Sura za kurogea watu na kufanyia ushirikina

Sura za kurogea watu na kufanyia ushirikina

😂😂 We kama sio Shiaa Ni Uliritadi , kwaiyo una chuki isiyo na kifani Broo.. M nakushaur ukwel huwa unajulikana na uongo unajulikana

Huu muda unaupoteza kuandaa hivi vitu ungefocus na Life maisha magumu , Kama Dini ilikua tu inaanza na viongoz wa Macca wakat ule wakashindwa kui stop na ikaenea kwa nguvu we nd utaeza msukuma 😂😂 Wenzako walimuita mpaka mchawi na bado akapanua wigo we unaekuja jamii forum utaeza ndugu yangu 😂 woiii si hatuku stopishi we ni mwana tunakushaur tu pambna na maisha huu ni utoto unaleta
Mbona huna hoja Bali unabwabwaja tu
 
Mbona huna hoja Bali unabwabwaja tu
Sasa Hoja za nini we unataka kuwaambia watu ujwel ukwel au unataka hoja zetu sema moja 😂

Hoja unataka hoja gan... unaambiwa Quran haina Connection na uchawi we kazi kungangania oohh Quran sjui ukisoma sjui nn sa tunakuelweshaje we jamaa 😂😂 we umeamua we amua
 
Kuna mstari mwembamba sana kati ya uchawi na Quran

Ukitaka kuyaita hata majini kwa Quran na vitabu vya kiislamu yanakuja

Ndio maana waganga wengi wanatumia Quran kurogea
 
Iko hivi, dini ya uislamu ni salama sana na upo wazi sana , ILA KUNA MAMBO YANACHANGANYWA SANA NA WAISLAMU WENYEWE, NIkweli kuna waislamu wanachanganya dini na ushirikina , ila hayo wanayoyafanya ni kinyume na Uislamu wenyewe, huo ushirikina mnaouona kwa baadhi ya waislamu sio dini ni utashi wa mtu, na nichukizo kubwa kwa Allah,

1. Kuhusu Ruqyah na Qur’ān kutumika kwa “kuitana majini”
Qur’ān na Sunnah zinavyofafanua Ruqyah

Mtume ﷺ amesema:
"عرضت عليّ الرقى، فلا بأس بالرقى ما لم يكن فيها شرك"
“Ruqyah si vibaya mradi haina shirki.”
(Muslim 2200)
Ruqyah halali ni ile yenye:

1. Maneno ya Qur’ān au Du‘ā sahihi kutoka Sunnah.
2. Isiyo na maneno ya kishirikina au majina ya majini.
3. Imetolewa kwa nia ya kuomba shifaa kutoka kwa Allah pekee.

Hivyo: Kusoma Surah Al-Falaq, An-Nās, Ayatul Kursi, n.k., kwa nia ya kinga au tiba — si uchawi, bali ni ibada. Mtume ﷺ mwenyewe alizisoma aya hizo kwa kujikinga (Bukhari 5017, Muslim 2192).

Kuitana majini kupitia Qur’ān ni kosa na si sehemu ya Ruqyah ya Kishariah. Hii ni upotofu unaopingana na mafundisho ya Mtume ﷺ.
2. Kuhusu Surah Al-Jinn na madai kuwa Qur’ān ni “mlango wa mawasiliano na majini”
Qur’ān 72:1-2 inasema:

Aya hii inasimulia tukio la kihistoria kwamba majini waliposikia Qur’ān walivutiwa na kuamini — si kwamba Qur’ān imewekwa kama chombo cha kuwaalika majini.
Mtume ﷺ hakuwahi kuisoma Qur’ān ili awaitane majini, bali walikuja kwa amri ya Allah kusikiliza.
Kuitumia Qur’ān kama “mlango wa uchawi” ni matumizi mabaya na ni haramu.
3. Kuhusu “Albadir” na matumizi ya Qur’ān kuomba madhara
Qur’ān imekataza kutumia maneno yake kwa madhara:

