Sukuma Gang sio watu wa kupuuzwa, itafutwe namna ya kuifuta hii itikadi ili kuleta Umoja wa Kitaifa

Falsafa itakayosimama ni ya Nyerere tu, mnajidanganya nafsi zenu na hilo Lirundi menu.
Mkuu, kwa taarifa yako ni vyema ujue kuwa hata falsafa ya Nyerere ya ujamaa na kujitegemea (aka ukomunisti mwepesi) nayo haipo nchini; ilianguka tangu 1985. Kilichodumu katika legacy yake ni umoja wa kitaifa, muungano wenye serikali mbili na chama dola (CCM) ambacho kimegeuka kuwa nyenzo kuu ya ufisadi na sasa kinatishia kusambaratisha yote: umoja wa kitaifa na muungano.

Kuhusu Magufuli naona watu hawako serious. Bila shaka elimu yetu siku hizi iko hoi sana. Watu hawajui kabisa maana ya falsafa! Magufuli alikuwa na falsafa? Ipi? Itajwe rasmi kisha yaletwe maandiko, mahojiano na hotuba zake zilizochapishwa (hata yasiyochapishwa) zikiibua na kufafanua coherently (kwa ufasaha) hicho kinachoitwa falsafa ya Magufuli.

Nyerere ana hazina kubwa ya machapisho ikiwa ni pamoja na hotuba na mahojiano yanayoakisi falsafa yake ambayo yanatumika katika vyuo, taasisi za elimu, think tanks ndani na nje ya Tanzania. Falsafa yake inachambuliwa na kupigwa critique na wanazuoni wakuu nchini, Afrika, Ulaya America na Asia. Anasifiwa, anakosolewa, analalamikiwa, anashukuriwa, anasahihishwa, anapuuzwa, n.k. na jamii mbalimbali nyakati zote (all the time).
 
Kwanza mtu ambaye hakuwahi kuandika hata kitabu kama Magufuli atatowa wapi falsafa?

Alichofanikiwa ilikuwa ni kupata kundi la mashabiki ambao wao wakiona wengine wanateswa ndio furaha yao maana kwenye issue za kutafuta mafanikio yao binafsi hawamo, hawa ni sawa na washirikina tu mateso ya mtu mwingine ndio furaha yao.
 
Wajinga hawatoisha nchi hii yaani MUNGU auwe watu kwa sababu ya shetani aliyepora hela za nchi bila ridhaa na kibali cha bunge kujenga uwanja wa ndege wa Chato kijijini kwake. Akawateua wapumbavu kama Sabaya na Makonda kisha kuwalinda awe na umuhimu kwa MUNGU?

Mnamtumikia shetani ndio maana MUNGU akamuondoa shetani Magufuli mfuateni kuzimu
 
Mna ushahidi ?
 
Msilazimsihe ukabila Tanzania.
 
Unamaanisha hata wafanyibiashara wa KARIAKOO ni kundi Hilo pia?

Kundi lililopo ni la WALIONACHO Wachache vs WASIONACHO kitu ambao ni wengi.

Hayo makundi mengine ni ya kufikirika. Na viongozi ndo waasisi walidhani wanaweza kutugawa Ili kututawala.

Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA inarudi Kwa mstari.

Aamen.
 
Falsafa inayoishi ni ya mwalimu Nyerere pekee yake. Wengine ni utapeli.
 
Sukuma gang ni lidude likubwa sana watawala wasipoangalia litakuja kuwameza one day.

Wanazani sukuma gang ni wasukuma tu la hasha, bali ni watu woote wanaoamini katika sera za Jemedali Magufuli
Upumbavu mtupu kama ni dude kubwa mnashindwaje kukiamusha na mkafanya mabadiliko mnayoyataka.
 
Unaiwaza CHADEMA tu kila siku. Mgawanyiko walete CCM lawama apewe CHADEMA.
 
Mbona watanzania wazamani ndio wenye akili kuliko wa Sasa hivi? Punguza matusi.
 
Katiba Bado inatambua uchumi wa ujamaa na kujitegemea.
 
Sukuma gang ni watu wabinafsi na wanaoamini kwenye siasa za fujo na kuteka na kuua wanaowakosoa. Mwenendo wao huu wakibanwa zaidi mwisho wataingia msituni. Waasi wa kwanza katika Taifa letu hili watakuwa sukuma gang.
Politics ni game,na ni mchezo mchafu duniani kote unatambulika hivyo kwa kuwa ndipo kwenye masilahi.kuuana na kupotezana ni kawaida kwenye politics-watu wanatofautiana tu njia za kupotezana wengine wanafanya direct kama Magufuli na wengine wanafanya kwa siri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…