Mkuu kwanza ujue siuchukii uislamu wala ukristo maana mie sipo huko ila nachukia ile hali ya kunigenisha ama kunisadikisha ama ama kunihalalisha katika dini hizo, chinjeni , kuleni, na wale wasio dini yenu wakichinja waache wale na si lazima achinje muislam ama mkristo ndipo kutakuwa na uhalali wa nyama hiyo, ila kama uhalali kwa muislamu upo katika kuchinja mnyama huyo na muislamu, sawa endelea ial usimlazimishe asiye wa dini hiyo kuamini hivyo, ama kumwambia yeye anaua hachinji! Alafu ujue, ni masuala ya kiafya zaidi hayo na siyo ya kidini.
Kuhusu uasilia wa Mwafrika, umegusia kitu tofauti, nishaeleza, mie naamini dini yangu ya kiafrika, haina kitabu bali ina mafundisho msingi ya nini nifanye na nini nisikifanye, nipo safi kabisa na wala sina tatizo katika hilo, kumbe ninapoongelea hapa naongelea mambo ya msingi na yenye tija, mfano sikatai mtu asivae nguo, asiwe na viwanda, asipande gari ila nitachukia vitu hivi vikitumika vibaya, kwa misingi hiyo, dini kama dini haipo muhimu kiasi hicho mpaka kuleta chuki, vita, kutengana na hata kuuana, dini siyo itakayokupeleka mbele ya haki ila maisha yako ya upendo, amani na umoja ambao ni tunu za Uasilia wetu , pale dini inapokuletea matatizo na hasa kama ni kitu ambacho huna asili nacho basi ujue ni tatizo na ndipo hapo inakuwa haina umuhimu wa kulinganishwa na umuhimu kama wa kuvaa nguo, ama nguo umeshaona zinaleta matatizo?Kubadilika kutoka kuvaa magome ya miti mpaka nguo ni hatua ya maendeleo ambayo ingefikiwa tu hata kama wakoloni hao wasingekuja, wazee wetu walishapiga sana hatua mpaka hapo. Uasilia wa Mwafrika unaufahamu sana ila tatizo ni hili hali tuliyogenishwa na kuona asili yetu kama ushirikina ama kutokuwa wa maana, bado narudia, dini hizi za vitabu zisitufanye tukose amani ama kuchukiana, na hili ndilo silitaki,kila mtu aamini anachoamini bila kujiona kwamba ana kibali cha kufanya kwaajili ya wengine hasa linapokuja suala la kichinja mnyama ambalo kwangu mimi naona ni dogo sana ambalo haliitaji watu kutoleana misuli, lingekuwa hivyo/litakuwa hivyo kama kuna kundi litalazimisha iwe hivyo. Alafu ujue wenyewe wakoloni wa hizo dini wametulia na mengi wameshaona hayafai sisi bado tunang'ang'ania kwa kujifanya tunazijua na hili ndilo tunatakiwa kulijua.