Mtume ﷺ amesema: "من دعا على مسلم بغير حق كان كالباغي عليه"
(Anayemlaani Muislamu bila haki ni kama anayefanya dhulma kwake) (Muslim 2587).
Hivyo, kutumia aya au du‘ā kuomba balaa au jinni kwa adui ni haramu na ni aina ya sihiri/shirk.
4. Kuhusu “Kombe, nazi, maandiko ya Kiarabu”
Mtume ﷺ alipokataza hirizi:
"إن الرقى والتمائم والتولة شرك"
(Hakika ruqyah za kishirikina, hirizi, na uchawi wa mapenzi ni shirki) (Abu Dawud 3883, sahih).
Lakini Maulamaa wamesema: Kuandika Qur’ān na kuosha ili kunywa kama tiba inajuzu kwa masharti (Ibn al-Qayyim katika Zād al-Ma‘ād), mradi:
Hakuna maneno ya kishirikina.
Imetokana na Qur’ān au Du‘ā sahihi.
Nia ni tiba kwa idhini ya Allah, si nguvu za maneno yenyewe.
Kutumia maandiko ya ajabu, majina ya majini, n.k., ni uchawi na ni haramu.
5. Kuhusu “vitabu vya uchawi vya Kiislamu” kama Shams al-Ma‘arif
Vitabu kama Shams al-Ma‘ārif vinafundisha uchawi na vimekatazwa wazi na wanazuoni wa Ahlus-Sunnah.
Hakuna ushahidi wa Mtume ﷺ kufundisha uchawi au kutumia “magic squares”.
Muislamu anatakiwa kujiepusha navyo kwa mujibu wa Qur’ān 2:102 na hadith: "اجتنبوا السبع الموبقات"… وذكر منها: السحر
(Jiepusheni na madhambi saba maangamizi… miongoni mwake ni uchawi) (Bukhari 2766, Muslim 89).

6. Miwisho

Ruqyah ya Kishariah = Aya za Qur’ān + Du‘ā sahihi + Nia ya kumuomba Allah → Halali.

Uchawi kwa jina la Qur’ān = Kuchanganya majina ya majini, hirizi, talismans → Haramu, ni shirki.(ushirikina na haufai)

Qur’ān haijaletwa kuitana na majini → Imekuja kwa ajili ya uongofu wa binadamu na majini.
Muislamu akitaka kinga: Ajikinge kwa dhikri, kusoma Al-Falaq, An-Nās, Ayatul Kursi, na kufuata Sunnah, si kwa mbinu za kishirikina.

Naamini utakuwa umenielewa zaidi
Upo kutetea ushirikina na dini?

Maana unaongea vitu ambavyo kana kwamba watu hawajionei

Unadhani kwann Quran na vitabu vyenu vinatumika kuita na kufuga majini ?

Kwanini waganga na waaguzi wanatumia Quran?
 
sipo kutetea ushirikina wala dini kwa upofu. Lengo langu ni kuweka msimamo wa Uislamu sahihi kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah, si kwa mazoea ya wachawi au waganga wanaotumia dini kama kinga ya kuficha uchawi wao.

Sasa ngoja nijibu hoja zako moja kwa moja kwa dalili,

SWALI LAKO: “Kwa nini waganga na waaguzi wanatumia Qur’an?”

JIBU:

Kama mlaghai au tapeli anavaa kanzu au ananukuu Qur’an, haimaanishi Uislamu unafundisha alichokifanya. Uislamu unakemea vikali kutumia Qur’an kwa uchawi au kumuita jinni.
Qur’an inasema:

"Na hakika majini walijua kuwa, hakika waliofanya hivyo (uchawi) hawatapata wokovu."
(Qur’an 72:5)
"Na hakika walimfundisha watu uchawi...na wala hawakumfundisha yeyote kabla ya kumwambia: Sisi ni majaribio, basi usikufuru."
(Qur’an 2:102)

SWALI KWAKO

Kama Qur’an ni chombo cha uchawi, mbona mwenye Qur’an sahihi hawezi kulogwa?
Mtume ﷺ alisema:
"Msomaji wa Ayatul Kursiy kila usiku analindwa na Malaika, na Shetani hawezi kumkaribia."
(Bukhari 2311)
Ikiwa Qur’an inaitwa kwa ajili ya sihiri au uchawi mbona Shetani anakimbia Qur’an?

SWALI LAKO LINGINE: “Kwa nini Quran inatumika kufuga majini?”

JIBU LAKO NI:

Qur’an haitumiki kufuga majini, bali wachawi ndio wanaipotosha na kuandika aya kwa muktadha wa kishirikina. Ni sawa na kuchukua dawa ya hospitali na kuitumia kama sumu — kosa si dawa, kosa ni mlaghai. ( Hapo nafikiri umenielewa vema,

MFANO WA MTUME SULAYMAN:

“Na hawakufundisha mtu yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni jaribio, basi usikufuru.”
(Qur’an 2:102)
Wachawi walipindua maarifa ya Sulayman kwa kutumia majina ya majini. Lakini Qur’an inasema:

“Na Sulayman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru.”
(Qur’an 2:102)
SWALI LA TATU KWAKO

Kwa nini Qur’an inawaita wachawi “makafiri” kama kweli Qur’an inatumika kufuga majini kwa halali? Au hili ulikuwa hulijui hili

HOJA YAKO NYINGINE UMESEMA “Maneno ya Qur’an yana nguvu za kishirikina”

JIBU:

Qur’an haina nguvu za kishirikina. Nguvu za Qur’an ni mafundisho ya Haki na maneno ya Mwenyezi Mungu, si hirizi au talismans. Kuitumia Qur’an kama hirizi ya “magic square” ni kutumia maandiko matakatifu kwa njia ya kishetani.

