Sumbawanga: Mfanyabiashara azikwa akiwa hai

Jinga kweli wewe,Bagamoyo ,Tanga wanakofutanuchawi ni Burundi? Huwa unatunza rekodi? Umewahi isikia Rukwa kwenye Mikoa inayoongiza Kwa matukio ya mauaji?
Acha ubishi basi huko mbeya tena kuna katekista kazikwa akiwa hai damn.......
Ukatili wa bara huu utaisha lini??? Mimi wa bara lakini najiuliza tu.
 
Ndio maana adhabu ya kunyonga ikawekwa na sheria yake haijafutwa hadi leo...

Yaani 1.8mil ndio ya kuua mtu kweli!!
 
Laiti ningekuw Rais kuna Kesi aisee wakihukumiwaa Kunyongwaa ni faster nasainii wakale kitanzii...!! Watu kama hawa ni kunyongaaaaa hadharani tena.
 
Sumbawanga. Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumpiga na kumpora fedha zaidi ya Sh 1.8 milioni kisha kumzika akiwa hai mfanyabiashara wa mazao, Baraka Nyangala (30) na kumsababishia umauti.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP), Shadrack Masija alisema tukio hilo lilitokea juzi kijiji cha Katazi wilayani Kalambo, ambako walikwenda kununua maharagwe wakiwa wote wanne; watuhumiwa na mfanyabiashara huyo.

Alisema mfanyabiashara huyo mkazi wa mtaa wa Kasisiwe Manispaa ya Sumbawanga akiwa na wenzake hao waliotambulika kwa majina kama Frank Simsokwe (33), Edfonsi Simsokwe (28) na Nikas Lunguya (38) wakitumia usafiri wa pikipiki, walipofika maeneo ya porini walimtaka asimamishe pikipiki yake.

Kamanda huyo alisema baada ya kusimamisha pikipiki hiyo mmoja kati ya watu hao alimpiga kwa rungu kichwani kisha kumpora fedha taslimu Sh1.84 pamoja na pikipiki.

Alisema baada ya kumjeruhi na rungu kichwani, waliamua kuchimba shimo porini kisha kumfukia mfanyabiashara huyo akiwa bado yupo hai na wao kutokomea kusikojulikana.

Alisema baada ya kutoweka ghafla kwa mfanyabiashara huyo, ndugu wa marehemu walitoa taarifa Polisi ambao kwa kutumia intelijensia na wataalamu wa uhalifu wa kimtandao, walifanikiwa kuwakamata watu hao.

ACP Masija alisema watuhumiwa hao waliwaongoza hadi eneo ambalo waliufukia mwili wa marehemu ambapo ulifukuliwa kwa uchunguzi na taratibu nyingine za kuukabidhi mwili huyo kwa ndugu zao kwa ajili ya maziko.

Alisema watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na Polisi na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
Wapumbavu hao, watavuna uovu wao
 
Kuna mambo wakati hufanywa na binadam akili sijui huwa imehama kichwani inaenda wapi? Baada ya tukio ndipo hurejea na majuto huchukua nafasi

Hivi kweli 1.8mil mtu 3 bado mnabaki hapo hata akili ya kusema ukimbie haipo na sijui unawaamini vp mliofanya nao tukio la kinyama kama hilo?
 
Tujitahid kuwapiga vita maadui wakubwa wa taifa 🇹🇿 LETU ambao ni UJINGA, UMASKINI NA MARADHI...

Unaua mtu Kwa 1.8 bila kufikiria impact zake...basi ni bora wange timiza azma Yao bila kuacha any doubt 🤨 but it's not allowed.......

UMASKINI, UJINGA NA MARADHI ndio maadui wetu wakuu na Kila mmoja wetu Kwa nafasi yake tujitahid kuwapiga vita
 
Sumbawanga. Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumpiga na kumpora fedha zaidi ya Sh 1.8 milioni kisha kumzika akiwa hai mfanyabiashara wa mazao, Baraka Nyangala (30) na kumsababishia umauti.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP), Shadrack Masija alisema tukio hilo lilitokea juzi kijiji cha Katazi wilayani Kalambo, ambako walikwenda kununua maharagwe wakiwa wote wanne; watuhumiwa na mfanyabiashara huyo.

Alisema mfanyabiashara huyo mkazi wa mtaa wa Kasisiwe Manispaa ya Sumbawanga akiwa na wenzake hao waliotambulika kwa majina kama Frank Simsokwe (33), Edfonsi Simsokwe (28) na Nikas Lunguya (38) wakitumia usafiri wa pikipiki, walipofika maeneo ya porini walimtaka asimamishe pikipiki yake.

Kamanda huyo alisema baada ya kusimamisha pikipiki hiyo mmoja kati ya watu hao alimpiga kwa rungu kichwani kisha kumpora fedha taslimu Sh1.84 pamoja na pikipiki.

Alisema baada ya kumjeruhi na rungu kichwani, waliamua kuchimba shimo porini kisha kumfukia mfanyabiashara huyo akiwa bado yupo hai na wao kutokomea kusikojulikana.

Alisema baada ya kutoweka ghafla kwa mfanyabiashara huyo, ndugu wa marehemu walitoa taarifa Polisi ambao kwa kutumia intelijensia na wataalamu wa uhalifu wa kimtandao, walifanikiwa kuwakamata watu hao.

ACP Masija alisema watuhumiwa hao waliwaongoza hadi eneo ambalo waliufukia mwili wa marehemu ambapo ulifukuliwa kwa uchunguzi na taratibu nyingine za kuukabidhi mwili huyo kwa ndugu zao kwa ajili ya maziko.

Alisema watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na Polisi na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
Moyo wa mtu ni kiza kinene na daima kikulacho ki nguoni mwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom