Suma G wa vituko uswahilini

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,635
Reaction score
4,160
[emoji121]
WAKUU,

Kwa wajuzi wa Old Schooled Bongo Flava wanamtambua huyu JAMAA WA kuitwa SUMA G AKA MZEE WA VITUKO USWAHILINI, POMBE, TUNAJISALITI n.k.

Katika harakati zangu nimemwona jamaa mmoja anakaanga viazi mitaa ya Feri kafanana na Suma G karibia kila KITU.

Kwa kuwa sikuwa na nafasi ya kwenda kuongea naye kutokana na dharura yangu,
Nimebaki najiuliza -

Kweli SUMA G achome viazi Mtwara kweli?!?!

Kwa wenye info zake TUJUZANE WAKUU.
 
Watu bado hamuelewi tu kwamba hizo ajira zisizo rasmi ndizo zenye pesa nyingi kuliko zilizo rasmi?
Hebu chukulia ananunua gunia la viazi kwa elfu 35 na mafuta ya elfu 20 anakaanga na kuuza hadi jioni anamaliza gunia lote anajikuta Ana Laki moja na nusu au na ishirini hivi (150/120) ukija kutoa hapo unakuta anabakia na zaidi ya elfu 50 mfukoni mwake.
Chukua hiyo pesa izidishe Mara 30(mwezi) utachokipata Njoo hapa tuambie ni mfanyakazi wa level gani analipwa pesa hiyo kama mshahara wa mwezi, utagundua kumbe maofisini tunapotezeana Muda tu.
 
Suma G nimeishi nae sana kitaa Karakata miaka ya 1997-2006

Jamaa ni choka kuliko maelezo,namjua vizuri sana na yeye ananijua vizuri sana.Soggy dog alikuwa anambeba mpaka chumba cha kulala.

Maisha hayana formula,ukimuona mwambie Criss anamsalimia.
 
Hivi nani hua anawafundisha hesabu za kijinga namna hii, kama ni rahisi hivi na wewe nenda ukawe mkaanga viazi basi
 
Hivi nani hua anawafundisha hesabu za kijinga namna hii, kama ni rahisi hivi na wewe nenda ukawe mkaanga viazi basi
Kikubwa ni kuheshimu na kuilinda pesa yako la sivyo hutaiona hata kama unapokea mamilioni ya pesa kwa mwezi...hapo kazini kwako Kuna mtu unapokea nae mshahara unaolingana lakini ukiangalia level za maisha yenu hazifanani kabisa.
Amini usiamini hao unaowaona hawana mabarabarani wanakipato kikubwa kuliko mkaaji ofisini na kutumwa kila kitu.
 
Hivi nani hua anawafundisha hesabu za kijinga namna hii, kama ni rahisi hivi na wewe nenda ukawe mkaanga viazi basi
Ujui kila kitu kina frame take na mfano accordingily..sasa apo.unajiongeza kwa kuboresha idea Tatizo liko wapi
 
Hivi nani hua anawafundisha hesabu za kijinga namna hii, kama ni rahisi hivi na wewe nenda ukawe mkaanga viazi basi
Naona hajazungumzia kodi ya anapouzia..gharama za nishati atakayotumia,kumlipa msaidizi,na Mara nyingi inategemea na eneo..wazo sio baya lakini sio rahisi kama anavyodhani.
 
Suma Genius, mzee wa hot pot family. Mwamba yuko active Instagram unaweza mfata DM atakujibu peaceful
 
Suma G nimeishi nae sana kitaa Karakata miaka ya 1997-2006

Jamaa ni choka kuliko maelezo,namjua vizuri sana na yeye ananijua vizuri sana.Soggy dog alikuwa anambeba mpaka chumba cha kulala.

Maisha hayana formula,ukimuona mwambie Criss anamsalimia.
Sio Deadbody anamsalimia?
 
Kawaida tu kwani nayo ni bizness,haushangai bakhresa anauza maandazi na chapati?
 
Hadi humu kuna watu wenye hesabu za "karatasi na pen? " aisee unahasara ww na wanaokutegemea
 
Hadi humu kuna watu wenye hesabu za "karatasi na pen? " aisee unahasara ww na wanaokutegemea
We ulijua wote tunamajumba ya kifahari, tumezaliwa Familia bora, tumesoma sana na tuna kazi nzuri?
Situmii karatasi wala pen mi nilikimbia umande hata kusoma na kuandika sijui lakini wanaonitegemea wanaenda chooni, hawavai nguo zenye viraka, Wana sehemu ya kuita nyumbani kwa hesabu zangu za kichwani tu zisizo la darasa hata moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…