Supermarket maarufu iitwayo Game imefuata nyayo za makampuni mengine kwenye MALL za Dar hasa Mlimani city kufunga biashara zao na kuondoka nchini.
Kuna tetesi DSTV ambayo zipo Channel maarufu za supersports nayo ipo njiani kufunga biashara zake nchini kutokana na kushuka kwa mauzo ya vingamuzi vyake.
Super sport ambayo huonyesha ligi ya mpira wa miguu Ghali duniani yaani English Premier League yenye timu maarufu kama Manchester United, Arsenal, Liverpool, Chelsea, Man City n.k imeonyesha kushuka ununuzi wa vingamuzi kutokana na Watanzania wengi sana kuacha kuangalia ligi za ulaya hasa za Uingereza na kushabikia sana Simba na Yanga kupitia Azam TV.
Ripoti ya siri iliyotolewa na multichoice Tanzania imeonesha hasara kubwa kwani ule ushabiki wa timu za England, Champions League umepungua sana nchini ukilinganisha na nchi zingine jirani kama Kenya, Uganda n.k.
Kutokana na hali hiyo wameamua muda wowote kufunga biashara yao na kutuacha tukiangalia Simba, Yanga, Namungo, Biashara United, n.k.
Kama ni taarifa hizi zina ukweli basi watanzania tutakuwa tumerudi nyuma kimpira miaka 20. Mabilionea 3 tu ndio wanaosababisha hali hii. Azam TV haina ubavu wa kununua haki za mechi zote za ligi kuu ya Uingereza, Dola za kimarekani sio za Zimbabwe milioni 600 kwa mwaka.
Tunaomba DSTV WATOE TAMKO.