Supermarket maarufu "Game" iliyopo Mlimani City inatarajia kufunga biashara zake

Supermarket maarufu "Game" iliyopo Mlimani City inatarajia kufunga biashara zake

Supermarket maarufu iitwayo Game imefuata nyayo za makampuni mengine kwenye MALL za Dar hasa Mlimani city kufunga biashara zao na kuondoka nchini.

Kuna tetesi DSTV ambayo zipo Channel maarufu za supersports nayo ipo njiani kufunga biashara zake nchini kutokana na kushuka kwa mauzo ya vingamuzi vyake.

Super sport ambayo huonyesha ligi ya mpira wa miguu Ghali duniani yaani English Premier League yenye timu maarufu kama Manchester United,Arsenal,Liverpool,Chelsea,Man City n.k imeonyesha kushuka ununuzi wa vingamuzi kutokana na Watanzania wengi sana kuacha kuangalia ligi za ulaya hasa za Uingereza na kushabikia sana Simba na Yanga kupitia Azam TV.

Ripoti ya siri iliyotolewa na multichoice Tanzania imeonesha hasara kubwa kwani ule ushabiki wa timu za England,Champions League umepungua sana nchini ukilinganisha na nchi zingine jirani kama Kenya,Uganda n.k.

Kutokana na hali hiyo wameamua muda wowote kufunga biashara yao na kutuacha tukiangalia Simba,Yanga,Namungo,Biashara United,n.k.

Kama ni taarifa hizi zina ukweli basi watanzania tutakuwa tumerudi nyuma kimpira miaka 20.Mabilionea 3 tu ndio wanaosababisha hali hii.Azam TV haina ubavu wa kununua haki za mechi zote za ligi kuu ya Uingereza,Dola za kimarekani sio za Zimbabwe milioni 600 kwa mwaka.

Tunaomba DSTV WATOE TAMKO.
Watu hawana furaha mpira wa nini?

Watafunga sana tu.

Anyway si tuliambiwa wanaccm tanzania ndio wengi? Wameshindwa kununua hivyo ving'amuzi? maana wao maisha ni bwelele
 
Game ipi iliyofunga biashara zake Mlimani City...mbona hadi J'2 imekuwa wazi muda wote???
 
Serikali katili ya CCM ndio chanzo ya yote hayo. Kila mtu sasa ameamua kuwa mmachinga ili kusogeza siku.
Ni kweli hata startimes wameanza uchinga siku nyingi kupitia kingamuzi Chao Sasa hivi wanatuuzia vitu vitu vya nyumbani kwa njia ya simu ukipiga mzigo unakuja mlangoni kwako.
 
Serikali katili ya CCM ndio chanzo ya yote hayo. Kila mtu sasa ameamua kuwa mmachinga ili kusogeza siku.
Acha ujinga mnalaumu kitu msichokifahamu,nikuulize Game pia wanafunga supermarket zao mbili huko Kenya jee huko kuna CCM? pia nikuulize wewe umewahi kuwa mnunuzi wa bidhaa hapo Game? Game wanafunga maduka yao kutokana na utamaduni wa wakazi wengi wa nchi za Afrika Mashariki kutokuwa wanunuzi wakubwa kwenye maduka makubwa tofauti na nchi za Kusini mwa Afrika ambazo wao wana tabia za kufanya manunuzi kwenye maduka makubwa kama wazungu wafanyavyo, kumbuka nchi za kusini mwa afrika zimerithi utamaduni wa wazungu, ni sehemu ndogo ndio hutumia maduka ya kwa mangi sijui kwa mpemba .
 
Tatizo ni OLE. Kiwango cha uchezaji wa timu yake hakitofautiani na Namungo.
 
Pale mkuki nilikuwa nafanya kazi kwenye duka la nguo flow ya kwanza kama mwaka hv lkn boss akashindwa akahamia city mall mana pale hakuna wateja na watu wengi nadhani hawapajui
Ile ni location ya wenye kipato cha chini wanaokaa Gongo la Mboto, Chanika, Kitunda, Buza, Temeke, etc. Hao ndio majirani kwa hiyo sitegemei maajabu ya mauzo pale. Mtu iweje atoke Buza kwa Rulenge aje kutazama VR pale Mkuki wakati hana hela ya kununua miguu ya kuku. Location ya malls nyingine ziko ushuani
 
From Dik uchwara to Coca cola feki and Simbachawa anapiga mkwaru.
 
Kutokana na hali hiyo wameamua muda wowote kufunga biashara yao na kutuacha tukiangalia Simba,Yanga,Namungo,Biashara United,n.k.
🤣🤣 Hizi habari mnatolea blog gani?
Kwa hiyo wamekasirika na hivyo wameamua kutuacha tuangalie Namungo,Biashara n.k
 
Dstv wahuni tu waache waende zao huko yan kuna wakat walifkia 240,000 kwa mwezi
ili uweze kuangalia mpira wa ulaya na Epl
 
CHUMVI CHUMVI CHUMVI"

utakuja usutwe na wanawake wa Buza kwa Mpalange siku moja.
 
Cabinet ya Mkapa ndiyo ilifanyia kazi uchumi wa nchi hii haswa Marehemu Daudi Balali walicho mlipa Mungu anajua
 
Pale mkuki nilikuwa nafanya kazi kwenye duka la nguo flow ya kwanza kama mwaka hv lkn boss akashindwa akahamia city mall mana pale hakuna wateja na watu wengi nadhani hawapajui
@ezekiel mbaga

Pale nilikuwa napenda ile supermarket kulikuwa wanauza maua na vyombo vya ndani kwa bei chee sana ukilinganisha masuper mengine. Juzi kati nimerud ninunue maua narudishwa na mlinzi kwamba hakuna ofisi huko uendako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom