Ni hatari Sana aisee.
Wenzetu ktk nchi zingine wapo very serious and very careful kwenye masuala kama haya.
Nakumbuka miaka ya nyuma niliwahi kusafiri kutoka Tanzania kwenda nchi Fulani nikiwa na dagaa wa kukaanga ambao walikuwa well packed ktk mifuko miwili ya nylon ya kilo tano kila mmoja, nilipofika Airport kule ugenini nilipata usumbufu mkubwa Sana kutoka kwa watu wa Food Security and Quality Control wa nchi ile. Hawakuniruhusu kuondoka airport nikiwa na wale dagaa mpaka walipoenda kuwapima kwenye Maabara zao na kuthibitika kwamba walikuwa salama kwa kuliwa na binadamu ndipo niliruhusiwa kuwachukua. Yaani wako very serious ktk suala zima la Usalama wa Chakula, hawataki masihara hata chembe.