Suluhusho pekee la kupatikana amani duniani ni nchi zote kufata sheria za Kiislamu, uovu utakoma, upendo utaongezeka

Suluhusho pekee la kupatikana amani duniani ni nchi zote kufata sheria za Kiislamu, uovu utakoma, upendo utaongezeka

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Mimi ni muumini wa dini ya Ukristo lakini nasema kutoka sakafu ya moyo wangu kuwa sheria za Kiislamu ndiyo suluhisho pekee na lakudumu la kupatikana kwa amani ya kudumu duniani kote.

Matatizo makubwa tunayopitia duniani yanatokana na kudharau matumizi ya sheria za Kiislamu badala yake kutumia sheria za kibabeli. Huo ndiyo ukweli ulio sahihi.

Karibuni tujifunze
 
Hebu ainisha hizo Sheria za kiislam na za kibabeli ili tujifunze zaidi.
 
Sio Uislamu tu hata Ukristo usingekubali kuwa liberals mambo yote yangekaa sawa. Ukristo imara na Uislam imara ni jibu tosha.
 
Ingekuwa uislam ndo dini ya kuleta amani basi nchi za kiislamu leo hii ndo singekuwa mfano wa Amani. Lakini matokeo yake ndo nchi zinazoongoza kwa machafuko na mauaji na ukandamizaji wa haki duniani. Upande wa pili nchi za Kikristo ndo zimekuwa mfano mzuri wa Kuigwa duniani
 
Mbona zipo nchi zinazofuata hizo sheria lakini bado kuna conflicts za ndani kwa ndani baina ya raia na serikali mfano Iran. Unless labda kama dunia nzima iwe Sunni au Shia. Tofauti na hapo bado kutakuwa na mvutano baina ya nani yuko sawa katika Uislamu wenyewe. Kinachofanya msuguano huo usiwe mkubwa ni kwamba wote wana common enemy wa kupambana naye kwa sasa, akiondoka basi tofauti zao zitaleta ugomvi mkubwa.
 
Amka wewe utajikojolea, Labda useme wale wanetu wa Majini matano.

Nyie wengine wote ni wahuni, wezi, wagomvi, wabaguzi, na wanyanyasaji wa kijinsia.
 
Mbona zipo nchi zinazofuata hizo sheria lakini bado kuna conflicts za ndani kwa ndani baina ya raia na serikali mfano Iran. Unless labda kama dunia nzima iwe Sunni au Shia. Tofauti na hapo bado kutakuwa na mvutano baina ya nani yuko sawa katika Uislamu wenyewe. Kinachofanya msuguano huo usiwe mkubwa ni kwamba wote wana common enemy wa kupambana naye kwa sasa, akiondoka basi tofauti zao zitaleta ugomvi mkubwa.
Nimesema sheria za Kiislamu Mkuu ambazo chanzo chake ni Mungu
 
Nimesema sheria za Kiislamu Mkuu ambazo chanzo chake ni Mungu
Sharia mkuu, kwani Iran si inaongozwa na Sharia? Lakini bado kuna migogoro ya ndani. Mbona waislamu wanahama penye sheria wanahaam nchi za scandianvia mpaka canada mkuu. Na pia nachosema hizo sheria labda ziambatane na kwamba dunia nzima watu ni masunni, au mashia otherwise utatokea mvutano.
Huo mvutano kwa sasa si mkubwa maana kuna common enemy.
 
Back
Top Bottom