Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Ni miaka inakaribia 20 toka Uwanja wa Taifa maarufu kama Benjamin Mkapa Stadium, au Kwa Mkapa au Lupaso uzinduliwe, tumeshuhudia mfululizo wa matatizo mengi hususan makubwa kama yafuatayo;
1. Kuvunjwa kwa viti vya kukalia kutoka kwenye majukwa ya moja ya timu kubwa
2. Kuvunjika kwa milango na masinki ya vyoo kwenye sehemu za kujihifadhi
3. Kuchakaa kwa pitch ya kuchezea mpira kutokana na ukosefu wa maji
4. Watazamaji kuvunja geti na kuingia bila utaratibu
6. Kukatika kwa umeme wakati wa mechi za kimataifa ikiwa ni ni pamoja na tukio la kwenye mechi ya jana kati ya Yanga na Rivers ya Nigeria
Tukubaliane tu kuwa Waafrika hasa Watanzania hatujui thamani ya raslimali (sense of value) tuliyonayo ndiyo maana tunaharibu kwa makusudi au kwa ujinga tu (bad mindset)
Serikali duniani kote hasina ufanisi kwenye menejimenti ya taasisi kama hizi.
Nashauri Serikali IBINAFSISHE usimamizi wa uwanja huu kwa kupitia zabuni ya wazi. Serikali ibakie kukusanya maduhuri yake na kodi za kisheria.
Nawasilisha