The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
!!
Maisha yangu au yako ni funzo kwa watu wengine. Katika umri huu mdogo nilionao, leo nakuletea baadhi ya sumu ambazo nimeshuhudia zikiua ndoto, maisha na mafanikio ya watu wengi sanaa!
1. Sumu ya marafiki wabaya.
Marafiki wabaya hukuingiza kwenye kutenda mambo mabaya yanayoweza kukupeleka shimoni. Wakati wote, ambatana na watu ambao wanaendana na kiwango cha ndoto zako pamoja na imani yako. Badala ya kuachana na ndoto zako, achana na marafiki ambao wanakukatisha tamaa kwenye ndoto zako. Marafiki wabaya wameua ndoto za watu wengi sana!
2. Sumu ya starehe mbaya.
Starehe nzuri ni ile yenye kiwango kidogo sana cha Matokeo hasi. Ukiona starehe yako ina hasara nyingi sana kuliko faida, achana na starehe hiyo, ni sumu, itakuua!
3. Sumu ya mahusiano mabaya ya kimapenzi.
Mahusiano ya kimapenzi humletea mtu faida nyingi kuliko hasara. Ukiona uko kwenye mahusiano, badala ya kufaidika unapata hasara kiimani, kimwili, kifikra na kiuchumi basi mahusiano hayo HAYAKUFAI ni sumu kwako.
Mahusiano mazuri humfanya mtu kuwa bora kila siku na ajutie maisha ya usingle aliyokuwa akiishi hapo kabla kwa kuona kuwa amechelewa kuingia kwenye maisha ya ndoa au Mahusiano.
5. Sumu ya kiimani au kidini.
Dini iliyo njema humbadilisha mtu kutoka kwenye tabia mbaya na kuwa mwenye tabia njema. Tabia njema ni tabia ambayo hukubalika katika jamii na haina viashiria vya kuumiza wengine kimwili na kihisia.
Mwizi, Malaya, Muuaji na Muongo huyo hana tabia njema kwasababu huumiza wengine kimwili au kihisia.
Kwahiyo, Dini na imani iliyo njema huwafundisha watu kuwa wenye tabia njema. Bahati mbaya sana, baadhi ya watu wamepokea Dini na imani vibaya ambazo zimegeuka sumu kwao na kwa wengine kwa kuwabadilisha tabia zao na kuwafanya wasiwe na tabia njema.
Baadhi ya dini huruhusu kuua wengine na kulipiza visasi jambo ambalo husababisha kuumiza wengine kimwili au Kihisia na kupelekea kukatisha ndoto na malengo ya mtu huyo kwasababu anaweza kuuawa au kufungwa jela kwasababu Dini za namna hii ziko kinyume na Sheria za nchi.
5. Sumu ya mawazo hasi (Mawazo mabaya).
Kadri ambavyo umejaza kichwa chako mambo ambayo ni mabaya ndivyo ambavyo akili yako inaharibikiwa na kupoteza uwezo wa kufikiri kwa kina. Unaweza kupoteza uwezo wa kujiamini kwasababu ya hofu uliyonayo.
Sumu ya mawazo hasi(mabaya) ambapo mtu huwaza kushindwa kwenye mipango yake au maisha yake kwenda kinyume na matarajio yake. Mfano, mtu anaweza kuwaza nikipata magonjwa itakuaje, nikipata ajali itakuaje, nikifa itakuaje, watoto au mke na mume wangu akifa itakuaje?
Akiniacha na kuoa mwanamke mwingine itakuaje. Hali hii inasababisha kuingia kwenye hofu na msongo wa mawazo.
Hofu ya kupatwa na mabaya inasababisha kupoteza uthubutu kutimiza malengo yako,kutokuwa na furaha lakini pia inasababisha kupatwa na magonjwa kwasababu msongo wa mawazo hushusha kinga ya mwili,mtu anaweza kupatwa na presha na kadhalika. Sumu ya kufikiria kupatwa na mabaya imeua watu wengi sana kimwili na kifikra!
NAKUTAKIA SIKU NJEMA. LAKINI, NAOMBA UNIJIBU SWALI LIFUATALO. JE, MKE NA MUME KUVAA SARE NI MAPENZI AU USHAMBA?NITAKUWA WA MWISHO KUJIBU.
Mwalimu Hakika