Sultani Tamba movies zake ziliegemea vitisho zaidi ila Mussa Banzi alikuwa anapiga kotekote mapenzi na vitisho.
Kuna movie ya Sultan Tamba inaitwa Wasiwasi, wanaume wawili wanagonga mlango usiku wa manane, mlango ulipofanguliwa wanauliza wapi kuna msiba.
Aliefungua mlango anashangaa na kusema hana taarifa za msiba, wakamuambia msiba upo tena ni wa mtu wako muhimu fanya utafiti utajua. Wanaondoka!
Yule jamaa hakuendelea kulala, akatoka kulelekea kwa mchumba wake anaetaka kumuoa karibuni, kufika tu anasikia kama mtu anaugulia maumivu kupitia dirishani. Kuchungulia anakuta mchumba wake amepigwa kisu cha tumbo.
Akaenda haraka kwenye mlango mkubwa ambao ulikuwa wazi akaingia ndani amuokoe ila ikashindikana.
Mama yake na yule binti nae akaamka maana alisikia sauti na kukurukakara, kuingia kwa binti yake anakuta keshakufa na mchumba wake ndio kashikilia kisu.
Ikaonekana yeye ndio kaua jumba bovu likamuangikia.
Na kuna nyingine inaitwa Miwani meusi!