Suluhisho la Kudumu la Kero Zote za Muungano, na Dawa ya Kutibu Sumu ya Ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari ni Kuwa na Serikali Moja ya JMT?

Suluhisho la kudumu ni kuuvunja huu muungano batili. Kinachoitwa kero kimekuwepo tangu 1964 mpaka leo.
Utazalisha KERO za kimipaka Kati ya Zanzibar na Tanganyika yawezekana ikatokea Vita kubwa sana isiyokoma.

Bahari ni uchumi kwa taifa lolote hupaswi kuwa na mtu mwingine mwenye control ya bahari jirani yako.

Kiusalama na kiuchumi Tanganyika itaathirika zaidi na kuvunjika kwa Muungano.
 
Nashukuru kwa taarifa mkuu. Nimefahamu kuwa:
1. Mwalimu Nyerere na CCM ndiyo maadui wakuu wa tamanio la Watanzania, Serikali tatu. Wawakilishi wa wananchi walipitisha azimio la kuirejesha Serikali ya Tanganyika lakini utekelezaji ukashindikana kwa sababu ya misimamo ya Nyerere na CCM.

2. Hayati Nyerere hakuwa akiitakia mema Tanganyika. Aliridhika kuona Zanzibar inanona kwa vinono vya Tanganyika huku Tanganyika ikishindwa kuvifaidi vyake.

3. Na wewe umeungana na maadui wa Tanganyika. Hutaki kuona Tanganyika inahuishwa, jambo ambalo halitafanikiwa asilani.

Kwa taarifa tu, haitakaa itokee Wazanzibar waukubali kuipoteza nchi yao, na Watanganyika nao hawatakubali nchi yao iendelee kuwekwa mafichoni.

Serikali moja ni ndoto isiyoweza kutimia.

Kama tunataka usawa, twende na Serikali tatu.
 
✅✅✅
 
Kabla ya huo muungano batili mipaka haikuwepo?!
 
Wabheja sana.

Bunge lilipitisha azimio la kuitaka serikali kuandaa utaratibu wa kwenda kwenye mfumo wa serikali tatu.

Azimio hilo bado lipo japo halikutekelezwa.

Hatuna wanasheria wa kuweza kuitaka mahakama kuilazimisha serikali kutekeleza azimio la bunge?
 
muono wa waTanganyika kwa Zanzibar ni ni wakikoloni zaidi, Eti Zanziba iwe mkoa ydani ya Tanganyika, Munaweza uwafata Rwanda nao muwambie kuwa wawe mkoa ndani Ya Tanganyika?
Rwanda pamoja na Burundi ilikuwa moja ya majimbo ndani ya German east Africa mpaka 1922, jimbo likiitwa Rwanda Urundi.
 
Wnasheria wapo na mahakama ipo, lakini mahakama haina "misuli" ya kuulazimisha muhimili uliojichimbia chini zaidi kutimiza matakwa ya matakwa ya Katiba.
 
hata maeneo ya Tanganyika yalikuwa ndani ya eneo la Zanzibar mpka early 1900's
Jaribu kuwa specific.

Hiyo early 1900's ni mwaka gani, na maeneo gani yaliyokuwa chini ya Zanzibar, na yalihama Toka Zanzibar kwa mkataba au makubaliano yepi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…