Mtume ﷺ alisema:
"Hakika hirizi, ruqya na tamaa (za kishirikina) ni shirk."
(Abu Dawud 3883)

MASWALI MENGINE KWAKO:
1. Mbona Qur’an inasema jinni wanamuogopa mtu mwenye imani na kumtaja Allah (Surah Al-Jinn 72:1-6)?
Unadhani mtu anayesoma Qur’an kwa ikhlasi anaweza kuitumia kuita majini?
2. Kama Yesu hakuandika hirizi, je, Paulo na makanisa leo yanayoandika “mafuta ya upako” na “maji ya wokovu” si ushirikina wa jina la Yesu?
3. Kama unadai Qur’an ni uchawi, kwanini wachawi wanaiandika kwa kubadilisha maana? Hiyo haithibitishi kuwa Qur’an ni Nuru na wao ni watu wa giza?
4. Kama Qur’an ni uchawi, kwanini watu wanapoisoma kwa ikhlasi wanatulia, wanapona, wanabadilika kitabia? Je, uchawi huleta ucha Mungu?

UNAPASWA KUELEWA KUWA

Qur’an ni Kitabu cha Nuru, lakini kama kitu chema kitatumiwa na mtu mbaya kwa nia chafu — kosa si Qur’an, kosa ni mtu.
Wachawi wanaoitumia Qur’an kwa kuandika majina ya majini, talasim, na hirizi — si wafuasi wa Qur’an, ni Wapingaji wa quraani
 
sipo kutetea ushirikina wala dini kwa upofu. Lengo langu ni kuweka msimamo wa Uislamu sahihi kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah, si kwa mazoea ya wachawi au waganga wanaotumia dini kama kinga ya kuficha uchawi wao.

Sasa ngoja nijibu hoja zako moja kwa moja kwa dalili,

SWALI LAKO: “Kwa nini waganga na waaguzi wanatumia Qur’an?”

JIBU:

Kama mlaghai au tapeli anavaa kanzu au ananukuu Qur’an, haimaanishi Uislamu unafundisha alichokifanya. Uislamu unakemea vikali kutumia Qur’an kwa uchawi au kumuita jinni.
Qur’an inasema:

(Qur’an 72:5)

(Qur’an 2:102)

SWALI KWAKO

Kama Qur’an ni chombo cha uchawi, mbona mwenye Qur’an sahihi hawezi kulogwa?

"Msomaji wa Ayatul Kursiy kila usiku analindwa na Malaika, na Shetani hawezi kumkaribia."
(Bukhari 2311)
Ikiwa Qur’an inaitwa kwa ajili ya sihiri au uchawi mbona Shetani anakimbia Qur’an?

SWALI LAKO LINGINE: “Kwa nini Quran inatumika kufuga majini?”

JIBU LAKO NI:

Qur’an haitumiki kufuga majini, bali wachawi ndio wanaipotosha na kuandika aya kwa muktadha wa kishirikina. Ni sawa na kuchukua dawa ya hospitali na kuitumia kama sumu — kosa si dawa, kosa ni mlaghai. ( Hapo nafikiri umenielewa vema,

MFANO WA MTUME SULAYMAN:

(Qur’an 2:102)
Wachawi walipindua maarifa ya Sulayman kwa kutumia majina ya majini. Lakini Qur’an inasema:

(Qur’an 2:102)
SWALI LA TATU KWAKO

Kwa nini Qur’an inawaita wachawi “makafiri” kama kweli Qur’an inatumika kufuga majini kwa halali? Au hili ulikuwa hulijui hili

HOJA YAKO NYINGINE UMESEMA “Maneno ya Qur’an yana nguvu za kishirikina”

JIBU:

Qur’an haina nguvu za kishirikina. Nguvu za Qur’an ni mafundisho ya Haki na maneno ya Mwenyezi Mungu, si hirizi au talismans. Kuitumia Qur’an kama hirizi ya “magic square” ni kutumia maandiko matakatifu kwa njia ya kishetani.

