Supplier wangu Muhindi aliekuwa na deni la Bilioni 80 kalimaliza, Nimekaa na kutafakari hawa watu wapo serious na biashara, bado tuna safari ndefu

Boss jamaa alinikopesha 100,000/= Kwa makubaliano baada ya wiki mbili atanirudishia pesa yangu...ila ilimchukua mwezi mzima kunirejeshea, ambapo na penyewe alinirushia kwenye simu 65,000
Huko 100k mbn mbali sana kiongozi. Nilikopwa 20k ni mwaka wa 3 sasa, yule mtu kapiga kimya kama hakuna kilichotokea. namm wala sijajishughulisha nae. Juzikati kaanza kunitafuta nna hakika anataka kupiga kizinga kingine hlf apotee tena. wabongo kupiga hatua ngum sana tunadidimizana sana.
 
Banker hana nidhamu ya kazi.
Naskia Hawa bankers ukienda kufanya withdrawal hata ya 40m ukimpa mgongo tu, atachukua taarifa zako zote
Mpige chini kabisa huyo bwege na akili zake ndogo.. Kuna watu hata aibu hawanaga, mtu anakopa Hela kwako anajisahaulisha Kwa makusudi akiona haulizi chochote kuhusu deni, anakuja kukukopa Tena..... Hao ni parasites ambao hautakiwi kabisa kuwa nao kwenye circle yako.
 
Pengine taasisi ilijiridhisha kwa kina kabla kumkopesha kiasi hicho Cha fedhwaa so Kama biashara zake zimeenda poa it's obvious atalipia mikopo yake dhamana zake ziwe huru.... Na Kama Mambo yangeenda kombo wazee wa minada na ufilisi wangelihusika.
 

Umenikumbusha mbali sana enzi za boom kukata, halafu Bado kama wiki mbili hivi ndio litoke lingine... Huwa ni kipindi kigumu sana na Cha mateso, wadada wanaliwa sana, watu wanaweka bond TV Kwa Hela ndogo mno...!!

Kwa nilichokuja kubaini Mimi wabongo tunapenda sana kupokea Hela na hatupendi kabisa kutoa, yaani hata kama mtu unadaiwa unaona kutoa Hela hili umlipe mdeni wako ni kama unaitupa chooni hivi, yaani kutoa Hela mfukoni mwako roho inakuwa unakuuma sana na wakati ni wajibu wako kulipa deni.. Sasa na principles za Hela haziko hivyo, hautakiwi kuwa na roho ya hivyo.

Integrity ni kitu ambacho wabongo hawana kabisa na wamekaa ki-opportunistic tu.

Tamaa mbele, uaminifu hakuna na ndio maana hata baadhi ya makampuni huwezi kuwakuta wabongo kwenye positions muhimu... Utakuwakuta kwenye vibarua huko.

Hivi unajua hapa nchini Kuna benki ambazo hazikopeshi kabisa wabongo ngozi nyeusi? Na sababu ya kufanya hivyo ni hizi hizi tunazoongelea hapa, mfano kama bank of Baroda hakuna mswahili anayeruhusiwa kusogea pale ... Waswahili waende wakakopeshane kwenye vikoba huko.

Masuala ya kumkopesha mtu halafu inafika siku ya rejesho anakwambia mara ooh nimempeleka mtoto hospital Hela zote zimeishia huko, wao hawataki..

Kuna muda Huwa naamini huu umaskini WA waswahili ni stahiki Yao..
 
Hiyo ni case nyingine ya Ufisadi na Utapeli. Haihusiani na Biashara.
Huwa nashangaa sana watu wanavyomtaja taja Lugumi Tena Kwa mitano ya heshima utafikiri labda huyo Lugumi ni business genius wakati ni mtu ambaye utajiri wake ulitokana na kutake advantage ya utawala mbovu uliokuwa umejaa rushwa na ufisadi.
 
unadhani hadi bank iliamua kumkopesha hizo billion 80 unadhani alikuwa na assets za gharama gani..!
 
