'Sugu' naye aingia chaka, achukua mkopo CRDB na kujenga hoteli kubwa jijini Mbeya

Status
Not open for further replies.
Kuna kitu kwetu sisi ngozi nyeusi nafikiri hakijakaa sawa,hivi kweli unawezaje kumtabiria njaa mpiganaji mwenzako kama huna roho nyeusi una nn sasa?,hivi mtu hata hiyo hotel haijaanza kuoperate tayari unamwombea njaa,kwa mentaliti hizi za kipimbi tutafika kweli,tena nimemkubali sana sugu kwani hajafisadi popote pale,kakopa benki na katimiza lengo lake la uwekezaji na kuwapatia ajira watz wenzetu,eeeh mola bariki wetu wenye fikra kama za sugu
 
HV aliyewaambia huyo sugu hana miradi mingine ni nani?
 
Ametoa mada kinafiki as if anajua ín and out ya sugu wakati hata kumjua hamjui zaidi ya kusoma habari zake, angeanza kwa anachojua na kudhani basi na wenginé wangekuja Tu kistaarabu
 
We unadhani malori ni biashara ya kudumu muulize gsm kapaki malori mangapi tangu magu aingie.. Nakwa vile nchi ina ukame unafikiri kuna biashara kusafirisha mazao gani sass hv?
Hivi una elimu ya biashara Au uchumi kwa ngazi yoyote ??? Usikurupukie fani za watu
 
Tunaposema hali ni ngumu ni sahihi kwa baadhi lakn sio kwa kila mtu hali ni ngumu si kweli kwamba kila mtu anaechukua mkopo kwaajil ya uwekezaj et amekosa fedha la hasha!watu wanaishi kwa akili wanachukua mikopo kuepuka bugudha na kashfa... Sometime mkopo unasimama kama security ya kumlinda mtu kuondokana na kufuatiliwa au kuhusishwa na kashfa za hujuma... By the way tupige kaz tuache kujadil watu ambao tayar wapo kwenye system na wana uhakika wa kesho... Tujadili na kushauriana fursa zilizopo ili tusukume vyema gurudumu hili zito la maendeleo
 
Unapiga tu ramli

Kwanza hilo jina la hotel sio la mtoto wake bali ni la Mama yake mzazi.

Kuna mistari ya nyimbo yake ya FREEDOM inasema

"I pay the cost to be the boss
Iknow about lost

If you dont know me, just dont talk about me

I don't lose, I either win or learn
We wanna be free, we dont wanna be rich, we just wanna be successful"
 
Safi sana sugu, Kimbe unafanya meandeleo makubwa sana jimboni kwakuwa, utasaidia sana kukuza uchumi na kutoa ajira za kutosha, ila mtoa Mada Ana wivu
 
Sikiliza Mpwa, Biashara ni ujanja wala sio Ujanja ujanja, kama unafikiri hataweza kulipa basi hayo ni mawazo yako sio yake! Lakini pia hakuna kitu kibaya kama kukatishana tamaa, akishindwa at the end atasema AT LEAST I TRIED IT, lakini mimi na wewe tutakua tunakodoa macho tu, nadhani tujenge mfumo wa ku-appreciate juhudi za Wabongo wenzetu
 
Unamponda na kumbeza Sugu kwa kupambana, kufanya kazi, kuwekeza na kutafuta kipato kwa njia halali!
Mwenzio anapambana we unamfanyia uchawi kwenye keyboard.
Una roho mbaya na akili za kipuuzi...
 
Sugu hana hela.. Mshahara wa ubunge anachukua laki tatu ukitoa madeni. Wenzie wana ma v8 yeye ana landcruiser la zamani alilopinduka nalo kitambo
Nyie ndio huwa mnasema hatuna hela. Sema sina hela usimjumlishe mwenzio maana si kila mwenye hela anajulikana maana kuna wenyenazo hata ukionyeshwa kuwa huo ndio flan mwenye hiki na kile unakataa.
 
