SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Ndugu wananchi, leo nakuja na mada ngumu kidogo.
Mazoea ya kitu hayahalalishi kwamba jambo hilo ni sawa. Linaweza kuwa tatizo lakini mazoea yakakufanya usione umuhimu wa kulitatua.
Tumekuwa tunaishi miaka mingi na uwepo wa soko la samaki pale Kivukoni au wengi wanapaita Ferry. Soko lile pamoja na faida kubwa za upatikanaji wa samaki, lakini limekuja na harufu kali ya shombo la samaki inayosambaa maeneo yale hadi karibia na Posta na kama umekuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, unawezekana ukaisikia mbali zaidi.
Bila kuongea mengi, naomba niseme hili ni tatizo kubwa. Maeneo yale kuna mahoteli mbalimbali makubwa, ni njia ya kwenda Kigamboni kwenye mahoteli na beach mbalimbali, tujiulize wageni wanasikiaje pale wanapokumbana na hali hii. Mimi ni mzaliwa wa Dar lakini ile harufu sijawahi kuizoea, kwa mgeni itakuwaje?
Binafsi naona kuna aina tatu za utatuzi wa hili tatizo:
Kwanza, ni kulijengea soko la samaki pale liwe la ndani na siyo la wazi kama ilivyo sasa. Pia ku control shughuli zote za sokoni pale zisifanyike nje.
Pili, kama la kwanza haliwezekani, ni kuwa na kampeni ya kusafisha hali ya hewa hasa maeneo yale. Hili zoezi sina utaalamu nalo ingawa nahisi litakuwa na gharama kubwa kwa hiyo silipendekezi sana.
Tatu, ni kulihamisha kabisa soko lihamie maeneo ya Kigamboni. Na hata huko nako, lisiwe soko la wazi ili isije kuwa kama tunahamisha tu tatizo.
Mada hii imeletwa kwa maslahi ya taifa na ustawi wa jamii yetu.
NB: Nakerwa sana na hali ya uchafu na harufu kwenye masoko yetu kwa ujumla.