SoC01 Suluhu ya kutumia takangumu kama mbolea asilia

SoC01 Suluhu ya kutumia takangumu kama mbolea asilia

Stories of Change - 2021 Competition

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tatizo la takangumu ni kubwa na lenye changamoto nyingi katika miji yetu... Manispaa nyingi hujaribu kwa kila namna kupambana na hili tatizo lakini juhudi bado hazijakidhi ukubwa wa tatizo.. Zipo kampuni zinazolipwa mamilioni kila mwezi kwa ajili ya kukusanya taka toka majumbani, kwenye masoko , sehemu za kutoa huduma mbali mbali, viwandani na hata maeneo ya biashara.

Kampuni hizi zikishakusanya hizi taka huzipeleka maeneo maalum ya kuhifadhia taka na huko huchomwa moto ambao nao huzua tatizo lingine la uchafuzi wa mazingira na madhara mengine ya kiafya kuazia kwenye ngozi, mfumo wa upumuaji na hata macho, kwakuwa taka hizi hubeba kila aina ya uchafu na mabaki na hazichambuliwi na kutengwa kulingana na makundi yake.

Natambua wazi kuna taka laini na taka hatarishi lakini hizi tatizo lake si kubwa kwakuwa zimewekewa utaratibu unaofanya kazi vizuri.

Kwenye taka laini kwa muktadha huu vinyesi, mikojo na maji machafu kuna madimbwi maalum ya kwenda kumwaga huko na kuna magari maalum kwa shughuli hiyo.. Na kuhusu taka hatarishi hasa zinatokoka kwenye mahospitali, viwandani, na kwenye maabara mbalimbali hizi nazo hukusanywa na magari maalum na kwenda kuchomwa kwenye matanuru maalum yajulikanayo kama incinerators..!

Sasa je unatambua ya kwamba unaweza kusaidia kutatua uchafuzi wa mazingira na hewa kwa kuzigeuza taka ngumu kuwa mbolea asilia, huku ukiongeza vipato kwa watu na kutoa ajira?

  • Ajira kwenye ukusanyaji
  • Ajira kwenye uchakataji
  • Ajira kwenye usambazaji
  • Ajira kwenye uuzaji na ununuzi
  • Ajira kwenye matangazo
  • Ajira kwenye vifungashio
  • Ajira kwa wenye vyombo vya usafiri
  • Ajira kwa wenye maghala
  • Ajira kwa wauza chakula na vinywaji
Nknk

Kama taifa tunaweza kuokoa mamilion ya fedha za kigeni na kuokoa uharibifu wa mazingira na kutunza ardhi yetu kama tukiamua kupitia mashirika, vikundi vya wajasiriamali na hata mtu mmoja mmoja kuwekeza kwenye mradi wa kuchakata taka ngumu na kuzigeuza mbolea asilia

Kinachotakiwa kufanyika ni hiki.. Yale maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka ngumu ..yanaweza kugeuzwa na kuwekwa viwanda vya mbolea, malighafi ya chuma na malighafi ya plastiki nk.. Badala ya kuzichoma moto taka na kusababisha uchafuzi wa mazingira na athari za kiafya..!

Viwanda hivi vikoje?
Unakuwa na mtambo wa kutenganisha taka kutokana na asili yake
Zinapofika dample humwagwa kwenye kinu kikubwa...kinu hiki kinakuwa na sumaku na mikanda inayotembea ( rolling pillars)

Sumaku itanasa vitu vyote vyenye asili ya chuma na bati na kuvidondosha kwenye mkanda wake na hivi vitapelekwa moja kwa moja mpaka sehemu yake..huko vinaweza kuuzwa kama chuma chakavu ama vikachakatwa na kuuzwa kama malighafi ya kutengenezea nondo nk

Mkanda w pili utakuwa na sensor za kuhisi(detect) vitu vyote vyenye asili na plastic..hivi navyo vitaelekezwa kwenye mkanda wake mpaka kwenye hifadhi yake(depositer tank) hapo vinaweza kuyeyushwa na kuwa malighafi ya kutengeneza vitu mbalimbali vya plastic

Mkanda wa tatu huu utakuwa mkanda mkuu ama mkanda jumuishi.. Huu utabeba takangumu zote zisizo na bati, chuma wala plastiki. Hizi zitasafirishwa mpaka kwenye hifadhi yake(deposit tank) na kufanyiwa mchakato wa kuzisaga ... Hapo unaweza kuongeza maji na kuziozesha kisha kuzikausha ama ukaziacha na kuzipaki tayari kwa matumizi ya kwenye mimea mbalimbali

Kwa namna hiyo taka ngumu zitakuwa malighafi hitajika tofauti na ilivyo sasa..huku mazingira yakitunzwa na kuokoa gharama kubwa za kuziteketeza na bado tukiokoa fedha za kigeni kwa kuacha kuagiza mbolea nje ya nchi, kuongeza wigo wa ajira na kutoa nafasi mpya za utafiti mpya kwenye nyanja za mbolea isiyo na sumu kwa faida ya kizazi kijacho.
 