Sawa mimi si ccm wala serikali ila ujue crdb ni benki yenye hisa za serikali na kuna influence kubwa.. Wakiamua kumbana bwana sugu kuna vipengele vingi sana kummaliza.. Na hii serikali unaijua?
Mkuu kama unajua sheria za mikopo wala usingeumiza kichwa chako kuandika yote hayo, ila kufupi jua tuu mtu huwezi kukopeshwa na taasisi yoyote kama huna kitu chenye dhamani ya hicho unachotaka kukopa, akishindwa kulipa watauza dhamana alizoweka,
Habari ya kwamba atafungwa sababu ya huo mkopo sahau,
Pia hujaweka ushahidi wa kama kweli kakopa na ni sh ngapi, kama ulivyoweka ushahidi wa huo ujenzi wa hotel unaoendelea.
 
Kwan serikal ina hotel mpk wapige marufuku kutumia hotel za watu binafsi pili ilo jina sio la mtoto wa sugu mtoto wa sugu na faiza anaitwa SASHA acha kutunga story
 
Sawa mimi si ccm wala serikali ila ujue crdb ni benki yenye hisa za serikali na kuna influence kubwa.. Wakiamua kumbana bwana sugu kuna vipengele vingi sana kummaliza.. Na hii serikali unaijua?
Kwa nini wambane kama anafanya biashara yake kihalali, ana leseni na kulipa kodi.
Acha mawazo ya kipuuzi....
Watu kama wewe ndo mnairudisha nyuma hii nchi.
Hotel ya Mbowe hivi sasa ina matatizo kutokana na ishu za kodi ambazo mwenyewe anapambana kuzitatua we unalia lia tu hapa...by the way hujaona hata wana ccm kina H.S Amon wanafunga hoteli?
Hujaona wazungu wamefunga hoteli zao na biashara za kitalii kwa sababu ya ishu za kodi na leseni?
Unataka tumini hao wote ni Chadema ndo maana wamekabwa?
Jiongeze ndugu yangu...
Wivu tu kwa Sugu..
ACHA UNAAA (kwa sauti ya Lyatonga)
 
Sawa mimi si ccm wala serikali ila ujue crdb ni benki yenye hisa za serikali na kuna influence kubwa.. Wakiamua kumbana bwana sugu kuna vipengele vingi sana kummaliza.. Na hii serikali unaijua?
Kwaio serikal inaimilik crdb?? Acha uongo wewe... Mbn magu hataki pesa ziende uko kama serkal inamiliki hisa anataka pesa zote ziende BOT msiwe nmatunga story mnakuja kutudanganya tulio na upeo
 
Point ya mtoa mada haiko sawa kwa sababu yeye anasema Sugu kaingia chaka, biashara yake itafeli kwa sababu ni Chadema....na anatoa picha kuwa hoteli ya Mbowe imepigwa na itakufa sababu ni Chadema...za wana ccm na raia wa kigeni hazioni?
 
Sawa mimi si ccm wala serikali ila ujue crdb ni benki yenye hisa za serikali na kuna influence kubwa.. Wakiamua kumbana bwana sugu kuna vipengele vingi sana kummaliza.. Na hii serikali unaijua?
Dah! Why people are too jumpy? Yaani hotel hata haijesha bado mshaanza kupiga ramli?
Wabongo tujifunze kutakiana heri kuliko shari jamani,heh!
 
At this point, I feel like I can allow myself to be goofy and take more risks, and even if I do fall on my face, I know it's not the end of the world and at least i tried to do something different.

Tumpe Kampani Sugu afikie malengo yake
 
Tz tuko na matatizo sana ! Mwanaume mwenzako anasimamisha mjengo afu unakuja kubwabwaja huku ...

Wewe unani sasa? [emoji23][emoji23]
Mimi nimetoa kama angalizo tu la kisiasa kwamba hilo deni lake lisije likamuweka mtegoni akashawishiwa kirahisi sasa mambo ya wewe una nini si mipasho hiyo ya kijinga.. Kwani mifano hai ipo ya wanasiasa kushawishiwa na vyama tawala inapokuja maswala ya kufilisiwa mfano ni john cheyo
 
Kwani Mbeya kuna ofisi za serikali kama ilivyo arusha na dodoma? Sidhani kama jamaa target yake ilikuwa ni kuitengemea serikali
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…