Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Moja kwa moja kwenye mada, mods msiuunge huu uzi na nyuzi nyingine, ladha zinatofautiana.
- Inawezekana kabisa walioko kwenye mifumo wanajua shida iko wapi, ila tatizo lao kubwa ni ubinafsi na kutojali watu wao - UBINAFSI NI TABIA MOJAWAPO SUGU YA MWAFRICA, NI SAWA NA UCHAWI TU.
- Bei ya mafuta inapanda walio wengi wanateseka na wewe unapata hela unakuwa tajiri na kwenda kuweka hela Ulaya kwa Wazungu (huu ni upumbavu acheni ufala), Unapata hela unakuwa Tajiriii mkubwaa HALAFU UNAKUFA na mitoto yako yote inabaki mifala tu maana mali zako uliua na kutesa wengi hauna tofauti na mchawi au jambazi anayeua bila sababu
- Viongozi acheni ubinafsi na kusaidia watu wenu dhidi ya hili janga, sikweli kwamba hamjui cha kufanya kusaidia wananchi, mkiondoa kodi zote za kijinga na Serikali kupunguza matumizi tayari mtakuwa mmetatua tatizo na wananchi watakuwa huru.
- Rais, WIZARA YA NISHATI IWE NA MAWAZIRI WAWILI, MMOJA NI MAFUTA NA GAS, MWINGINE UMEME NA VYANZO VYAKE, Huyu wa mafuta na gas kazi yake iwe uchimbaji na utafutaji wa mafuta na gas na vyanzo vyake, udhibiti wa bei za mafuta na gas. Huyu wa umeme abakie na uzalishaji wa umeme, udhibiti wa bei za umeme na usambazaji wa umeme ndani na nje ya nchi.
- Rais, WIZARA YA FEDHA WEKA JICHO KALI NA IWEKEE MANAIBU WAWILI NA MAKATIBU WATATU WABOBEZI, HAKIKISHA HII WIZARA HAINA WANASIASA KABISA KUANZIA WAZIRI NA WATENDAJI WAKE, TEUA WATU PROFESSIONALS KUWA WABUNGE WAPE ILE WIZARA ACHANA NA HAWA BLAH BLAH POLITICIANS.
- Hivi serikali ikiamua kufanya seminar zake online, mikutano online, trainings online, kusiwe na posho, safari za ndani na nje zipungie, ikabana wizi, misafara ikapunguzwa, per diem zikatolewa, posho za wabunge zikatolewa, matumizi ya magari yenye kubwa yakatolewa - Baada ya HAYA KODI ZOTE KWENYE MAFUTA ZIKATOLEWA MWANANCHI SIATAKUWA AMEPONA HAPA.
- Nyie Viongozi wengi wenu mnaonekana MISIKITINI NA MAKANISANI eti mkifanya ibada na familia zenu huku mamilioni ya mnaowaoongoza ni masikini ambao mmewaletea nyie umasikini eti muwe na maisha mazuri ambayo mngeyapata tu bila kufanya wenzenu watumwa.
- Wazungu, Wachina, Wahindi, Waarabu wameshajua MIAFRICA NI MIFALA na iko tayari kutesa wenzao ili iishi vizuri kwa kuchukua rushwa, hapa sasa ndugu zetu mnabezwa sana kwa namna wanavyowapa rushwa ili kutesa ngozi nyeusi wenzenu kwenye ardhi yenu, HAPA MNACHEKWA NA NYIE MNAITWA NYANI TU.
- WEUPE (Wazungu, Waarabu, Wachina na Wahindi) wanafanya umafia ugenini kwa watu wengine na kuhakikisha faida na utajiri unakwenda makwao kunufaisha ndugu zao.
MWAFRICA anadhuumu WAAFRICA WENZIE NA KUWAPELEKEA UTAJIRI WEUPE na kuacha maisha duni kwao TENA MWAFRICA HUYU AMESOMA MPAKA DEGREE, MASTERS NA PHD KABISA - ukiwa na tabia hizi huna tofauti na mawakala wa utumwa enzi zile waliosaidiana na wakoloni kukamata mababu zetu na kuwapeleka utumwani kwa malipo ya shanga na nguo - SAIDIENI NDUGU ZENU WEUSI WANAOTESEKA NA UMASIKINI.
- UMAFIA UNAFANYWA KUSAIDIA WATU WENU MNAOWAONGOZA SIO KUWAANGAMIZA KUVIMBISHA MATUMBO NA KUNUFAISHA WAGENI aka FOREIGNERS - muwaige mabeberu.
- Tuache siasa, tumieni akili kutatua matatizo, kama hizo akili hamna kuweni huru ili Watanzania wote tushirikishwe kuisaidia hii nchi.