Upvote 40
USAFI%20DAR.jpg
 
Takwimu za uzalishaji taka kwenye majiji..naomba nitoe mfano wa jiji la Dar pekee

Jiji la Dar es Salaam linakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani 4,600 za taka kwa siku. Kati ya hizo ni asilimia 45 hadi 50 tu zinazopokelewa katika dampo sawa na tani 1,200 – 2,000 ya taka zinazokisiwa kuzalishwa kwa siku ambapo taka zinazobaki huishia kwenye maeneo ya wazi, mitaro ya maji, barabara na makazi.

Hizi ni taka nyingi mno kwa siku na ni malighafi inayopotea bure huku ikiongeza gharama za kuzikusanya na kuzihifadhi tena... Lakini kupitia mradi huu Kutakuwaa faida nyingi miongoni mwa jamii kama; kuongeza thamani ya taka na kipato katika jamii, kupunguza malundo ya taka katika mitaa na maeneo ya jamii, kupunguza gharama za uendeshaji wa dampo, kupunguza gharama za udhibiti taka katika Manispaa na kuongeza uelewa wa jamii katika uchambuzi wa taka kuanzia ngazi ya kaya.
 
Hali ilivyo Dodoma
Jiji ya Dodoma inakisiwa kuzalisha tani 350 za taka ngumu kwa siku ambapo kata za nje ya mji uzalishaji tani 114 na Kata za mjini uzalisha ni tani 236. Aidha wastani wa tani 150 tu ndiyo zinaondoshwa mjini kwa siku sawa na asilimia 66%, hali hiyo imekuwa ikichangiwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya kukusanyia taka!
Hapa kama unavyoona Dodoma pia panafaa kabisa kuweka kiwanda
 
Uzi Murua,lakini je,huu uwekezaji unaweza fanywa na wawekezaji wadogowadogo kweli..
Nikimaanisha hata kwa level ya mtaa..badala ya eneo la dampo..?
 
Wazo murua kabisa. Mawazo au fikra pevu ni nguzo mojawapo ya mitaji muhimu sana (intellectual capital) katika mafanikio ya kimaisha. Tuko hivi tulivyo kulingana na tunavyofikiri, ajabu utajiri tunauita uchafu! Remember, waste is wealth. Don't cast or dump it!
 
Uzi Murua,lakini je,huu uwekezaji unaweza fanywa na wawekezaji wadogowadogo kweli..
Nikimaanisha hata kwa level ya mtaa..badala ya eneo la dampo..?

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Yeah hata kwa mashine ndogo inawezekana kabisa kiwango tu cha uzalishaji ndio kitapungua
 
Wazo murua kabisa. Mawazo au fikra pevu ni nguzo mojawapo ya mitaji muhimu sana (intellectual capital) katika mafanikio ya kimaisha. Tuko hivi tulivyo kulingana na tunavyofikiri, ajabu utajiri tunauita uchafu! Remember, waste is wealth. Don't cast or dump it!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Remember, waste is wealth. Don't cast or dump it![emoji1752][emoji1752][emoji1752][emoji1752][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Njia nyingine ya kuhamasisha ukusanyaji taka ni kwa kutoa ofa ya kununua kiroba kilichojaa taka kwa shilingi 500 hivi.. Hivyo basi badala ya mtu kulipa kutupa taka zake wewe ndio unamlipa
Na kurahisisha kutenganisha taka unawashauri wawe na viroba tofauti kwa taka tofauti.. Ukipata sehemu nzuri mtaani kwako huna haja hata ya kwenda dampo na kwa kufanya hivyo unaweza kuvutia hata mitaa mingine ilete taka zao
Kuna vijana wengi waokota chupa za maji mitaani, hii inaweza kuwa ajira nyingine kwao na chanzo kingine cha mapato
CC: Kavirondo
 
Gharama za mashine zikoje kwa mwekezaji mdogo..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Wazo murua kabisa. Mawazo au fikra pevu ni nguzo mojawapo ya mitaji muhimu sana (intellectual capital) katika mafanikio ya kimaisha. Tuko hivi tulivyo kulingana na tunavyofikiri, ajabu utajiri tunauita uchafu! Remember, waste is wealth. Don't cast or dump it!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Tuko hivi tulivyo kulingana na tunavyofikiri, ajabu utajiri tunauita uchafu! Remember, waste is wealth. Don't cast or dump it![emoji1752][emoji1752][emoji1752]
 
Kuna haya masalia ya tairi mbovu, mipira yake ya ndani soli za viatu, katambuga nk.. Malighafi kama hii inapopatikana dampo inaweza kutengwa na taka nyingine na ikauzwa separate kwenye viwanda vinavyohitaji hizo malighafi
IMG_20210821_150059_800.jpg
 
Tuendelee kujifunza

Hii teknoloji tayari wenzetu wanaifanyia kazi katika ukamilifu wake.. Nina hakika tukiamua kwa dhati ya moyo hatuwezi kushindwa
 
Uchomaji wa namba hii unateketeza malighafi nyingi bila kujua

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom