Sultan Tamba na Mussa Banzi Chukueni maua yenu japo bado tunawadai muendelezo wa baadhi ya filamu. Kanumba alichangia kuua soko la filamu

Sultan Tamba na Mussa Banzi Chukueni maua yenu japo bado tunawadai muendelezo wa baadhi ya filamu. Kanumba alichangia kuua soko la filamu

Kwa nini mtitu hapendi spotlight, amefanya makubwa lakini naona hataki kuwa mbele ya camera kabisa na sasa yuko wapi
Si kwamba hapendi spotlight bali alikuwa hataki kujichanganya na wasanii, kifupi anawadharau. Kwa sasa yupo na mishe zingine maana amepigwa sana vita na Wahindi (hasa Steps), walifikia hatua ya kumletea TRA kwa kisingizio kuwa anakwepa kodi, akapigwa hela nyingi sana (ili kufirisiwa), kilichomsaidia ni kwamba alikuwa pia amewekeza nchini Nigeria...

Ila ukweli Mtitu ana mchango mkubwa sana kwenye film industry ya Tanzania, na anaijua vizuri industry, pengine bila yeye baadhi ya wasanii kama Kanumba wasingefika hapo...
 
Si kwamba hapendi spotlight bali alikuwa hataki kujichanganya na wasanii, kifupi anawadharau. Kwa sasa yupo na mishe zingine maana amepigwa sana vita na Wahindi (hasa Steps), walifikia hatua ya kumletea TRA kwa kisingizio kuwa anakwepa kodi, akapigwa hela nyingi sana (ili kufirisiwa), kilichomsaidia ni kwamba alikuwa pia amewekeza nchini Nigeria...

Ila ukweli Mtitu ana mchango mkubwa sana kwenye film industry ya Tanzania, na anaijua vizuri industry, pengine bila yeye baadhi ya wasanii kama Kanumba wasingefika hapo...
Yeah anaonekana ni mtu makini na shule ipo. Nahisi ni creative genius na pia introvert hivyo inakuwa ngumu kufit kwenye entertainment industry haswa ya Tanzania ambayo professionalism ni ndogo sana.

Uzuri kwenye entertainment na media nimechangamana nayo sana na kiukweli, mtu mwenye akili na kujielewa, ni ngumu kupata space haswa kwa nyakati. Nimeona comment yako inakuonesha kama mtu uliye jikoni kwenye movies, natumai siku moja mambo yatabadilika
 
Nimeona comment yako inakuonesha kama mtu uliye jikoni kwenye movies, natumai siku moja mambo yatabadilika

Natumaini siku moja mambo yatabadilika ila ni pale tu wasanii wakiacha kuchanganya kazi na siasa, maana huku ndo kulikojaa machawa promax na makuwadi wa kuwakuwadia wakubwa totoz.

Dah, ngoja niishie hapa...
 
Natumaini siku moja mambo yatabadilika ila ni pale tu wasanii wakiacha kuchanganya kazi na siasa, maana huku ndo kulikojaa machawa promax na makuwadi wa kuwakuwadia wakubwa totoz.

Dah, ngoja niishie hapa...

Entertainment industry yote imeoza kwenye mambo hayo mkuu na hayaishi. Hata Nigeria yapo ila tu kwenye kazi, umakini usiathirike
 
Cindy na Candy hivi yule demu anaitwa nani,?
Cindy/Candy jina lake ni Jesca Oscarion kwa bahati mbaya alifariki miaka kadhaa iliyopita.
IMG_20240219_222050.jpg
 
Issue ya movies kuwa na Part 1 na Part 2 nadhani msambazaji alikuwa anawalazimisha na wenyewe walililalamikia sana.

Kingine kinachinisikitisha ni kuwa mtitu wa game first quality huwa hatajwi ilhali yeye ndio alitengeneza movie za mwanzo za Kanumba na Ray kama Johari, sikitiko langu, A point of No return, oprah na nyingine nyingi

Huyu jamaa movies zake zilikuwa kali ila zilizohit ni zile zenye mahadhi ya kinaija

Kingine, Mussa Banzi na sultani, movies zao zilikuwa na uhalisia sana sanaa na story kali ila kwenye uigizaji kuna walakini. Kuna kama game of love, watu wanaigiza kama wanaigiza maneno waliyokariri badala ya kuuvaa uhusika
Jeff na Blandina kuna baadhi ya scene walipuyanga
 
Jina la uigizaji anaitwa Mikala ,jina halisi nimelisahau.

Aliwahi kuigiza pia filamu inaitwa The lost twins .Humo ndani amecheza na mama Monalisa (Natasha) (Suzan Lewis) ,Kanumba nk.

BTW huyo dada amefariki kitambo kwa ajali ya gari huko Marekani ila ana mdogo wake wanafanana mno (99%) .