"Hakika hirizi, ruqya na tamaa (za kishirikina) ni shirk."
(Abu Dawud 3883)

MASWALI MENGINE KWAKO:
1. Mbona Qur’an inasema jinni wanamuogopa mtu mwenye imani na kumtaja Allah (Surah Al-Jinn 72:1-6)?
Unadhani mtu anayesoma Qur’an kwa ikhlasi anaweza kuitumia kuita majini?
2. Kama Yesu hakuandika hirizi, je, Paulo na makanisa leo yanayoandika “mafuta ya upako” na “maji ya wokovu” si ushirikina wa jina la Yesu?
3. Kama unadai Qur’an ni uchawi, kwanini wachawi wanaiandika kwa kubadilisha maana? Hiyo haithibitishi kuwa Qur’an ni Nuru na wao ni watu wa giza?
4. Kama Qur’an ni uchawi, kwanini watu wanapoisoma kwa ikhlasi wanatulia, wanapona, wanabadilika kitabia? Je, uchawi huleta ucha Mungu?

UNAPASWA KUELEWA KUWA

Qur’an ni Kitabu cha Nuru, lakini kama kitu chema kitatumiwa na mtu mbaya kwa nia chafu — kosa si Qur’an, kosa ni mtu.
Wachawi wanaoitumia Qur’an kwa kuandika majina ya majini, talasim, na hirizi — si wafuasi wa Qur’an, ni Wapingaji wa quraani
Tulia kwanza halafu uje kujadili ,hata kama unatumia CHATGPT,hakikisha haukopi kopi ovyo
 
Tulia kwanza halafu uje kujadili ,hata kama unatumia CHATGPT,hakikisha haukopi kopi ovyo
Hii kichwa ni zaidi ya hicho kidude ulicho kitaja, bado una hoja dhaifu sana juu ya uislamu , endelea kuja na hoja zako na zitajibiwa ipasavyo.
 
YESU BADO ANAOKOA. OKOKENI WAISLAMU MUACHE DHAMBI. MUMKIRI NA KUMPOKEA YESU MIOYONI MWENU KWA IMANI
YESU YUPI SASA ANAEOKOA,YULE ALIEKATANDIKWA NA KUWEKWA MSALABANI AU YUPI?

KAMA ALISHINDWA KUJIOKOA MWENYEWE MSALABANI ATAWEZAJE KUNIOKOA MIMI TENA
 
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Ruqyah?,

Ingawa Waislamu wanadai Ruqyah ni njia ya "kukinga na sihirk", ukweli mchungu ni kwamba sehemu kubwa ya sura zinazotumika (kama Surah Al-Falaq, An-Nas, Ayatul Kursi,Surah Al- Jinn) zinasomwa kwa nia ya kuwasiliana na ulimwengu wa majini.

Mfano,Surah Al-Jinn (Qur’an 72) inasimulia jinsi majini walivyosikiliza Qur’an na kuteka mafundisho. Leo hii, wachawi wengi wa Kiislamu wanatumia aya hizo kwa kujua kuwa majini huelewa lugha hiyo na hujibu miito yao.
View attachment 3426640

“Na tulipomuelekea kwako kundi la majini, kusikiliza Qur’an…” (Qur’an 46:29)

Hii ni hoja hatari sana, kama majini wanaweza kuelekea na kusikiliza Qur’an,

je, si inamaanisha kuwa Qur’an inaweza kuwa mlango wa kuitana kati ya binadamu na majini?

Tuangalie Albadir na Kuomba Mabaya Kupitia Qur’an

Licha ya madai kuwa Ruqyah ni kinga tu, katika vitendo, Waislamu wengi hutumia aya hizo kuomba madhara kwa adui, kulipiza kisasi, au kuleta balaa.

Mfano halisi ni "Albadir", sala maalum inayosomwa kwa kumdhuru mtu. Kuna dua zinazotumia.

Suratul Falaq na An-Nas zikisomwa kwa nia ya kupeleka jinni amtese adui

Aya ya Qur’an 21:69 ("Ewe moto, kuwa baridi kwa Ibrahim") ikigeuzwa kinyume – kuleta joto kwa adui

Surah Taha 69 kuhusu Harut & Marut ikisomwa kwa kutumia “majina ya malaika wa uchawi” ili kufungua mlango wa roho mbaya
View attachment 3426641

➡️ Hii ni dhambi ya kuchanganya maandiko ya kidini na uchawi wa kishetani sawa kabisa na giza lililokatazwa katika Biblia (Kumb. 18:10-12).