Umenena vyema Mr muhimbu......

Jamaa mpk leo two yrs kamute na kilo yangu kimya tunaishia ku view status hasa mm ndo namview maake mwaka unaweza kata sijapost chochote

Mmepanga deal sijui mchongo umetiki wote au kidg muelezee muhusika aliyekutonya ama mmefanya wote deals hiyo bhn kiasi ni hiki hata km umemdhulumu kivingn Kuna uaminifu atakupa......

Lkn mtu anakimbia mitini ukipiga ntakuchek badae huyo...... Inakuwa ndo zake

Watu wa hivyo ukikutana na wengine ndo kulogwa....... Kusomewa sijui nn kwa ujinga......

Nasema Tena kaka aliyenambia issue ya integrity mtu mzima km 70 ana kampuni zake anachonisisitiza nataka kwenye maisha utendaji uwe na integrity

Akaniambia Kuna vitu nilikosa kwa kitokuwa na integrity so sitaki na wewe upite hapo japo hakunishirikisha ni nn alifanya Ila ananisisitiza integrity iz all in your life.....

Tuko pamoja Mr 👊
 
Huyo jamaa yako hiyo Hela itamtesa sana kwenye nafsi yake maisha yake yote, maana kila akikumbuka alikufanyia dhuruma Tena wewe rafiki yake bila sababu, basi itakuwa inamuuma sana..!!

Integrity ni nguzo kuu ya kutengeneza network ya kukupa wewe mafanikio.

Wale raia wa Ethiopia ambao kila siku Huwa wanakamatwa nchini kwetu hapa kwenye maroli wakibebwa kama mizigo wakielekea South Africa..

...unaambiwa wanaendaga kule South hawana hata nguo za kubadilisha, wakifika kule wanakutana na WA Ethiopia wenzao ambao tayari wamesha make life, Kwa hiyo hao wenzao ambao tayari Wana maisha wanachofanya ni kuwakopesha mitaji ya biashara hao wenzao waliofika hawana kitu kabisa....

Baada ya mwaka Mmoja tu hao new comers wanakuwa tayari na wao wameshaji stabilize kibiashara na hatimae Sasa wanarejesha zile pesa walizokuwa wamekopeshwa na wenzao kama mitaji....! Kisha maisha yanaendelea.

Na ndio maana Ethiopians ndio diaspora yenye maendeleo zaidi kuliko waafrika wengine huko south Africa.

Sasa hebu chukua huu utaratibu WA kuwezeshana wa Ethiopians halafu uuletea Kwa mbongo uone kama hujaambulia maumivu na mkaishia kwenye uadui.
 
Mimi nshasahau kumdai Ila najua ana deni langu

Yeah wabongo tunashindwa kuwa waaminifu hasa mtu akikopa hela sijui kwann tunashindwa kurudisha hela ya mtu ?

Mimi sijawahi kopa nishindwe kumrudishia hata kwa kuchelewa ntaomba excuse nyingi lkn ntalipa sijawahi kimbia na deni la mtu!

Uaminifu mwingne mpeane michongo ikifanikiwa unaweza salitiwa kabisa kabisa kama hamkuwa wote!!

Ila tukijitahidi kuwa na uaminifu japo kidogo tutafika mbali

Mwingne akishajua basi una toa hela vizinga haviishii yaani wabongo changamoto san
 
Kujua Hilo tuu ni hatua kubwa sana keep up
 
Sisi wahindi ukoo mzima tunaishi nyumba moja. Hio pesa ni ndogo sana tukijichanga bukubuku mwezi tu inafika na hapo hatujawashirikisha wajomba mumbai na mashangazi wa Delhi
Ni kweli hawa jamaa wanapigana tafu sana, hawachekani mmoja wao akikwama. Bongo ndugu wanafurahia sana ndugu yao wa Damu akikwama kibiashara au hata kufilisika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…