'Sugu' naye aingia chaka, achukua mkopo CRDB na kujenga hoteli kubwa jijini Mbeya

'Sugu' naye aingia chaka, achukua mkopo CRDB na kujenga hoteli kubwa jijini Mbeya

Status
Not open for further replies.
Amekopa shilingi ngapi?

Tupe figure mkuu sio unapiga porojo tu
 
Nimetoa mada kama mchambuzi tu sasa wanazani mimi nimekuja na ajenda za chama hii ni warning kwa mwekezaji kama kuna namna atafute suluhu mapema kwa vyoyvyote vile ccm lazima itatumia deni hili kama fursa 2020 ukizingati unyeti wa jimbo la mbeya

Kwa uandishi wako inaonekana siyo mfanya biashara, huja wahi kukopa bank na hujui taratibu za mikopo!
Nani alikuambia ukikopa bank na kushindwa kulipa unafungwa au nikosa?

Namna hii wewe ndiye msomi na hujui fursa za kifedha na namna ya kuzitumia,
acha wageni watutawale maana hatuna tunalo jua zaidi ya kubishana na chuki za kusiasa.
Wenzetu wanakopa wanajenga viwanda na mahotel sisi tunaogopa kwakua tunajua tutafungwa.
MUNGU ATUSAIDIE KUTOKA KWENYE FIKRA HIZI
 
Kwanza Sugu ni mwanamziki
Shoo yake moja anachukuliwa kwa milioni tano na kila siku anapewa ofa lakini kulingana na majukumu ya kibunge anashindwa kwenda kupiga shoo
Mdomo wake ndio mtaji wake yeye kama yeye akiamua azunguke tanzania nzima kupiga shoo atakusanya sh ngap?
Na unajuwa ana semi ngapi? zina muingizia sh ngap kwa kila mwezi

Usikurupuke Sugu ni habari ingine
Wewe jipe moyo wakati mimi nimeanza kujipanga kuinunua hoteli hiyo maana najua lazima itapigwa mnada tu. Ni suala la kusubiri na kuona.
 
Ukiwa na fursa ya kukopa bank,kopa ufanye kile ulichokusudia.Uoga wako ndiyo umaskini wako.
Mtoa mada mtu wa ajabu sana hawa ndo wanakufa maskini, mi mwenyewe mjasiriamali mdogo ila majuzi nimekopa 10m bank...sasa kwa akili za mtoa mada atasema nimeingia chaka wakati tunapiga biashara kama kawaida!
 
Sawa mimi si ccm wala serikali ila ujue crdb ni benki yenye hisa za serikali na kuna influence kubwa.. Wakiamua kumbana bwana sugu kuna vipengele vingi sana kummaliza.. Na hii serikali unaijua?

Wambane kwa lipi?
 
tehe tehe tehe napita..............
January bado haijaisha
 
Jamaa atatoboa tusikatishane tamaa we kama unaogopa kuanzisha biashara kipindi hiki piga kimya
 
Kwanza mdaiwa hafungwi,pia una uhakika gani kwamba kakopa mabilioni? atalipa tu maana Sugu ana vitega uchumi vingi pia hiyo hoteli inaweza fanya vizuri hata kama hali ya uchumi haijakaa sawa.
 
Kukopa kuna taratibu zake na hao bank hawakukopeshi ili waje wakufilisi.. tayari sana uhakika wa kupata pesa yao na wanajua wataipata vipi..siku hizi kama unaona kuwa huwezi tena kulipa deni linalokukabili unaenda pale bank mnakaa mnajadiliana na wao pia wanakupa ideas ufanye nn ili kulipa hilo deni
 
Pamoja na ubunge, muziki, hotel. Pia Sugu anamiliki malori.

Pia unapaswa kufahamu aliyekopa CRDB sio SUGU kama SUGU ni kampuni ambayo SUGU ni mmoja wa ma-director.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom