Kuchanja kwa Waislaam ni ibada ! ''Mmeharamishwa (mmekatazwa!) nyamafu (kibudu) na damu (kisusio !) na nyama ya nguruwe, na kinyama kilichochinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kilichokufa kwa kusongeka koo (kunyongwa) na kilichokufa kwa kupigwa na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa kwa kupigwa pembe na alichokila mnyama, ila kama mkiwahi kukichinja kabla hakijafa. Na mmeharamishiwa (mmekatazwa) kilichochinjwa panapofanyiwa ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Na ni haramu kutaka kutaka kujua siri kwa kuagua kwa mabao (kupiga ramli). Hayo yote ni maasia. Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi . Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema Yangu, na nimekupendeleeni Uislaam uwe dini yenu.
''Wanakuuliza wamehalalishiwa nini ? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlichowafunza wanyama kuwinda na ndege wa mawindo. Mnawafunza alivyokufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu; Hakika Mwenzezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. Quran: Al Maida: 3-4.