Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Sumaye: Kinana anapiga dili za meno ya Tembo

Ocampo four

JF Senior Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
5,789
Reaction score
2,159
Jana kwa mara nyingine waziri Mkuu mstafu Ndg. F. Sumaye alimlipua katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi A. Kinana na kusema katibu mkuu huyo kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na uuzaji wa meno ya tembo (pembe za ndovu)... "Soma gazeti hapa chini"

Ilimbukwe kuwa mwaka jana kituo cha utangazaji cha Aljazeera kilitoa data kuhusu tembo wa Tanzania kuuwawa na kuonyesha kwamba mwaka 2007 kulikuwa na jumla ya tembo 146,879 na mpaka mwaka jana 2014 tembo hao wameuwawa kwa asilimia 64% na kubaki tembo 56,000 tu...

Mytake: Hili suala la Kinana tulifikiri ni uzushi ila ukiona waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa miaka 10 kaliweka wazi mbele ya wananchi ni wazi hakuna ubishi tena katika hilo....
1441954402518.jpg
 
Mkuu ni CCM ndio wanaotumalizia tembo wetu...kinana ni mmoja wao tu
 
Sumaye we sumaye why sasa umekosa ya kusema,ulipokuwa waziri mkuu si ndo ungemkabili?kwa sasa ni sawa na majungu tu pole
 
Nchi hii bana, aliyajua lini hayo?

Mzee Lowassa anasema"Go to court or shut up and keep quiet. "

Wameishi kwa raha ujana wao sasa wanataka wavuruge nchi
 
Wakuu kuuliza si Ujinga hivi hizo ni Pembe au Meno ya Ndovu?
Pili hua yanafanyia kazi gani au ni Malighafi ya kutengenezea bidhaa gani?
 
Sasa huyu sumaye kama kapagawa mwanzo aliona utani but sasa hivi ashajua ukawa kushinda uchaguzi ni shida so anaomba yatokee hata machafuko na yeye angemshughulikia alivokua Waziri Mkuu kama si unafiki ni nini na sura yake tu na macho unajua ni mtu wa aina gani.
 
Wewe weit uchaguzi uiashe atafilisiwa kila kitu na najua analijua hilo ndo mana kama kapagawa
 
Ukawa wanatumia mbinu za kisayansi kuendesha kampeni.
sumaye analipua mabomu na kwa akili za kawaida mtu kama sumaye wananchi wa kawaida watamuamini anayosema maana alikuwa waziri mkuu anajua kila kitu tofauti na slaa kama angezungumza wengi wasingeamini maana hakuwahi kuongoza serikalini.
lowassa anashambulia kwa sera ya kuleta mabadiliko ya maendeleo.
sehemu yoyote kwenye mkusanyiko wa watu ukikusanya maoni utakuta lowasa anakubalika kwa wastani mkubwa kupita jpm.
 
Back
Top Bottom