SUWASA yafafanua hoja ya Mdau kuhusu uhaba wa maji Kata za Unyianga na Mtamaa Mkoani Singida

SUWASA yafafanua hoja ya Mdau kuhusu uhaba wa maji Kata za Unyianga na Mtamaa Mkoani Singida

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
MAELEZO KUHUSIANA NA HUDUMA YA MAJISAFI KWA KATA ZA MTAMAA NA UNYIANGA NA MANISPAA YA SINGIDA KWA UJUMLA

Kata za Unyianga na Mtamaa ni mojawapo ya maeneo ambayo yana uhitaji wa kusogezewa huduma ya majisafi katika Manispaa ya Singida na Serikali inatambua hilo na imeshachukuwa hatua stahiki.

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na: Katika kipindi cha muda mfupi, Serikali inatekeleza mradi wa maji wa Visima 900 ambapo Manispaa ya Singida ina visima vitano na kisima kimoja kinachimbwa Unyianga na cha pili kinachimbwa Mtamaa na kazi inaendelea.
WhatsApp Image 2024-12-24 at 14.50.44_243000c6.jpg

WhatsApp Image 2024-12-24 at 14.50.43_3615502e.jpg
Aidha, katika mradi wa majisafi wa Miji 28 ambapo kwa Manispaa ya Singida unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 42, tayari Mkandarasi yupo site na tayari ameshachimba visima Mtamaa B ambapo visima viwili vina uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita 35,000 na 45,000 kwa saa.

Vilevile mradi huo utajenga matenki matano ya maji ambapo tenki mojawapo linajengwa Unyianga baada ya vyanzo kukamilishwa.

Mradi wa majisafi wa Miji 28 kwa Manispaa ya Singida unajumuisha kazi za uchimbaji visima kwa lengo la kuongeza uzalishaji maji kwa siku wa sasa kutoka lita milioni 10.5 hadi kufikia lita milioni 28 kwa siku, ulazaji wa mabomba kwa urefu wa kilomita 55 na ujenzi wa matenki matano ambapo kata za Mtamaa na Unyianga zinanufaika na mradi huu mkubwa na wa kihistoria kwa Manispaa ya Singida.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano - SUWASA
24 Desemba 2024
Pia soma ~ Wananchi wa Unyianga Singida na shida ya maji
 
Ukichora graph ya muda toka uhuru wetu, vs maendeleo, utaona kama taifa kuna namna tumefeli.
 
Ukichora graph ya muda toka uhuru wetu, vs maendeleo, utaona kama taifa kuna namna tumefeli.
Tena tumefeli pakubwa tukisema miaka mnne 4 ya Uwogozi Kuna Mambo mengi yamefanyika lkn Bado hatumkubali ati Kwa Sababu kutoka Zanzibar
 
Back
Top Bottom