DOKEZO Responded SUMA geti la UDOM wanakamata vyombo vya usafiri na kuvitoza pesa. Je, zinaenda wapi?

DOKEZO Responded SUMA geti la UDOM wanakamata vyombo vya usafiri na kuvitoza pesa. Je, zinaenda wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumezuka tabia mpya geti la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kuna baadhi la Jeshi la Polisi wakishirikiana na SUMA wanasimamisha pikipiki kwa kigezo cha kuwakagua na kisha wanachukua pesa kwao mara nyingine 10,000/=, 5000/=, 20,000/= kitendo ambacho sidhani kama ni kwa mujibu wa sheria na pia hamna cha control number labda tuseme ni faini ya makosa.

Target yao sana sana ni pikipiki na mara nyingine Bajaj.

Sasa askari kwa SUMA anakuuliza leseni ya udereva iko wapi kwani hiyo ni kazi yake? Haya yote si yanapaswa kufanywa na road trafiki, na je hizo pesa wanazochukua kwa kigezo cha makosa kama mtu hajavaa helmet, hana viatu, hana bima, hajalipia LATRA zinakwenda wapi si ndio rushwa hiyo na upigaji?

IMG_6515.jpeg

Ufafanuzi wa Chuo ~ UDOM: Madai ya Walinzi wa geti la kuingia chuo kuchukua fedha kwa Bajaj na Bodaboda yanafanyiwa uchunguzi
 
Back
Top Bottom