🥥 Kombe, Nazi, na Maneno ya Kiarabu ni Uchawi wa Vifaa unaotumika sana

Katika maeneo mengi ya Afrika na Mashariki ya Kati, uchawi wa Kiislamu umetapakaa kupitia

📜 Kombe:

Kombe la glasi hujazwa maji, kisha aya za Qur’an huandikwa kwenye karatasi au kombe lenyewe. Sheikh anasoma Ruqyah juu yake, kisha mgonjwa au mteja huambiwa anywe maji hayo au ajipake. Mara nyingine hutumika kuonyesha picha ya adui kupitia kivuli.
View attachment 3426644

🥥 Nazi:

Hugawanywa vipande vinne au saba, huandikwa majina ya mtu, aya za laana, au majina ya majini kisha kuzikwa, kuchomwa moto, au kutupwa usiku kwa “madhara.”
➡️ Huu ni uganga uliosafishwa na jina la Qur’an!

View attachment 3426646
View attachment 3426647

✍️ Maneno ya Kiarabu:

Katika hirizi, vitambaa, nazi, n.k. huandikwa kwa kalamu surah ya Qur’an, majina ya malaika, na maandiko ya kisiri yanayojulikana na wachache. Mchanganyiko huu huitwa "talasim" (magic squares au maneno yaliyofichwa).
View attachment 3426648
➡️ Hili ni sawa na hirizi ya kishirikina. Inashangaza kuwa Uislamu unaruhusu uandishi wa Qur’an kwenye vitu vya kunywa au kuvaa.

Kuna Vitabu Vinavyofundisha Uganga kwa Kivuli cha Dini

Vitabu vya wanazuoni wa Kiislamu vingi vimejaa mafundisho ya Ruqyah ya kishirikina, mfano

Shams al-Ma'arif (Sun of Knowledge) – kitabu maarufu cha Kiislamu kinachofundisha uchawi, majina ya majini, talismans

Al-Buni's Magic Squares – chati za kutumia aya kwa kuleta pesa, mahaba, au madhara

Hisnul Muslim – ingawa ni kitabu cha dua, kinatumika kama kitabu cha uchawi wa ki-Qur’ani kwa wasioelewa kiroho

Manabii wa kiyahudi waliotumwa na YEHOVA kupitia Biblia wanakataa Matendo Haya ya “Kiroho”

“Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake motoni, wala asiyetabiri kwa kutumia wachawi au mizimu.”
(Kumbukumbu 18:10-12)

“Mungu ni Roho; nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”(Yohana 4:24)

Tofauti na Qur’an inayotumika kama maneno yenye nguvu za ajabu, Biblia inafundisha kwamba nguvu ya kweli inatoka kwa Mungu mwenyewe, si kwa maneno yanayorudiwa kisiri.

Yesu na mitume na manabii haakuwahi kutumia majina ya siri, nazi, wala maandishi ya kisiri.

Yesu alifukuza pepo kwa mamlaka isiyotegemea zana za kidini.

Ruqyah, pamoja na “Aya za Kinga”, ni mfumo wa uganga wa kisasa uliojificha nyuma ya maandiko matakatifu. Hutumiwa:

Kuitana na majini

Kufunga au kulaani adui

Kutengeneza hirizi, maji, nazi, na vyombo vya uchawi

Kupitisha imani za giza chini ya kivuli cha dini

➡️ Hii si ibada ya kweli. Ni ushirikina uliopakwa rangi ya Uungu.
ipo hivyo lakini havifanyi kazi kivile namana NETANYAHU wangemuandika katika nazi zote za duniani lakini wapi na wapi hahahaha YESU NDIO ALFA NA OMEGA
 
nyuzi kama hizi zinazoanzishwa kwa lengo la kutukana, kudhihaki na kukejeli imani au dini za watu wengine ni kwanini Moderator wanaziruhusu? mpaka nafikia umri huu sijawahi kumuona mtu mwenye hali nzuri ya kiuchumi na mwenye kudhihaki imani za watu wengine mara nyingi watu wa aina hii kama mtoa mada huwa ni watu wenye hali ngumu za kiuchumi.....nenda hata kwenye vijiwe watu wanaokaa muda wote wanazungumzia mambo ya dini dini dini kiuchumi huwa wana hali ngumu sana
Sio kashifa mkuu jamaa kaweka na vielelezo, kama kasema uongo njoo ukanushe kwa vielelezo na wewe, ili tujue kama ana kashifu dini ya wengine au kasema uhalisia.
 
Back
Top Bottom