Suzuki yangu pasua kichwa

Lyambasa

Senior Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
153
Reaction score
43
Wadau poleni na majukumu.Nina Suzuki Escudo Cc 1590.Matatizo ya gari hii yananichanganya Sana.Kwanza gari inachemsha Sana,Haina nguvu na Sasa inakula mafuta balaa Lita moja kwa km 2.

Pia Sasa imeanza mchezo wa kupasua pipe ya return Cha ajabu hata ukiwasha na kubaki silence tatizo bado lilelile.Wenye changamoto Kama yangu nijuzeni pa kuanzia.

 
Licha ya hayo aliosema mkuu hapo juu kuna swala la cylinder head kupinda, engine block kutoboka, kupinda etc, swala la radiator kutobola, swala la oil cooler kwenye vile vidude vyake vya ndani kupata kutu etc kujua kama cylinder head ina shida weka coolant kwenye radiator halafu washa gari vuta resi ukiona mapovu mapovu kwa juu na maji yanaruka ruka fungua engine kaipime cylinder head kama imepinda kaipige pasi kama imepinda sana weka ingine pima na engine block hio
 
Ahsante kiongozi. Tatizo la kula mafuta nini utatuzi wake.
 
Ahsante kiongozi, Mimi suala la gari kula mafuta tatizo ni mini kiongozi?
Kwanza nikuulize, Je huwa unaongeza coolant kwenye rejeta kila siku? Yaani kila siku ukifungua rejeta unaona coolant imepungua?

Mimi kwa harakaharaka mkuu naweza sema kuna shida kwenye cooling system. Na uwezekano mkubwa ni ECT sensor kuwa kimeo japo ni kama tu huo ulaji wa mafuta unarelate na cooling system. Lakini hapo ni mpaka ipimwe.

Otherwise iangaliwe kwanza kama cyclinder head imepinda, au kama kuna leakage yoyote kwenye cooling system ambayo ipelekea gari kuoverheat.
 
Hapana,mara nyingi huwa naongeza coolant kwenye reserve tank.Mkuu vipi kuhusu kupasuka kwa pipe ya return kunasababishwa na nini?
 
Hiyo gari ni tamu sana, ukiitengeneza vizuri, ni gari ambayo inakubali matengenezo na haisumbui, ningekupa namba ya fundi akusaidie ila naogopa tofali, au njoo pm.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan w jamaa umenifanya niachie kicheko ambacho sikukitaji kabisa kwa siku ya leo. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

mkuu ,hata kuna mzee jirani yangu anahii gari kila siku mbovu mpaka ameshakuwa fundi gereji[emoji1787] japo yeye hajastaafu.
 
mkuu ,hata kuna mzee jirani yangu anahii gari kila siku mbovu mpaka ameshakuwa fundi gereji[emoji1787] japo yeye hajastaafu.
Ila kweli hizi gari zikianza matatizo ya kwenye injini na mifumo ya upoozaji, itakusumbua mpaka utaje jina lako halisi.

Kuna rafiki yangu alikuwa nayo ikaanza matatizo kama hayo akafungua cylinder head na ikapigwa pass ikarudishiwa ikawa sawa.

Akapata safari ya kwenda Ikwiriri ikaenda kufia pale Kibiti, ilipasua hozi ya kupitisha coolant, tukamfata na tukabadili kabisa cylinder head ndo ugonjwa huo wa kuchemsha ukaisha.

Ukaja ugonjwa mwingine wa kutetemeka na miss zisizoisha, alibadili had control box zen akapata kuna fundi fulan hiv anadeal na hzo gari tu ndo ikawa pona pona yake, hata hvyo hakukaa nayo tena alipopata mteja aliiuza faster.

Ndo maana nilipoona comment yako nimecheka sana hadi sasa bado nacheka tu. Tena ngoja nimchek jamaa nimkumbushe ile gar pasua kichwa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo dawa yake jichange,uende kariakoo ukatoe hiyo engine,ufunge nyingine used,sidhani kama hata zinafika 1.5M,this is only if you still love that vehicle,maana kuna watu ni ving'ang'anizi wa magari,yuko tayari hata hiyo gari ifungwe engine ya Toyota lakini lile body hataki kabisa kuachana nalo.
 
Ila kweli hizi gari zikianza matatizo ya kwenye injini na mifumo ya upoozaji, itakusumbua mpaka utaje jina lako halisi...

[emoji23]mkuu, hii gari hapana kabisa aise wazee wengi inawaletea umasikini,jamaa yako alibugi sana aise yani vijana wengi huwa hawanunui hii gari kabisa, huwa ninawaona wazee wanavohangaika mtaani mara ibadili muungurumo ianze kulia kama mashine ya kusaga nafaka ,ikipita kwenye kabonde kadogo tu inatoa kishindo kikubwa mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…