Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Watu wengi wakiulizwa maswali kama hayo huwa hawajui ku reject the premise.Hiyo falsafa kubwa sana ni ipi hapo?
Nilichokiona mimi ni kwamba Nyerere alitumia tu common sense ya kawaida ambayo mtu mwingine yeyote mwenye akili za kawaida, naye angesema vivyo hivyo, pengine labda kwa kutumia maelezo na mfano tofauti lakini maudhui yakawa ni yaleyale.
Mporaji yeyote wa mali ya mtu hana haki ya kumpangia chochote huyo aliyempora hiyo mali yake.
Hicho ndicho Nyerere alichokisema, kimsingi.
Utamporaje mtu koti lake halafu uanze kumpangia mambo kuhusu hilo koti?
Wewe mporaji hukuwa na huna haki ya kumpora mtu mali yake.
To me thatβs just basic common sense. I donβt see it as being a big time philosophical idea.
Just a basic moral compass issue.
However, the example he [Nyerere] gave was very easy for anybody to understand.
Kungekuwa na temptation ya kuonesha kuwa tumejiandaa, tutaweza. Nyerwre angeweza jusema tupo tuliosoma nje tutaongoza nabkusomesha wengine. Lakini hakusema hivyo.
Nyerere rejected the legitimacy of the question.
Ukiielewa hiyo falsafa, ni jambo dogo lakini la msingi sana.
Usipoielewa, ndiyo mpaka mwaka huu 2024 unaona watu wanajiuliza wanashindwa kuelewa. Wengine mpaka leo bado hawamuelewi Nyerere.
Ni falsafa kubwa iliyowapita wasioielewa, halafu ni ndogo sana kwa wanaoielewa.
Ni kama wewe unavyoweza kuona kusema sentensi ya Kiingereza ni kitu kidogo sana, kwa sababu unakijua. Lakini kwa asiyekijua, ni kitu kigumu.
Kuna siku nilikuwa nawaelezea watu, wengine supposedly wasoni kabisa, the logic of elimination method katika kupata majibu ya hesabu. Wale watu wengine walikuwa hawanielewi kabisa. Narudia kwa mfano wa jinsi unavyoweza kufanya elimination ku converge kwenye jibu kutafuta jibu la square root, wale watu wengine bado walikuwa hawanielewi.
Mpaka leo najiuliza, kwa nini watu wengine wanakuwa na shida sana kuelewa mantiki ndogo tu kwangu, halafu wengine wanaelewa kwa urahisi kabisa.