Supu ya pweza inanimalizia hela nashindwa kuiacha

Selemani Sele

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2023
Posts
319
Reaction score
711
Za jioni wakuu, supu ya pweza ni maarufu sana Dar es salaam mida ya jioni ambapo tunaona watu wanauza supu kwenye vimeza vyao.

Sasa kitu kinachofanya nije leo ni ulevi wa supu ya pweza aisee nimejitahidi kuacha nimeshindwa yaani kila nikitoka kazini njia ya kwenda nyumbani kuna kibanda cha pweza kama wana dawa vile hawa watu unasema ninywe supu ya mia tatu ,mara unapiga kachori, paap kata mkia wa elfu mbili, weka na prawn puuh elfu tano imeenda.

Nikaamua nipige hesabu kila nikila pweza niandike kwenye google notes aiseee nimekuja kupiga hesabu mwezi december 2023 nimetumia elfu 65600 ukichezesha mwaka mzima kama laki 7 hv jamani si Tv mpya hiii.
Nifanyeje niache huu ulevi wa supu ya mdudu pweza.

Tushee experience walevi wenzangu
 
Badilisha njia unaporudi nyumbani
 
Kwa kuwa unatumia fedha zako kula, we jenga shavu.

Mimi nina addiction ya tambi mbichi. Natafuna kile kipakti kimoja cha Santa Lucia ndani ya siku mbili.
Lakini naenjoy.
 
kwani pesa kazi yake ni nini mdogo wangu.....mabula sai kafa kaziacha..م
 
Mpe hizi taarifa mkeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…