Super Thursday: Azam Fc vs Mbeya City Fc

Super Thursday: Azam Fc vs Mbeya City Fc

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Leo ndio leo asemaye kesho muongo. Leo ndio siku ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.Ni mechi ya kukata na shoka,ni mechi itakayoamua nani awe kileleni mwa msimamo au wote watabaki nafasi ya pili na ya tatu kama watatoka droo na Yanga wakashinda.

Timu zote mbili hazijafungwa mpaka leo hii wanaingia uwanjani kukamilisha mechi za mzunguko wa kwanza.wote wana pointi 26 on top of the table wakitofautiana uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.Yanga atakuwa anaomba mechi hii iishe kwa droo na yeye ashinde ili akae juu kwenye msimamo wa ligi.

Hii itakuwa mechi ya timu yenye vipaji,kiu ya mafanikio na support kubwa ya fans (Mbeya City) na timu isiyo na shida,wenye kiu ya ubingwa ( azam Fc). Mwisho wa siku aliyejipanga vizuri ataibuka na matoke mazuri.
Binafsi nawatikia ushindi Mbeya City Fc.
 
Natamani kuona hii game live toka pale Chamanzi kuisupport Mbeya City.
Msaada wenu wadau nitawezaje kufika huko nikitokea maeneo ya Posta kwani me mwenzenu mgeni kdogo wa hili jiji.!!
 
Mbeya City hawana uwezo wa kuwavimbia Azam, watapigwa kama wamesimama.
 
Game la kawaida tu, watu ndio wanaolipaisha!
 
Kwa hapa mbeya pamechangamka kama vile gem lipo sokoine kumbe chambazi, wanambeya wote wanazungumzia mbeya city,. Nawatakia ushind mbeya city,. Timu ya kwetu mbeya
 
Bahati mbaya kule Chamazi hakuna viroba ni full juisi sijui mtasingizia nini
 
Mimi ni Mbeya City mwili mzima, Azam wakae chonjo, vinginevyo wataogeshwa juice zao!
 
Japo siamini amini hivi,lakini hopeful Mbeya City watatuletea raha leo.
Mkuu najua mnaipenda timu yenu na mimi sina masilahi yoyote na timu yoyote kati ya hizo mbili, lakini Azam wako vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom