Suluhisho la matatizo ya bandarini: Iundwe Wizara itakayodeal na masuala ya Bandari tu

Suluhisho la matatizo ya bandarini: Iundwe Wizara itakayodeal na masuala ya Bandari tu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Nimewaza hapa na kujiuliza , je, ningekuwa kiongozi ningetatua vipi kadhia za Bandari ya Dar es Salaam na Bandari zingine kwa manufaa ya taifa?

Suluhisho nambari moja ni kuunda wizara maalumu itakayodeal na masuala ya Bandari tu.

Bandari ya Dar es Salaam pekee inaingiza fedha nyingi zaidi ya Wizara kadhaa. Jambo la maana ndilo la kulitilia u serious hiyo ndio akili.
Kuna wizara hazina hata faida kwa taifa hili. Ikiwezekana zivunjwe na nguvu ipelekwe Bandarini huko pesa ikusanywe na huduma bora zitolewe nchi isonge mbele.
 
Kwamba kwa akili yako Taasisi zote za serikali zinazofanya kazi bandarini hazitoshi, Waziri(Mwanasiasa) ndo ataweza? Yan kwamba TPA yenyewe, TASAC, TRA, TBS, TISS, JWATZ, Police, Suma JKT....hawatoshi, Waziri wa Bandari(Tuseme mtu kama Joseph Musukuma, au Lusinde, au Gwajima, au Deo Sanga) ndo wataweza?
Taasisi zingine pale TPA zinaongeza foleni tu for sure.
 
Kila tatizo likuindiwa wizara hii nchi itakuwa na wizara milioni
 
Tunahitaji wizara chache kuliko tulizo nazo kwa sasa na pia tunahitaji idara nyingi imara na makini kushughulika mambo ya taifa.

Hatuhutaji hizi Wizara; ya habarai na michezo, ya katiba na shera, ya sera na bunge , ya uvuvi na mifugo, ya ardhi, na hiyu ya bandari pia haihitajiki
 
Hello!

Kuna kipindi niliwahi kuleta Uzi hapa juu ya suala hili .

Bandarini kuna changamoto nyingi kwakuwa ndio sehemu ambayo uchumi wa nchi hii umejificha.

Hivyo basi ili kupunguza au kuondoa changamoto za bandari zetu sasa ni vyema iundwe wizara ya Bandari.

Nimemaliza
 
Hili sio suluhisho! Bandari sio siasa! Bandari ni issue technical!

Kuunda wizara ni kuongeza mzigo wa watu wa kuhudumiwa na serikali wakati hujatatua kiini cha tatizo
 
Wewe ndiye uliyeshauri kwenye mjadala mmoja clubhouse kuundwe wizara ya machinga ili kukabiliana na changamoto za wamachinga nchini!
 
Upigaji hautaisha,ukienda huko Mitaani shujaa wa Wananchi ni yule Mpigaji chronic anasifiwa na Jamii nzima.

Hii ndio Jamii iliyomsifu Dokta Shika kuwa kawapiga Warusi Dola za kutosha.

Tumelijenga Taifa letu kuwa la Wezi.

Anyway Bariadi Chenge anasifika sana.
 
Bandari haiendeshwi kiivyo wapo waanze kufumua bongo wote wezi kupitisha Sheria kali tu dhidi yao

Tukishindwa tulete mkoloni tu aje kumanage mbaya anaweza kuja kijana tu akaweka mambo sawa sema ndo ivyo kila siku mazee
 
Wewe ndiye uliyeshauri kwenye mjadala mmoja clubhouse kuundwe wizara ya machinga ili kukabiliana na changamoto za wamachinga nchini!
Hapana. Kuunda wizara ya machinga ni sawa na kuubariki ujinga na umaskini.
Machinga wenyewe wanauza bidhaa za mchina. Wamachinga wanajenga uchumi wa China kwa kiasi kikubwa na si uchumi wa Tanzania
 
Sasa hivi Wakenya wanagawiwa Vitambulisho vya Nida kwa Laki mbili unusu bila bughudha.

Piga Mwingi nenda zako Taifa limejaa Wezi hili.

No way out😥
 
Back
Top Bottom