Sanaa za uyu mzee wa Toronto za kitoto, akiwa tabora kama mkuu wa mkoa alienda hospital flani hivi ,kuna jambo pale hosp lilikua lilizushwa ,katika kikao cha ndani akawambia jamani sasa naenda kwa wandishi wa Habari nitakemea sana ,nalinda ugali watu vicheko na kweli nje alitema nyongo kama ni kweli.
Na hii imekua ni tabia ya waliowengi hasa wateule kwenye taasis mbalimbali kila mtu hupambana namna ya kumfurahisha alie juu, hizi media msiziamini , mtu akiita press tiyari nyuma mwongonzo ulisha kamilika ,ataongea nini na maswali gani anatakiwa uliza.
Mwaka mmoja namaliza pale udsm , kabla ya sherehe pale M/city tukaitwa kwanza leo kesho ni sherehe kwa nganzi tofauti kwa pamoja , yani msomi kisa tu yupo pala na kacheo anasema live
Jamani mnajua mgeni rasmi sio raisi tu maana si Amiri jeshi mkuu ila mnajua alisha kuwa rais wa nchi , jitahidini kuchangamka nami nautaka ugali wangu.
Sasa ukiwa na wanazuoni, watumishi katika taasisi za serikali wa namna hii what next , kama sio nchi kusinyaaa.
Kuna uhuni sana kwenye watu wa serikali hasa kwenye taasisi za umma , utasikia yule agusiki mtu wa mtu flani serikalini so wengine ni nyau ndani ya serikali ,mfano watumishi wa chini katika kila idara?
Majuzi dogo wangu alinipigia sim kwa masikitiko sana ni mtumishi idara flani so waliitwa kwenye kikao flani katika idara yao na mkuu wa idara akaja fungua kikao , ati anaanza salamu ati
Kazi na utu yale yale ya kiongozi Jw kwenye press alifanya, ujinga gani huu.
Hali ni mbaya sana ,pa kuanzia ni katiba mpya kurudisha mifumo kwenye reli na sheria mpya , hakatazwi mwananchi yoyote kuwa sehemu ya siasa ni haki yake lakini je mpaka makazini, maofisini , upumbavu huu ufe
Mbona hakuna mwajiriwa anaulizwa dini yake ,kabila lake wakati wa kuajiriwa? Na uzuri hata katika hafla mbali mbali salamu zote hutumika katika kusalimia . Hiweje katika vikao vya watumishi tumia salamu ya chama kimoja , basi zitumike salamu zote mfano
Kazi na utu
People's power
Chauma ........
Act wazalendo....
Tuache ujinga Taifa la wote hili