikia alikuwa anamtongoza Jide kwa sms akaonywa hakusikia. Ila una maswali na wewe kama polisi !! alafu yote yana majibu yaliyowazi.
 
Ila Jide ana miaka mingapi maana kuna siku nikicheki diary yake...uso umekomaa sana yani pamoja na ma make up lakini wapi..
Sema wanaficha umri wao ila sura zinawaumbua sana.
Emenem kazaliwa 1972 ila nahisi Jide ni mkubwa kushinda Eminem

Emi kumbe wa 72 aisee kumbe kikubwa hivyo? Ila Jide atakuwa kwenye 78 hivi 72 hajafika uko.
 
Yaani umaarufu wa Jide umetokana na mifarakano au sijakuelewa vizuri??

Back
Top Bottom