Account ya IG ni hii luckiya07
Umechanganya madesa mkuu. Cindy sio mikala. Mikala ni huyu hapa japo wote wameshafariki.
mqdefault.jpg
 
Sultani Tamba movies zake ziliegemea vitisho zaidi ila Mussa Banzi alikuwa anapiga kotekote mapenzi na vitisho.
Kuna movie ya Sultan Tamba inaitwa Wasiwasi, wanaume wawili wanagonga mlango usiku wa manane, mlango ulipofanguliwa wanauliza wapi kuna msiba.
Aliefungua mlango anashangaa na kusema hana taarifa za msiba, wakamuambia msiba upo tena ni wa mtu wako muhimu fanya utafiti utajua. Wanaondoka!
Yule jamaa hakuendelea kulala, akatoka kulelekea kwa mchumba wake anaetaka kumuoa karibuni, kufika tu anasikia kama mtu anaugulia maumivu kupitia dirishani. Kuchungulia anakuta mchumba wake amepigwa kisu cha tumbo.
Akaenda haraka kwenye mlango mkubwa ambao ulikuwa wazi akaingia ndani amuokoe ila ikashindikana.
Mama yake na yule binti nae akaamka maana alisikia sauti na kukurukakara, kuingia kwa binti yake anakuta keshakufa na mchumba wake ndio kashikilia kisu.
Ikaonekana yeye ndio kaua jumba bovu likamuangikia.
Na kuna nyingine inaitwa Miwani meusi!
Yes filamu nyingi za Sultan Tamba zilikuwa filamu zakutisha tisha na ndicho kitu nilichokiandika mwanzoni kabisa mwa uzi.
 
Sultan Tamba na kundi lake la Tamba Arts group ambapo humo ndani unakutana na waigizaji kama Riyama Ally, Mwajabu Kazimili (Bi Nyamisi),Rehema Msangule (Doreen Nsyuka),Sanjo,Ringo,Chilisosi, nk

Mussa Banzi na kundi lake la White Elephant waigizaji wake kama vile Ramadhan Ally (Main character kwenye sijui la kufa, My Darling nk,Evans Moshi (Mack wa shumileta),Jenifer Kyaka (Odama), Jenifer Mwaipaja (Shumileta) ,mganga ndele nk.

Japo kuna waigizaji walikuwa wanaigiza huku na huku yani kwa Sultan Tamba na kwa Mussa Banzi na kuna wale ambao wapo either kwa Sultan Tamba au kwa Mussa Banzi.

Tuendelee,

Kifupi hawa jamaa ndio walioleta mapinduzi kwenye suala zima la filamu na filamu zao kwa kiasi kikubwa yaliakisi maisha halisi ya mtanzania .

Sultan Tamba alikuwa bingwa zaidi kwenye filamu za kutisha kuliko filamu za kawaida ,mfn filamu kama Nsyuka, Roho mbili, Mama Yangu anakula nyama za watu, Mzee wa busara, Chite Ukae,Sanda nyeusi ,Tabana, Jinamizi , Mume bwege,Girlfriend Nk

  1. Mussa Banzi alikuwa yupo vizuri zaidi kwenye filamu za mapenzi kuliko filamu za kutisha mfano Cindy na Candy, Dear Doctor,Shenaiza, Sikio la kufa ,My Darling,The game of love, Odama, Veronica, Zogo kisiwa Cha mauti, Kihongwe, Kinyamkela,Karibu paradiso,Joanita nk

Filamu tunazowadai muendelezo wake kwa hamu

1)Chite Ukae -Iliishia part one na walituahidi kuleta muendelezo wake ila mpaka leo kimya.

Hii ni miongoni mwa filamu zenye uchawi wa hali ya juu , tunamuona mwanadada Doreen nsyuka(Rehema Msangule) akipitia misukosuko mingi ya kichawi na akawa ametembea vilinge vingi ila jibu alilopewa ni Moja tu inabidi afariki kwa muda wa siku 3 kisha atafufuka upya kwa njia za kichawi/kiganga.

Misukosuko huu aliupata pia kwenye filamu ya Nsyuka part 2,Doreen alifariki ili Nsyuka atulizwe akaja kufufuka siku ya tatu wakati gari lipo njiani linaelekea makaburini.

2)Kihongwe (Nguvu za Giza)- Hii filamu ilikuwa nayo inasisimua sana, tunamuona muigizaji Ibrahimu Mbwana (bad boy fighter)(Desmond) kama mtu tajiri sana,sasa rafiki wa mke wake anaitwa Nolinda akaingilia penzini ili amtapeli Desmond Mali zake na hizo Mali Nolinda akatumie na mwanaume mwengine anayempenda kwa dhati.

