Suluhisho la Kudumu la Kero Zote za Muungano, na Dawa ya Kutibu Sumu ya Ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari ni Kuwa na Serikali Moja ya JMT?

Visiwa vya Unguja na Pemba vikiwa wilaya we unaathirika kivipi?
Athari zake ni hizi.
1. Utaifa wa Zanzibar utakufa na kuzikwa milele. (Waza familia yako (familia ya kimasikini na kinyonge) na familia ya kaka yako (yenye utajiri na nguvu) ziungane ziwe familia moja, baba wa familia awe mmoja tu ili kumiliki na kutawala na wengine wote muwe chini yake, vipi utakuwa tayari!)

2. Zanzibar haitapata chochote kipya zaidi ya kutoa karibu vyote kwenda Tanganyika. Kifupi hali ya maisha itakuwa mbaya Zanzibar. (Kumbuka kwa sasa Zanzibar inakula matunda ya kipato kutoka Tanganyika kuliko hata Zanzibar inachokizalisha yenyewe, na hali hiyo itakoma mara moja Zanzibar ikiwa sehemu ya wilaya za Tanzania)

3. Ndani ya mwaka mmoja tu, huenda Zanzibar itakuwa imemezwa na watanganyika.
 
Maisha ni mafupi lakini safari yake ni ndefu sana πŸ‘πŸ›«
 
tangu mwanzo,
maoni ya wengi na ndoto za mwl. J.K Nyerere yako sambamba kabisa na ya wanainchi wengi wa Jamuhuri ya Muungano wa wa Tanzania, kwa macho, kwa maoni, mtazamo na numbers. Haihitaji elimu ya ubobevu kuliona na kulibaini hili πŸ’
Kati ya Nyerere na maoni ya wengi utachagua lipi?
 
Mami unatafuta kusomewa albadr na waunguja wewe.
 
tangu mwanzo,
maoni ya wengi na ndoto za mwl. J.K Nyerere yako sambamba kabisa na ya wanainchi wengi wa Jamuhuri ya Muungano wa wa Tanzania, kwa macho, kwa maoni, mtazamo na numbers. Haihitaji elimu ya ubobevu kuliona na kulibaini hili πŸ’
Basi kila Nchi (Tanganyika na Zanzibar)ipigie kura tujue kweli.
 
JokaKuu Nguruvi3 .....

Rasimu ya katiba iliyoandikwa na kina Warioba ilishatoa suluhisho la kudumu.
zitto junior
 
Wanasiasa wanaopigania serikali tatu hawajali wala kuzingatia maslahi yaTanganyika. Ifike wakati wasipewe hata maiki kuongea kwenye umma.

Muungano unatakiwa kubaki hivyo hivyo ulivyo au tufikie serikali moja.

Wajukuu zetu hawatatusamehe kuruhusu wawe na majirani Mujahideen na kupambana na makundi ya kina Mulla Mohamed.
 
Majibu ya muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar yapo kwenye rasimu ya Jaji Joseph Sinde Warioba,Hivyo hizo hoja zako za kikasuku hazina faida yoyote zaidi ya kuwa mbabaishaji tu.

Wananchi wa pande zote mbili washa toa maoni ya namna gani muungano unapaswa kuwa,hivyo basi mambo ya TANU na ASP ni zilipendwa hayana nafasi kwa kizazi cha sasa.

Hizi sio zama za zidumu fikra za Mwenyekiti.
 
Serikali moja ya Kidemokrasia inayowajibika kwa Wananchi ndio suluhisho muafaka juu ya kero zote za Muungano nchini Tanzania.
Jambo ambalo mnasahau ni kwamba muundo wa Muungano usha tolewa suluhu na wananchi wa pande zote mbili.

Wazanzibar hawako tayali kupoteza historia yao,Utamaduni wao na utambulisho wao,ambao umedumu karne nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…