Sultani gani aliye na shutuma za mauaji Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Zipi ni propaganda sasa, kama unakiri wazi wazi kuwa waarabu walijishughulisha na utumwa Zanzibar
Hiram,
Huu ni ushauri wangu kwako.

Ukitaka kuwa msomi mzuri jilazimishe kuweka kichwa chako
wazi kupokea fikra mpya.

Ukikifunga kichwa chako daima utakuwa na fikra hizo hizo
zako hutojifunza kitu kipya.

Hebu nenda kasome Transatlantic Slave Trade na Belgian
Slavery.
 
Nimepokea ushauri wako na mimi nakupa ushauri nenda kasome kuhusiana na Moresbay Treaty 1822
 
Nimepokea ushauri wako na mimi nakupa ushauri nenda kasome kuhusiana na Moresbay Treaty 1822
Hiram,
Nimeusoma miaka mingi sana iliyopita.
Huwa nacheka sana mtu anaponiambia nikasome.

Unaitwa ''Moresby'' si ''Moresbay.''

Kuna mahali hapa jamvini nilieleza kuwa miaka mingi nyuma nilikuwa
Blantyre, kijiji kidogo nje ya Glasgow, Scotland alikozaliwa David Livingstone.

Kijiji hiki kimeguezwa kuwa moja ya makumbusho ya taifa la Uingereza.
Huwezi kufika lakini hebu fanya utafiti ujue kuna nini hapo.
 
Mzee acha porojo hebu leta historia yako juu ya Zanzibar tuipime na ukileta hapa leta historia na sio hisia na udini
Upime nini kwa kuwa wewe una uwezo gani wa kupima watu wengine? Kasuku au panya wa mpiga filimbi wa Hamelin
 

Hakika hasira ni mtambo wa khasara.........kuniita miye "bibi" yako ni dhahiri ya mapungufu yako hata kwa umri ulonao......kwa heri "bwana"
 
Hakika hasira ni mtambo wa khasara.........kuniita miye "bibi" yako ni dhahiri ya mapungufu yako hata kwa umri ulonao......kwa heri "bwana"
Safari,
Siwezi kukosa adabu kiasi hiki.
Soma vizuri hilo bandiko na hiyo sentensi.

Nimesema:''Bibi yangu (yaani nyanya yangu)
akiniita mimi ''Mwamedi.''

Sina maana wewe nakuita bibi yangu mie.

Niwie radhi sana ndugu yangu ikiwa umedhani
nimekutukana.

Siwezi kufanya kitu kama hicho.
 
Nimekwambia kwaheri "bwana"
Safari,
Unaniaga ukiwa katika fikra kuwa nimekutukana.
Hiki ndicho kinachonitia unyonge.

Ndugu yangu hebu soma jibu langu na tusafiane
nia.

Sijakutukana mdogo wangu.
Labda niongeze.

Umeniita, ''Mhamedi.''
Jina langu halitamkwi hivyo.

Nami nikakwambia kuwa bibi yangu nikikusudia
nyanya yangu na yeye akiniita ''Mwamedi.''

Siku akifurahi huwa ananiita ''Bwana.''
Kwa utamaduni wa pwani nyanya ni ''mke'' wa mjukuu.

Wakati mwingine akiniita, ''mume wangu.''

Hiyo ''bwana'' sijakukusudia wewe.
Nielewe ndugu yangu.
 
Safari,
Unaniaga ukiwa katika fikra kuwa nimekutukana.
Hiki ndicho kinachonitia unyonge.

Ndugu yangu hebu soma jibu langu na tusafiane
nia.

Sijakutukana mdogo wangu.
Pamoja na tafauti zetu kisiasa na kimaisha bado nakuheshimu kwa kuwa u mcha mungu na naamini hata lafajiri hii umetoka msikitini........mimi nimekusamehe "bwana". Hakuna haja ya kulumbana
 
Pamoja na tafauti zetu kisiasa na kimaisha bado nakuheshimu kwa kuwa u mcha mungu na naamini hata lafajiri hii umetoka msikitini........mimi nimekusamehe "bwana". Hakuna haja ya kulumbana
Safari,
Sawa umenisamehe nakushukuru.
Lakini nakuapia kwa jina la Allah sijakutukana.
 
Mkuu unahoja.

Lakini kuna tofauti Kati ya slavely kama mfumo waaisha (mode of production) katika human evolution Na Slave kama Slave trade!
Jamii zote zimepitia mfumo wa "utumwa" lakini sio jamii zote zimefanya au kupitia biashara ya utumwa!
 
Mkuu unahoja.

Lakini kuna tofauti Kati ya slavely kama mfumo waaisha (mode of production) katika human evolution Na Slave kama Slave trade!
Jamii zote zimepitia mfumo wa "utumwa" lakini sio jamii zote zimefanya au kupitia biashara ya utumwa!
Does it change the fact on how the slaves were obtained? And the pain?

FYI kabla ya pesa kuwepo watumwa walikuwa wanachukuliwa kwa nguvu. No payment or compensation na medium ilikuwa ni vita. Kijiji chenu kinavamiwa na mnachukuliwa utumwani. Hata huku kwetu akina Mirambo na Mkwawa (japo leo ni mashujaa) walifanya sana haya mambo wakati ule. Yule Tipu Tip baadae alikuwa nawanunua hawa watumwa kutoka kwa hao mashujaa wetu. Historia bahati mbaya ni mbaya
 
Mkuu Safari

Nimekubaliana nawe katika quote niliyoikoti awali. Na nilichokielezea ni vitu viwili tofauti Na hiki ukisemacho.

Biashara ya utumwa Na utumwa kama mfumo wa kimaisha ambazo jamii zote zimepitia baada ya ujima (Communism) ni tofauti Na utumwa unaoulezea hapa!

Utumwa huu wa kina Isike, Sultani, Na Tib tibu ni zao la ubebari uliovuka mipaka (imperialism) ambao mtumwa ni bidhaa. Lakini utumwa as mode of production haikuwa utumwa wa matiki ya utumwa wa imperialism!
 
ENOUGH..YATOSHA....MSHAPATA MLIYOPATA...KAMA MATESO MSHAWAPA..WAACHIENI MASHEKH WETU

 
Kuna sinema inaitwa Afrika Addio / Africa blood and guts , inaonyesha live jinsi waarabu walivyokusanywa na kuuawa kikatili siku ya mapinduzi 1964. Pande zote za kisiasa zanzibar wana makosa ya kihistoria. Wanahitaji truth and reconciliation ili vizazi vijavyo viishi kwa mshikamano.
 
Kweli kabisa wote wanamakosa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…