Kwa njia za kawaida Nolinda alifanikiwa tu kumchuma pesa za kawaida ila akawa haridhiki anataka apate mpaka nyumba na magari ila ikashindikana ndipo akahamia kwenye upande wa nguvu za giza ,huko napo akakwama mara mbili kwa kukosea masharti ya mganga ndele, njia ya mwisho aliyopewa ni kuchukua kivuli Cha Desmond kifukiwe makaburini kwa siku 7 kisha kifukuliwe na kutunzwa kwenye jeneza ambalo atakuwa anakaa nalo Nolinda siku zote ,akitaka chochote anaenda kwenye huo mawili anauongelesha na Desmond mzima anatimiza.

Kwa hiyo kilichofanyika, ilichukuliwa bastola ikafanyiwa mambo ya kishirikina kisha Nolinda akaenda kumuulia nayo Desmond ,ikapatikana miili miwili (mmoja kama kivuli) , huo mawili kivuli ndio uliozikwa kwa siku saba na kufufuliwa .

Nolinda alifanikiwa kumtapeli parefu Desmond kishirikina alijengewa nyumba, na mpenzi wake naye akajengewa nyumba na Desmond akimdanganya ni kaka yake amepata matatizo ya kudhulumiwa nyumba na hana pa kuishi hivyo akamuomba amnunulie nyumba Desmond akafanya hivyo.

Mwisho wa filamu tunaona Desmond anapata ajali ya kweli na anakufa kifo cha kweli baada ya kupewa laana na mama yake baada ya kumfukuza mama yake mzazi na mkewe wa ndoa.

Lakini tuliambiwa kutakuwa na muendelezo wa Kihongwe sehemu ya 2 mpaka leo kimya.

3)Shumileta sehemu ya 3.

Tunaona Evance Mushi (Mack) anafanikiwa kurudi duniani baada ya kutokea vita kubwa huko ujinini kati ya Shumileta na mdogo wake wakimgambania Mack.

Tunataka tuone muendelezo utakuaje baada ya hapo maana tuliahidiwa muendelezo, wale makini hawakufungwa na Mack haikuwa na Kinga yoyote ya kutoendelea kusumbuliwa na hao majini ,sasa je nini kitaendelea baada ya hapo na uzuri Main Characters wote wapo hai mpaka leo .

Filamu zingine zilizohitaji muendelezo ni Kinyamkela ,Tabana ,Zogo kisiwa Cha mauti nk.


Tuendelee.

Mbali na Musa na Sultan Tamba
, mwingine aliyejitahidi tahidi alikuwa Jumanne Kihangala(Tuesday Kihangala) na alipata umaarufu zaidi na tamthilia ya jumba la dhahabu, amewapika wengi kupitia kundi lake la fukuto,kama vile Miriam Jolwa(Jini Kabula),Jackline Pentzel,Baga Mteme,Kitale,Nikita,nk

Tuendelee

Baada ya hawa jamaa kutamba kwa muda mrefu ujio wa Steven Kanumba ukaja kuharibu filamu za bongo kwa kiasi kikubwa na akajitengenezea mazingira ya yeye peke yake kung'aa.

Makosa ya Kanumba yalikuwa ni haya .

  • Kutuletea waigizaji kwa kuangalia urafiki uliopo baina yao bila kujali kipaji alichonacho.Kanumba alikuwa mtu wa kuokota okota akikuona upo smart na kuna filamu anataka kutoa anakuita ukaigize hata kama huna kipaji anakwambia utajulia huko huko .Na hili baadhi ya waigizaji waliwahi kulisema mfano Jackline Wolper ,Wema Sepetu,Kenny,Hao akina Hemed ,Mlela nk.
  • Zamani waigizaji wengi walilelewa na kupikwa kwenye vikundi /makundi ya Sanaa lakini yeye kwa Kanumba ilikuwa tofauti anakubeba tu ukaigize ukiwa na muonekano mzuri automatically utapendwa tu hata usipojua kuigiza.
  • Kanumba ndiye muanzilishi wa filamu ambazo zinakosa uhalisia mfano white maria, magic house nk
  • Kanumba ndiye aliyeanza kuharibu filamu za bongo kwa kulazimisha kila filamu iwe na part one na part two hata kama ni filamu ya saa Moja kitu ambacho zamani hakikuwepo,Zamani ukiona filamu ina part one na two basi ujue ina deserve maana filamu nyingi za zamani zilikuwa zinachukua si chini ya saa moja na nusu kwa filamu moja.Na ukiona kuna muendelezo wa part two basi lazima muisubiri kwa hamu tofauti na kipindi cha Kanumba.
  • Kilichombeba Kanumba enzi zake ni kule kujipendekeza pendekeza kwa wanaigeria kuomba collabo kinyume na hapo kawaida tu nk.


Itaendelea
Vipi mkuu mbona makasiliko ...
 
Back
Top Bottom