Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

Sukari ina addiction
Hamna tofauti na mateja
Wa unga,ona watu wanavyotapatapa
Humu

Ova
 
Ndipo tutagundua andazi bila chai nalo kumbe linatafunika
Yes, exactly. Ndipo tutagundua wazee wetu zama hizo walikunywa uji kwa malimao au maziwa mgando, walikula ugali, kande, mtori na mazagazaga mengine asubuhi kabla hawajaenda kazini- nyie mmekalia sukari, haya sasa.
 
Reactions: apk
Ila nchi za afrika bana,yaani kila duka unakuta kuna sukari inatoka brazil . Sasa najiuliza hivi viwanda vyetu sukari vinaweka wapi baada ya kuzalisha?

Sasa fikiria hata wewe sukari itoke brazil ni kilometer ngapi mpaka hapa? Halafu zingatia na shilingi yetu ilivolegea dhidi ya dollar
 
Mpaka nimeanza kuwaza,kwani aliesema chai ni lazima iwe na sukari badala ya chumvi ni nani...
 
Na bado hiyo sukari itauzwa bei ya chini kuliko ya kwetu , ndio tushangae . Hata ya Malawi ni bei ya chini , lakini wanatulazimisha wananchi tununue sukari yetu kwa bei ghali , hawa jamaa sijui wakoje !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…